Tuesday, January 30, 2018

RAIS JOHN MAGUFULI KUZINDUA PASIPOTI YA ELEKITRONIKI.


Jonas Kamaleki- MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli kesho atazindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo utafanyika Jumatano, Januari 31, 2018 kuanzia saa moja na nusu asubuhi, Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Mrakibu wa Uhamiaji ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda katika mahojiano maalum na Idara ya Habari (MAELEZO).
Mtanda amesema kuwa Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki ni sehemu ya Mfumo wa Uhamiaji Mtandao ambao utakuwa na visa, vibali mbali mbali na manejimenti mipakani.
Kwa kuwa teknolojia inazidi kukua, Tanzania haiwezi kubaki nyuma ndiyo maana imeamua kuingia katika masuala ya digiti.
Uzinduzi huu utahudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.
Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waheshimiwa, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wa Serikali wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo kwa mujibu wa Mtanda.
Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika kutoa huduma zake kwa wananchi kwa njia ya mtandao. Ikumbukwe kuwa usajili wa makampuni chini ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamezindua usajili wa makampuni kwa njia ya mtandao, miamala ya pesa inafanyika kwa kiwango kikubwa kwa njia ya mtandao na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwepo kulipa kodi mbali mbali.

RAILA ODINGA AJIAPISHA KUWA RAIS WA KENYA.



Raila aondoka uwanja wa Uhuru Park


Punde tu alipofika na 'kula kiapo' Raila Odinga ameondoka.
Wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu na ghamu, bila kutegemea kwamba atachukua muda mfupi hivyo.
Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ' si mapinduzi ya serikali'
Raila 'akula kiapo'

Odinga akula kiapo uwanja wa Uhuru Park

Raila Odinga amefika katika pamoja na viongozi kadha wakuu wa NASA na kujiapisha akishika Biblia.
Amewaambia kuwa mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper ataapishwa baadaye.
Viongozi wengine wenza wa Nasa Moses Wetangula na Musalia Mudavadi pia hawakufika katika wuanja huo.
Bw Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya.
"Hatua ya leo ni kuelekea kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya"
"Maelekezo mengine mtayapata baadae"

Bw Raila Odinga amezungumza na kituo cha habari cha KTN kwa njia ya simu ambapo amesisitiza kwamba Rais Uhuru Kenyatta hakuchaguliwa kwa njia halali.
Alipoulizwa anni atamwapisha, amesema: "Ngoja uone” na akasisitiza kwamba wanachokifanya leo kina msingi wake katika sheria na si mapinduzi.
“Hatutambui uchaguzi wa Oktoba 26 (uchaguzi wa marudio ambao Odinga alisusia), zaidi ya asilimia 86 ya Wakenya hawakushiriki. Tuna serikali ambayo si halali ambao inajidai kuwa mamlakani,” amesema.
Kuhusu taarifa kwamba amepokonywa walinzi, amesema: "Walinzi wangu waliondolewa muda mrefu sana uliopita. Najihisi kuwa hatarini ndio lakini watu raia ndio usalama wangu.”
Bw Odinga ameitaka serikali kutotumia nguvu kuusambaratisha mkutano wa leo.
"Wafuasi wangu wamo safarini kuelekea Canaan. Safari yetu ni halisi na haiwezi kuzuiwa.


  • Raila Odinga azungumza na vyombo vya habari dakika chache kabla ya kuelekea ‘kuapishwa’.
    Akizngumza kwa njia ya simu na kituo cha habari cha KTN, Odinga amesema kuwa hawakutarajia kufungwa kwa vyombo vya habari.
    Ni hali ya ‘kusikitisha’ na ‘inaonesha kuwa tumefika kiwango cha Uganda.'
    Alipoulizwa nani haswa atamuapisha, Odinga alijibu ‘ngoja uone.’
    Alielezea kuwa shughuli yao ni halali na haikiuki katiba. Pia amesema haamini kwamba wanachokifanya si mapinduzi ya serikali.

    MH RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE JAKAYA KIKWETE AKIWA ADDIS ABABA ETHIOPIA.

     Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu  Mstaafu wa Lesotho Mhe. Tom Thabane.
     Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Rais wa Zimbabwe Mhe Emerson Mnangagwa.
     Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete na akiwa na Rais Zuma wa Afrika Kusini
     Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na akiwa na Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dkt. Thomas Kwesi Quartey.
     Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na akiwa wake za waasisi wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika. kushoto kwake ni Mama Maria Nyerere na kulia kwake ni Mjane wa Hayati Rais Obote wa Uganda..
    Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na Rais wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina 
    Rais Mstaafu na Mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika Usulihishi wa Mgogoro wa Libya, Dkt. Jakaya Kikwete katika taswira mbalimbali akiwa Addis Ababa, Ethiopia katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika