Monday, March 11, 2013

SIMBA YAMPIGA MDOGO WAKE COAST UNION 2-1 TAIFA

 Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa, (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Coastal Union, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, leo. Katika mchezo huo Simba imeshinda mabao 2-1, bao la kwanza likifungwa na Mrisho Ngasa, katika dakika ya 45+4 na bao la pili likifungwa na Haruna Chanongo katika dakika ya 45+4. Bao la kufutia machozi la Coastal Union, limefungwa na Razack Khalfan, katika dakika ya 49. 


Katika hali isiyokuwaa ya kawaida timu ya Simba ilichelewa kuingia uwanjani dakika tano hali iliyofanya mashabiki wa timu hiyo wapigwe na butwaa lakini wakati timu zinakaguliwa, Simnba iliingia uwanjani ikitanguliwa na wachezaji wawili, ambao kipa Abel Dhaira na Abdallah Seseme ndiyo waliosalimiana na wapinzani wao na wachezaji wengine waliingia uwanjani wakati Coastal wakiwa tayari wamejipanga uwanjani. 

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba, kilieleza kuwa sababu ya kuchelewa imetokana na kuzuiliwa katika hoteli ya Safaya iliyoko maeneo ya Kariakoo walikoweka kambi ambayo inadaiwa kuwa wana deni la Sh 35 milioni zilizotokana na kambi ya timu hiyo toka mzunguko wa kwanza.

 Kutokana na kitendo hicho Simba inakabiliwa na adhabu kutoka kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwani kanuni za Ligi Kuu Bara kuwa timu inatakiwa kuingiwa uwanjani saa moja kabla ya mchezo kuanza.
 Haruna Chanongo, akijiandaa kupiga shuti mbele ya mabeki wa Simba.
 Mrisho Ngasa, akiwachachafya mabeki wa Coastal Union

No comments:

Post a Comment