Tuesday, March 12, 2013

RAILA ODINGA APINGA MATOKEO YA URAIS KENYA APELEKA KILIO CHAKE MAHAKAMANI

Raila Ondiga
Mgombea wa Urais Kenya Raila Odinga amepinga matokea ya Uchaguzi yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo na kuyaita matokeao ya njama yaliyopangwa makusudi kuvuruga uchaguzi wa Urais Kenya.
Kutokana na matokeo yaliotangazwa  na tume ya uchaguzi ya kumpa ushindi Uhuru Kenyatta aliwashukuru wapiga kura kwa kujitokeza kwa wingi na aliishutumu tume kwa kushindwa kufanya maamuzi ya haki na kufanya madudu katika kuhesabu kura.
Aliendelea kusema serikali imetumia mamilioni kununua vifaa vya kisasa vya kuandikisha na kuhesabia kura lakini cha ajabu vifaa vilishindwa kufanya kazi na kusababisha kura kuhesabiwa upya kitu kilichofanywa kwa makusudi ili kupanga matokeo. Kamwe mimi na wafauasi wangu hatukubaliani na matokea na ili haki itendeke tutaelekea mahakamani na alimalizia kwa kusema mvumilivu ula mbivu kwa hiyo ndugu zangu tuvumilie tusubili maamuzi ya mahakama, asante kwa kunisikiliza

No comments:

Post a Comment