Saturday, October 12, 2013

PICHA LIVE KUTOKA KAITABA YANGA IKIWAUA KAGERA SUGAR 2-1


 Beki wa Yanga, Kelvin Yondan, akichuana na mshambuliaji wa Kagera Sugar, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. 

Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-1, huku bao la kwanza likifungwa na Mrisho Ngasa katika dakika ya 1 na bao la pili likigungwa na Hamis Kiiza katika dakika ya 57, na bao la Kagar Sugar lilifungwa na Godfrey Wambura katika dakika la 47.

Mchezo huo kati ya Kagera Sugar na Yanga, umeziweka timu hizo katika mbio za presha kuelekea mchezo wao wa Oktoba 20, kwa utofauti wa pointi 1. 
 Wachezaji wa Yanga, Mbuyu Twite (kushoto) Hamis Kiiza (katikati) na Mrisho Ngasa, wakishangili bao la kwanza lililofungwa na Ngasa katika dakika ya 1.
 Kikosi cha Kagera Sugar.
 Kikosi cha Yanga, kilichoanza kuwakabili Wana Nkurukumbi.
 
 Wachezaji wa Yanga, wakishangilia bao la pili.
 
Benchi la Yanga.

No comments:

Post a Comment