Tuesday, February 24, 2015

KITUO CHA POLISI PAMOJA NA MAGARI VYACHOMWA MOTO NA WANANCHI HUKO ILULA MKOANI IRINGA BAADA YA POLISI KUTAKA KUKAMATA MUUZA POMBE ZA KIENYEJI

Hapa wananchi wakiwa wameziba barabara kwa Mawe na kwa kuchoma moto matairi katikati ya barabara
Kuna vurugu kubwa ambayo inaendelea hivi sasa kwenye mji mdogo wa Ilula  

Tuesday, February 17, 2015

MHE. CHIKU GALLAWA AKAGUA UJENZI WA MAABARA MANISPAA YA DODOMA, AMUAGIZA MKURUGENZI KUWACHUKULIA HATUA WATENDAJI WANAOSHINDWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA MAABARA

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (mwenye kilemba kichwani) akimsikiliza Afisa Mtendaji wa Kata ya Msalato Dodoma  Ndg. Herman Malindira (kulia) akiwasilisha taarifa ya mradi wa ujenzi maabara kwenye sekondari ya Chikole Feb. 16, 2015.
 Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) akitoa maagizo kwa viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Msalato baada ya kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa maabara wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015.
 Mhe. Chiku Gallawa (katikati) akionesha kutokuridhishwa na hatua ya ujezi wa maabara kwenye sekondari ya Miyuji inayojengwa na Kata za Miyuji na Mnadani ikiwa hatua ya msingi wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015, Amemuagiza Mkurugenzi Manispaa ya Dodoma kuwachukulia hatua watendaji wote walioshindwa kusimamia ujenzi wa maabara.
 Mhe. Chiku Gallawa (katikati) akiwaagiza viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Chamwino kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa maabara sekondari ya Chinangali ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili, Mhe. Gallawa ameonesha kutokuridhika na ujenzi wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015 na kukuta maabara ik kwenye hatua ya ujenzi wa msingi.
Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) akiwaagiza viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Chang’ombe kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa maabara sekondari ya Lukundo ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili, Mhe. Gallawa ameonesha kutokuridhika na ujenzi wa Maabara Manispaa ya Dodoma wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Feb. 16, 2015.

Monday, February 16, 2015

SASA WATAKOMA KIKOSI CHA JWTZ CHATINGA TANGA RASMI HAO WANAOJIITA MAGAIDI KUWASHIKISHA ADABU.

Jeshi la wananchi kwa kushirikiana na polisi nchini limeongeza askari wa vikosi vya ardhini katika zoezi la kukabiliana na vikundi vinavyodaiwa kuwa vya kigaidi katika mapango ya mleni yaliyopo eneo la amboni jijini Tanga kufuatia askari wa jeshi la wananchi kuuawa kwa risasi huku wengine wakijeruhiwa katika mapigano baina yao na vikundi hivyo.

ITV imeshuhudia msafara wa magari ya kijeshi pamoja na yale ya maofisa wa kijeshi na huduma ya kwanza yakipita katika barabara kuu itokayo Tanga kwenda Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania kisha kuingia katika njia iendayo katika mapango yaliyodaiwa kuwa ni sehemu maalum ya maficho ya vikundi hivyo vya kigaidi na msemaji wa polisi kamishna wa polisi -operesheni Paul Chagonja kutwa nzima simu yake iliita bila majibu lakini msaidizi wake alipoke na kudai kuwa bosi wake yupo kwenye kikao.
 
Hata hivyo baadhi ya familia zilizopo katika eneo la Mleni zinadaiwa kuhamisha makazi kufuatia milipuko ya risasi na silaha nzito za kijeshi zilizokuwa zikirindima katika kipindi cha siku mbili nyakati za mchana na usiku, hatua ambayo baadhi ya makundi ya vijana yanaojihusisha na kazi ya kupasua mawe katika mapango hayo kulalamikia ukosefu wa kazi kwa sababu ya mapigano hayo ambayo pia yamewapa hofu na maisha yao.
 
Baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga wameshauri mapango hayo yaharibiwe kwa kutumia vifaa maalum vya kivita na jeshi la polisi lisahau suala la silaha zao zilizoibwa katika matukio tofauti na makundi hayo.

Sunday, February 15, 2015

KUTOKA AMBONI TANGA POLISI YATOA TAMKOA HALI NI SHWARI, ASKARI WA JWTZ AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI.


Baadhi ya magari ya Polisi yakiwa kwenye moja ya barabara ya kuelekea Mapango ya Amboni, wakati wa Doria maalum iliyoanza jana baada ya eneo hilo kuvamiwa na waliodaiwa kuwa ni Magaidi wa Al- Shabaab. Hata hivyo Polisi Mkoa wa Tanga leo imetoa tamko kuwa hali katika mapango hayo ni shwari baada ya kufanikiwa kuwatimua watu hao walioonekana kutimkia mpakani mwa nchi ya Kenya.
Sehemu ya mawe ya Msitu wa Amboni...
Baadhi ya askari Polisi wakiwa katika doria, ambapo imeelezwa kuwa jumla ya askari wanne wamejeruhiwa katika tukio hilo na askari mmoja wa JWTZ alifariki dunia baada ya kupigwa risasi ya tumbo

BARAZA LA BIASHARA MKOA WA DODOMA LASISITIZA USHIRIKIANO BAINA YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI ILI KUONGEZA FURSA ZA UWEKEZAJI NA KUKUZA UCHUMI WA DODOMA


 Mkuu wa Mkoa Dodoma na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akitoa hotuba ya kufungua mkutano wa baraza hilo Mjini Dodoma juzi 
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) Raymond Mbilinyi akiwasilisha majukumu ya Baraza hilo katika kusaidia mabaraza ya biasara ya Mikoa na jinsi ya kukuza ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi wakati wa mkutao wa baraza la biashara Dodoma lililokutanisha viongozi wa  wafanayabiashara wa chini na juu
 Wajumbe wa baraza la biashara Mkoa wa Dodoma wakifuailia mada juu ya ushirikiano wa serikali na sekta binafsi na kuzalisha fursa za uwekezaji Mkoani Dodoma wakati wa Mkutano wa Baraza hilo  

 Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogowadogo (wamachinga) Manispaa ya Dodoma Nobert Donald akiwasilisha changamoto zinazowakabili wamachinga mbele ya wajumbe wa mkutano wa baraza la biashara Mkoa wa Dodoma  
Mwenyekiti wa wafanyabiashara, wakulima na wenyeviwanda Mkoa wa Dodoma (TCCIA) Faustine Mwakalinga akiwasilisha mada juu ya fursa za kipekee za uwekezaji katika Mkoa wa Dodoma na Changamoto zilizopo wakati wa Mkutano wa Baraza la Biashara Mkoa wa Dodoma

Tuesday, February 3, 2015

RAIS WA UJERUMANI ATEMBELEA KANISA KUU LA KILUTHERI LA AZANIA FRONT JIJINI DAR ES SALAAM

 Muonekano wa Kanisa la Azania Front
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa (kulia), akimkaribisha Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck alipofika kutembela kanisa hilo Dar es Salaam leo jioni.
 Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck akisalimiana na Mama Anna Mkapa baada ya kuwasili kanisani hapo.


 Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck (katikati), akisaini baada ya kufika kanisani hapo.
 Wanakwaya wakitumbuiza.


 Askofu Malasusa na Rais wa Ujerumani, Gauck wakiteta jambo.
Rais Gauck akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo pamoja na waumin

RAIS WA UJERUMANI JOACHIM GAUCK ALIPOWASILI NCHINI JANA USIKU


Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  akishuka kwenye ndege akiambatana na mkewe Bi. Schadt wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana usiku jijini Dar es salaam.
Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakifurahia jambo walipokuwa wakitazama vikundi mbalimbali vya burudani vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Rais huyo uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jana usiku jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiwa mwenye furaha mara baada ya kumpokea Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  na Mkewe Bibi Schadt (walioshika maua), uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  akiwa na mkewe Bi. Schadt  na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakitazama vikundi mbalimbali vya burudani wakati wa mapokezi ya Rais huyo wa Ujerumani uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana usiku jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kumpokea Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck wakiwa na nyuso za furaha. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
**************************
Na. Aron Msigwa -MAELEZO.
Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na msafara wake amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu majira ya saa 2.40.
Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo akiwa ameambatana na mkewe Bibi Schadt  amelakiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilali pia mapokezi ya burudani za ngoma za asili kutoka vikundi mbalimbali na wananchi waliojitokeza kumpokea.
Rais huyo  ambaye anaitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza kufuatia  mwaliko kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete atapata mapokezi rasmi kesho katika viwanja vya Ikulu majira ya saa 3 asubuhi ambapo rais huyo akiwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete atapata fursa ya kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kupigiwa mizinga 21.
Akiwa nchini Tanzania Rais Joachim Gauck atakuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam na baadaye kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Vyama vya hiari, uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa Dar es salaam.
Pia Februari 4, 2015, Rais huyo ataelekea Zanzibar ambapo atakutana na kuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kabla ya kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania  Februari 6, 2015 rais huyo wa Shirikisho la Ujerumani atatembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti ,Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  na Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu jijini Arusha