Wednesday, January 28, 2015

MWENYEKITI WA CUF PROF:IBRAHIM LIPUMBA APANDISHWA KIZIMBANI

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, akiwa kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo mchana wakati alipofika kusomewa shitaka la kesi yake ya jinai kwa kuwashawishi wafuasi wake kufanya fujo baada ya kutiwa mbaroni jana alipokuwa akiongoza maandamano ya wanachama wa CUF.
Prof. Lipumba akiwa kwenye kizimba cha mahakama tayari kusomewa shitaka linalomkabili.
Wafuasi wa CUF, wakiwa nje ya Mahakama hiyo wakimsubiri mwenyekiti wao....
Gari za Polisi zikiwa tayari nje ya Mahakama hiyo kukabiliana na vurugu ambazo zingejitokeza....huku wakiimarisha ulinzi.
Prof. Lipumba akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupata dhamana na kutoka nje ya Mahakama hiyo.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAFANYABIASHARA JONSON MINJA KIZIMBANI.

  
NA John Banda,Dodoma
MWENYEKITI wa Shirikisho la vyama vya Wafanyabiashara Nchini Jonson
Minja  amefikishwa Mahakama ya Mkoa wa Dodoma kwa Mashitaka mawili
ikiwemo la kuchochea Wafanyabiashara  wasilipe kodi ya Serikali.
Akisoma Mashitaka hayo Wakili wa Serikali Gogfrey Wambari mbele ya
Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Rebbeka Mbiru alisema mtuhumiwa alitenda
makosa hayo tarehe 6 Septemba 2014 alipokuwa katika mkutano na
Wafanyabiashara katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.
Wambari alisema Mtuhumiwa alitenda makosa mawili ya Kushawishi
Wafanyabiasha kutenda kosa la jinai na kosa la pili kuzuia ukusanyaji
wa Kodi kwa kutumia Mashine za Kielotroniki EFD.
‘’Kifungu cha 390 kinasomeka pamoja na kifungu cha 35 cha Sheria ya
adhabu sura ya 16 ni  kosa kushawishi vitendo vyovyote vya jinai’’
‘’Kifungu cha 107 kifungu kidogo C cha Sheria ya kodi sura ya 332 ya
mwaka 2004 ni kosa kuzuia ulipaji wa Kodi ya Serikali ‘’alisema
Wambari.
Aidha Wambari alimtaka Hakimu kuzingatia umbali wa anakoishi mtuhumiwa
wakati atakapokuwa akitoa masharti ya dhamana.
Kwa upande wake Mtuhumiwa wa Kesi hiyo Jonson Minja 34 alipoulizwa
makosa hayo na Hakimu alikana mashitaka yote.
Hata hivyo hakimu wa Mahakama hiyo Rebbeca Mbiru alitoa masharti ya
dhamana ya Mtuhumiwa kwa kusema kuwa anatakiwa awe na Wadhamini wawili
mmoja wapo akiwa mtumishi wa Serikali na wote wawili wawe na vitu

Mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyabiashara Jonson Minja mwenye koti
akisindikizwa katika mahakama ya mkoa wa Dodoma Chini ya ulinzi wa
askari polisi.

Saturday, January 24, 2015

SOMA ALICHOKISEMA PROF. MUHONGO ALIPOTANGAZA KUJIUZULU.

Na Chalila Kibuda, Dar
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhuongo, amejiuzulu wadhifa huo kutokana na kuchoshwa na sakata la Akauti ya Tegeta Escrow.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Barabara ya Samora, Profesa Sospeter Muhongo amesema ameamua kujiuzulu ili kuwa sehemu ya suluhisho la suala la akaunti ya Tegeta Escrow.

Aidha Muhongo alisema kuwa suala la ankauti ya Tegeta Escrow limekuwa likizungumzwa na kufanya mambo mengine yasiendelee na huku watanzania walio wengi ni masikini wakihitaji umeme na sio kuuliza tegeta Escrow.

"Suala hili mimi nililikuta toka mwaka 2012 na sijaweza kuchukua fedha katika ankauti ya Tegeta Escrow, mimi sio mla rushwa, mimi sio mwizi na hakuna mtu yeyote anayeweza kunipatia rushwa, 

“Akaunti ya Tegeta Escrow ilitawaliwa na mvutano wa kisiasa, kibiashara, ubinafsi, uongozi na madaraka sasa watu wakae kujadili masuala mengine hata bunge litumie muda kujadili mambo  mengine  pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatumia muda mwingi kujadili suala la Escrow.

Hivyo nimeamua kujiuzulu nafasi ya uwaziri ili niweze kuwa sehemu ya bunge na kuendelea kuchangia katika masuala ya maendeleo kwani suala la escrow sio suluhisho kwa watanzania". Alisema Muhongo

Muhongo alisema kuwa anashukuru sana kwa kushirikiana vizuri na makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na baraza la mawaziri.

Aidha alisema kuwa kuchelewa kujiuzulu alitaka wananchi wajiridhishe pamoja na kumalizia kazi zingine ambazo zilikuwa mezani kwake ili zikamilike hivyo asingeweza kufanya halaka kwani anajiamini kuwa ni mchapakazi na muadilifu

HIKI NDICHO ALICHOKIFANYA RAIS KIKWETE ATEUA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI KWA MARA YA 4 NDANI YA MIAKA 10

By Ombeni Sefue:.
Mabadiliko ya Mawaziri
.Mawaziri wawili wamejiuzulu
i) Ardhi-Tibaijuka
ii)Nishati na madini-Sospeter Muhongo
Walio teuliwa
1. George Simbachawene- Waziri Nishati
2.Mary Nagu-Waziri wa Nchi mawasiliano na Uratibu
3.Christopher Chiza-Waziri uwezeshaji na Uwekezaji
4.Halson Mwakyembe-Ushirikiano wa afrika mashariki
5.Lukuvi-Ardhi Nyumba na Makazi
6.Steven Wasira-Kilimo chakula na Ushirika
7.Samwel Sitta -Wizara ya Uchukuzi
8.Jenista Muhagama-Sera na uratibu wa Bunge

MANAIBU Waziri
Masele -OMR Muungano
Kairuki -  Ardhi
Ummy - Katiba na Sheria
Anna Kilango- Elimu
Mwijage - Nishati

Tuesday, January 20, 2015

CCM HAITARUHUSU WANUNUA URAIS 2015 WAPAMBE WAO WANAOENEZA TAARIFA ZA UONGO KUADHIBIWA.


 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari, Katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibara asubuhi hii, kuhusu moja ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM, ya kuwataka wanaotaka kuwania urais kupitia CCM na wapambe wao kuacha kueneza taarifa za uongo kwenye vyombo vya habari na kwamba atakayebainika kufanya hivyo atachukulia hatua kali za kinidhamu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisisitiza jambo katika mkutano huo na waandishi uliofanyika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Znzibar asubuhi hiii.
……………………………………………………………………
Mwaka huu 2015 ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano. Hii ni kwa mujibu wa katiba ya nchi. Ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM kwa nafasi hizo haijatolewa bado.

Itakumbukwa Kamati Kuu iliyopita ya tarehe 13/01/2015, iliyoketi Kisiwandui Zanzibar ilipitisha ratiba ya shughuli za kawaida za Chama kwa mwaka 2015 na kupanga kushughulikia ratiba ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wa CCM vikao vijavyo.

Pamoja na kutotolewa kwa ratiba hiyo, bado zimekuwepo harakati nyingi za wanaotaka kuteuliwa na CCM kugombea nafasi mbalimbali hasa ya urais wa Jamhuri ya Muungano. Harakati hizo baadhi halali, nyingi haramu.

Pamoja na kutaadharishwa mara nyingi juu ya madhara ya harakati hizo kwa umoja na mshikamano wa Chama bado baadhi yao wamekuwa wakiendelea na harakati hizo.

Kwa muda sasa kumekuwepo na uzushi mwingi juu ya baadhi ya wanaotaka kuwania nafasi hizo kujadiliwa na hata kuchukuliwa hatua na vikao vya chama. Maneno haya kwa sehemu kubwa yamekuwa yakisambazwa na wagombea wenyewe au wapambe wao.

Uzushi huu, hauna nia njema kwa CCM, unalengo la kukigawa Chama na kuonyesha kama vile Chama hakina kazi nyingine ila kujadili na kushughulika na watu hao. Kwa mara nyingine CCM inapenda kuwataadharisha wagombea hao na wapambe wao kujiepusha na kusambaza taarifa zisizokuwa za kweli. Kwa kuwa vitendo hivi vinakigawa Chama chetu.

CCM haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya wote wanaosambaza taarifa hizi. Ni vyema wagombea wakawadhibiti wapambe wao na wakajichunga wenyewe dhidi ya hujuma hizi kwa Chama kwani zitawapotezea sifa ya kugombea.

Wengi wa wanaosambaza taarifa hizi ni wagombea au wapambe wasiojiamini kutokana na matendo yao, ambayo hata wao wana mashaka na uadilifu wao. Hatuoni sababu ya mgombea anayefuata sheria, kanuni na taratibu za Chama kuhofia kuchukuliwa hatua kila vikao vya Chama vinapofanyika.

Ukitenda kwa haki huna haja ya kuogopa vikao na kuzusha uongo na uzushi usio na ukweli. CCM inaamini matendo haya hayatajirudia.

Aidha Chama Cha Mapinduzi kinawaomba wanachama na wananchi kuzipuuza taarifa zinazosambazwa kwa kuvinukuu vyanzo visivyo rasmi, kama kuna hatua au taarifa kwa umma juu ya hatua yoyote katika mchakato huu basi itatolewa na wasemaji halali wa Chama na si kutoka vyanzo vya barabarani.

Itakumbukwa pia baada ya Kamati Kuu iliyopita kukutana tulitangaza kufanyika kwa kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili kwa ajili ya kushughulikia masuala ya kimaadili kwenye sakata la Escrow kwa viongozi wa Chama walioko kwenye vikao vya Chama vya maamuzi.

Jana kumekuwepo na harakati nyingi za vyombo vya habari na watu binafsi kujaribu kupata taarifa ya nini kimetokea kwenye kikao hicho cha Maadili.

Tunapenda kuwakumbusha kuwa kwa mujibu wa taratibu taarifa za kilichotokea kwenye kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili huwa hazitolewi kwa umma mpaka baada ya kufikishwa kwenye Kamati Kuu. Hivyo basi tunawaomba kutulia na kusubiri taarifa rasmi baada ya kufikishwa kwenye Kamati Kuu kuliko kuhangaika sasa hivi, jambo linaloweza kusababisha kuokotwa kwa habari za barabarani ambazo nyingi si za kweli. Tulieni subirini taarifa rasmi. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na;- Nape Moses Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi. 20/01/2015

Monday, January 19, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AHUDHURIA SHEREHE ZA KUSIMIKWA ASKOFU MKUU JIMBO LA DODOMA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Beatus Kinyaiya baada ya kusimikwa rasmi kwenye  Sherehe iliyofanika jana Januari 18, 2015 katika Kanisa la Mt. Paulo wa Msalaba Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Sherehe ya Kumsimika Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Beatus Kinyaiya iliyofanyika katika Kanisa la Mt. Paulo wa Msalaba Dodoma
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu mbalimbali waliohudhuria sherehe ya kusimikwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Beatus Kinyaiya kwenye  Sherehe  iliyofanika katika Kanisa la Mt. Paulo wa Msalaba Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Beatus Kinyaiya baada ya kusimikwa rasmi kwenye  Sherehe iliyofanika katika Kanisa la Mt. Paulo wa Msalaba Dodoma

Wednesday, January 14, 2015

WANAFUNZI 84 WA UDOM WATIWA MBARONI KWA KUHAMASISHA MAANDAMANO MJINI DODOMA.


 Baadhi ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa kwenye gari ya polisi baada ya kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma leo.
Baadhi ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa chini ya ulinzi kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma leo.

Monday, January 12, 2015

kashfa nzito morogoro:MAMA AJIFUNGUA MANESI WATUMBUKIZA MTOTO KWENYE NDOO.


Manesi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wameingia kwenye kashfa nzito ya kusababisha kifo baada ya kudaiwa kumtumbukiza mtoto mchanga kwenye ndoo kwa zaidi ya saa 3.
 
Katoto kachanga kalikotumbukizwa kwenye ndoo kwa zaidi ya saa 3.

Tukio hilo ambalo kwa sasa ni gumzo mkoani hapa lilijiri hivi karibuni ambapo mwanamke aitwaye Zainabu lsmali, mkazi wa Kididimo jirani na Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine ‘SUA’ alishikwa na uchungu wa kujifungua na kukimbizwa katika hospitali hiyo kwa msaada wa jirani yake aliyejitambulisha kwa jina la Mama Sira Manga.
Ndoo iliyotumika.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juu ya tukio hilo, Mama Manga alikuwa na haya ya kusema: “Huu ni uzembe mkubwa wa manesi. Tulipofika hospitali mtoto alizaliwa akiwa hai lakini alikuwa njiti kwani alikaa tumboni kwa mama yake miezi 7 badala ya 9.
Ndugu wa mama akiwa na mtoto huyo.
“Cha ajabu usiku huo manesi baada ya kumcheki mtoto walisema ni wa kike lakini eti walidai amekufa hivyo waliamua kuchukua matambara ya mzazi yaliyotumika kujifungua na kumzoa mtoto huyo na kumuweka kwenye ndoo ambayo kwa kawaida sisi wazazi huwa tunakwenda nazo leba.
“Walituambia tukazike, unajua kutoka hospitali hadi Kididimo juu ya Milima ya Uluguru ni mbali na gari lilichelewa kutufuata hivyo mtoto huyo alikaa kwenye ndoo zaidi ya saa 3.
Mama wa mtoto huyo, Zainabu lsmali
“Tulipofika nyumbani na kumtoa mtoto kwenye ndoo tukamuona anahema na kufumbua macho baada ya kumtingisha akakohoa ndipo tukamkimbiza tena hospitali.
Pamoja na jitihada za manesi hao, kesho yake mtoto huyo alifariki dunia baada ya kitovu chake kuingiza hewa kwani kilikuwa bado hakijakatwa.
Baba wa mtoto huyo, Haji Kondo.
Mama wa mtoto huyo, Zainabu alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema:
“Roho inauma sana lakini mzungumzaji wa tukio hilo ni mume wangu.”
Baba wa mtoto huyo, Haji Kondo alipohojiwa na mwandishi wetu alisema: “Ni kweli nimempoteza mwanangu lakini nisingependa kutoa lawama kwa manesi kwani mke wangu bado anaendelea kuzaa.”
Mwandishi wetu alifika hospitalini hapo na kuzungumza na daktari mfawidhi, Dokta Rita Lyamuya ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Daktari mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dokta Rita Lyamuya.
“Ni kweli tukio hilo limetokea kwenye wodi yetu ya wazazi.
“Manesi walitimiza jukumu lao la kumhudumia mzazi lakini kwa bahati mbaya tuna changamoto ya umeme kukatika bila taarifa hivyo wakati manesi wakimzalisha alijifungua mtoto njiti.
“Ghafla umeme ulikatika na kutokana na giza, manesi walijua mtoto amekufa hivyo waliwaeleza wanandugu kwamba mtoto amefariki dunia.
“Ndugu walimchukua walipofika kwao na kukitoa kwenye ndoo walibaini mtoto bado yupo hai.
“Walimleta tena hapa hospitali na tulifanya juhudi za kumtibu lakini kwa bahati mbaya amefariki dunia

PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO YA SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.


 Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia Mkono wananchi wakati alipowasili katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha Sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika leo.
 Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama leo wakati wa  Sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar akifuatana na Paredi Kamanda Luteni kanali Mohamed Khamis Adam  katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika leo katikauwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za kilele cha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika kilele hicho Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Wafanyakazi wa Ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ wakipita mbele ya jukwaa kwa maandamano wakati wa sherehe za Kuadhimisha miaka 51 ya mapinduzi ya Zanzinar akiwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati akiwasili uwanjani hapo.
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif.
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
 Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mkuu wa majeshi....
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Shein wakati akiwasili uwanjani hapo na baada ya kukagua gwaride la heshima.
Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Rais wa Zanzibar, Dkt. Shein.

Tuesday, January 6, 2015

POLISI WAFYATUA MABOMU KUZIMA VURUGU WAKATI WA ZOEZI LA KUAPISHWA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM


Polisi Jijini Dar es Salaam wamelazimika kufyatua risasi hewani na kufyatua mabomu ya machozi kufuatia kuibuka kwa vurugu katika hoteli ya Land Mark ambapo shughuli ya uapishaji wa wenyeviti wa serikali Mitaa zinafanyika.
Vurugu hizo, zimeibuliwa na kambi ya upinzani ambayo imelalamikia kuwa Mwenyekiti mmoja wa Chama tawala CCM aliyeapishwa hakuwa ameshinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika mwaka jana.