Thursday, October 31, 2013

UWANJA WA TAIFA WAGEUKA WESTGATE MABOMU YARINDIMA BAADA YA KAGERA SUGAR KUCHOMOA BAO DAKIKA ZA MWISHO KWA MKWAJU WA PENARNATI DHIDI YA SIMBA


 Askari wa kutuliza ghasia, FFU, wakipiga mabomu ya machozi hewani kuwatawanya mashabiki wa Simba, waliokuwa wakifanya fujo kwa kung'oa viti na kurusha uwanjani baada ya timu ya Kagera Sugar, kusawazisha bao lao kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 90+, iliyotolewa na mwamuzi, Mohamed Theophile. Penati hiyo imepatikana baada ya beki wa Simba Joseph Owini, kumchezea vibaya Daud Jumanne, penati hiyo iliyopigwa na Salum Kanon, imezifanya timu hizo kutoka sare ya 1-1, wakati bao la SImba likifungwa na Amis Tambwe katika dakika ya 45.
 Askari wakimdhibiti mmoja wa mashabiki wa Simba.
****************************************
BAO la beki wa kulia wa Kagera Sugar, Salum Kanoni lilipoteza amani ndani ya Uwanja wa Taifa baada ya mashabiki wa Simba kuanza kung’oa viti hali iliyosababiosha Polisi walipue mabomu ya machozi kutuliza vurugu hizo.
Kagera ambao walikuwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Asimi Tambwe katika kipindi cha kwanza, walipata bao la kusaweazisha kupitia kwa Kanoni kwa njia ya panalti baada ya Joseph Owino kumwangusha Daudi Jumanne katika eneo la hatari.
Kwa sare hiyo hali ya Simba imeendelea kuwa tyete kwani bado wamebaki katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 21 nyuma ya Yanga yenye pointi 22 huku Azam na Mbeya City wakiwa juu kwa pointi 23 kila moja wakitofautiana mabao ya kufunga.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa katika dakika zote kwani timu hizo zilikuwa zikihitaji pointi tatu ili wajiweke sehemu nzuri kabla ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba itamalizia mzunguko wa kwanza kwa kucheza na Ashanti United mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jumamosi ya Novemba 2. 
 Kipa wa akiba wa Simba, Abel Dhaila, akimlalamikia mwamuzi wa akiba baada ya mwamuzi wa kati kutoa penati katika dakika za majeruhi.
  Kipa wa akiba wa Simba, Abel Dhaila, na Kocha Mkuu, Abdallah Kibaden, wakimlalamikia mwamuzi wa akiba baada ya mwamuzi wa kati kutoa penati katika dakika za majeruhi.
 Wachezaji wa akiba wa Simba wakisikitika baada ya kuamuliwa kupigwa penati hiyo.
 Askari wakiendelea kumdhibiti shabiki aliyekamatwa baada ya mashabiki hao kuvunja viti na kuanza kuruka uwanjani.
Askari wakiendelea kudhibiti vurugu..
 Sehemu ya viti vilivyoharibiwa..

Wednesday, October 30, 2013

MUNGU BARIKI BABU SEYA,RUFAA YAO YAANZA KUSIKILIZWA.


 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza 'Papii Kocha' wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, kabla ya kuanza kusikilizwa kwa rufaa ya kesi yao kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo. Nguza na Papii walihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na ulawiti. 
 Baadi ya watu waliohudhuria kusikiliza rufaa hiyo leo katika mahakama ya Rufaa.
 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii.
 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza wakiteta jambo na wakili wao, Mabere Marando.
 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza 'Papii' wakiwa na nyuso za furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kusikiliza maombi yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyoitoa mwaka 2010.

Tuesday, October 29, 2013

MH RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AENDA LONDON -UINGEREZA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Swissport katika uwanja wa ndege wa kimataifa ya Julius Nyerere wakati akielekea kwenye ndege jioni ya jana, Jumatatu, Oktoba 28, 2013, kwenda London, Uingereza, kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambako atahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali Uwazi (Open Government) uliotishwa na Serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe na Meneja wa Shirika la ndege la Emirates uwanjani hapo Bw. Aboubakar Jumaa. PICHA NA IKULU

Sunday, October 27, 2013

MKUU WA MKOA WA DODOMA DR REHEMA NCHIMBI ASISITIZA MAADILI MEMA KWA WANAFUNZI MASHULENI.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi ametoa wito kwa shule zinazomilikiwa na taasisi za dini kuhakikisha zinaziba mianya yote ya mafundisho yasiyofaa kwa wanafunzi yanayoletelezwa na mabadiliko ya utandawazi ili ziweze kuzalisha wanafunzi wenye ubora kielimu na kimaadili.

Dr. Nchimbi alibainisha kuwa hivi sasa kumekuwa na mianya mingi inayowezesha mafundisho mbalimbali yanayopatikana kpitia maendeleo ya utandawazi ambayo baadhi yamekuwa na viashiria vinavyochangia kuharibika kwa tabia, maadili na mfumo mzima wa wanafunzi kujifunza na kuwaasa wanafunzi kuwa makini sana na masuala ya utandawazi katika safari zao za masomo kwani wasipotumia utandawazi ipasavyo itachangia kuharibikiwa katika masomo yao.

Dr. Nchimbi aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya tisa ya sekondari ya wasichana ya huruma inayomilikiwa na shirika la watawa wakatoliki la misericodia iliyopo jimbo katoliki mjini Dodoma ambapo mahafali hayo yalikwenda sambamba na jubilei ya miaka 50 tangu watawa hao wa misericodia kuanza kutoa huduma za elimu hapa nchini.

Dr. Nchimbi aliongeza kuwa katika ulimwengu wa sasa wa utandawazi na maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano kumekuwa na maumizi mabaya ya teknolojia hizo yanayofanywa na wanafunzi matokeo yake tunazalisha wataalamu na viongozi wasiokuwa na maadili  na pia amezitaka shule ningine hapa nchini kujipanga nazo kupambana na tatizo hili.

Mkuu huyo wa mkoa pia alishukuru mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za dini katika kuhudumia jamii akiainisha upande wa kutoa huduma za elimu kwa jamiinna kusema kuwa serikali inatambua na kuthamini sana mchango huo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi hizo za kidini ili kwa pamoja waendelee kuhudumia jamii na kusaidia kuleta maendeleo hapa nchini.

Kwa upande wake askofu mn'gatuka wa jimbo katoliki Dodoma Mwashamu Martias Isuja akitoa historia alisema kuwa miaka ya hapo awali mfumo wa elimu hapa nchini ulikuwa finyu hasa kwa upande wa wasichana kwenda shule ndipo kanisa kupitia mashirika yake mbalimbali yakaanza kuwekeza kwenye elimu. Aliielezea shule hiyo ya Huruma kama miongoni mwa shule za kwanza hapa nchini ambazo zilianza kwa kutoa huduma za stadi/maarifa ya nyumbani na kuendelea kupiga hatua mpaka leo hii.

Kwa upande wao wahitimu wa kidato cha nne wakiwakilishwa na mwanafunzi Ritah George aliyesoma taarifa ya wanafunzi wanaotarajiwa kuhitimisha masomo yao ya kidato cha nne mwaka huu wameomba uongozi wa shule kushughulikia changamoto za maktaba yenye nafasi za kutosha, vifaa vya kujifunzia kama kompyuta,viwanja vya michezo na walimu wa michezo.




Sehemu ya wanafunzi 46 wanaotarajia kuhitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Huruma iliyoko mjini Dodoma wakisikiliza salamu za mkuu wa Mkoa wa Dodoma (hayupo pichani) wakai wa mahafali ya 9 ya kidato cha nne shuleni hapo yaliyoenda sambamba na jubilei ya miaka 50 tangu watawa wa misericordia kuanza kutoa huduma za elimu hapa nchini, mahafali hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki.

BABA MZAZI WA MSANII WEMA SEPETU MZEE ISAACK SEPETU AFARIKI DUNIA.


Habari zilizotufikia hivi punde mtandao huu , zinasema kuwa, Baba Mzazi wa msanii wa Filam nchini na Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu, Balozi Issac Abraham  Sepetu, amefariki Dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya TMJ Mikocheni jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa.

Aidha imeelezwa kuwa, Balozi Sepetu alikuwa amelazwa katika hospital ya TMJ akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi uliokuwa ukimsumbua.

Hadi umauti unamkuta,Balozi Isaac Sepetu alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar.

Mtandao huu unaungana na waombolezaji wote wa Msiba huu na Mwenyezi Mungu, Aiweke Roho ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu, Mahala Pema Peponi .

-Amen.

Saturday, October 26, 2013

MKE WA MWANAJESHI WA JWTZ AOMBA MSAADA ILI KULEA WATOTO WAKE MAPACHA WA 3.


Na John Banda, Dodoma
MWANAMKE wa mwanajeshi aomba msaada kwa wasamalia wema ili aweze kuwahudumia watoto wake kwa chakula mavazi na elimu kutokana na ugumu wa maisha kiasi cha kushindwa kupata hata lishe ya kuwapa mapacha watatu aliojifungua kinyume na matarajio yake.
Mwanamke huyo Rehema Khamis [30] mkazi wa mkalama kata ya makulu manispaa ya Dodoma aliomba msaada huo baada ya kuona toka ajifungue watoto hao watatu imefika wakati ameshindwa kuwapatia hata uji wenye lishe huku mshahara wa Mumewe ukiishia kwenye madeni.
Rehema alisema  alijifungua watoto hao wa kiume wawili na wa kike mmoja Hassan, Husen na Hasanati katika hospitali ya Rufaa ya Dodoma na sasa wanakaribia kuwa na umri wa mwaka mmoja aliowachisha kunyonya wakiwa na miezi 7 kutokana na kukosekana maziwa.
Alisema hakutarajia kupata watoto watatukwa mpigo kutokana na tayali alishakuwa na wengine wawili hivyo alijua akipata mmoja angepumzika kuzaa ili ajipe nafasi ya kuwalea, hivyo kutokana na watoto hao kuhitaji chakula, mavazi na hata elimu kwa hao wakubwa imekuwa ni sababu ya kuhitaji msaada.
‘’Watu wa kada mbalimbali wamekuwa wakifika kuwaona watoto hawa lakini ni kama uwanja wa \maonyesho na kutaka kuniona mama yao wakishatuona wanaondoka lakini si kwa kuleta msaada wowote hivyo naomba wenye uwezo na moyo wanisaidie ili niweze kuwapa malezi bora’’,alisema Rehema.
Nae Baba wa watoto hao Abubakari Ally Hamad Mwanajeshi wa ajira mpya katika jeshi la wananchi wa Tanzania [JWTZ] kikosi cha 673 Msalato Dodoma alisema mahitaji yamekuwa hayatoshelezi kutokana na mshara anaopata kuishia kwenye madeni ambayo amekuwa akikopa kwa wanajeshi wenzake.
Alisema pesa hata madeni hayo ambayo amekuwa akikopa hayatoshelezi mahitaji ya watoto hao ambao hata hivyo hahitaji kuongeza wengine, hata hivyo aliwataka watu mbalimbali zikiwemo taasisi za kiserikali kumsaidia kutokana na watakavyojaliwa na mwenyezi mungu ili aweze kuwa tunza watoto wake.
Kwa upande wake Ofisa mtendaji wa kijiji cha makulu Namsfu Mihungo alisema wao kama serekali wanajitahidi kufikisha ujumbe kwa watu kuhusu familia hiyo kuhitaji msaada na kufika kuwaona lakini hawakujua kama hakuna msaada unaotolewa, hivyo watajipanga kuona nini watafanya ili kuisadia familia hiyo kwa kadili watakavyoweza.




Rehema Khamis akiwa na watoto wake mapacha watatu na dada yao ambapo hata hivyo kaka yao hakuwe mwenye umri wa miaka 13, mama huyo anahitaji msaada ili aweze kuwatunza kuwalea




Rehema Khamis [30] akimlisha uji mtoto mmoja kati ya mapacha watatu huku wengine wakisubilishwa mpaka wakwanza amalize  kutokana na mama huyo kukosa mtu wa kumsaidi kuwalea watoto hao.