Monday, October 21, 2013

MADEREVA WAPIGA VIROBA WAKIWA SAFARINI KUFUTIWA LESENI:DR REHEMA NCHIMBI MKUU WA MKOA WA DODOMA



Na John Banda, Dodoma

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi amewataka madereva wa magari ya Abiria na mizigo  wanaopitia mkoa huo kuacha kutumia kilevi chochote ikiwemo viroba wanapokuwa Barabarani la sivyo kufutiwa Leseni zao.
Mkuu huyo wa mkoa alitoa kauri hiyo siku ya usalama Barabarani iliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma juzi.
Nchimbi alisema ulevi kwa madereva hao umekuwa ukiwasababishia kuwa wazembe barabarani pindi wanapokuwa wakiendesha magali ya abiria kwa maana ya mabasi na maroli ya mizigo na huwa ni chanzo cha ajali za mara kwa mara.
Dr huyo wa Farsafa alisema ana taarifa za kutosha za ulevi kwa baadhi ya madereva hao na hivyo atatumia jeshi la polisi kuwanasa na kuwafutia leseni zao.
Aliongeza kuwa mbinu watakayotumia jeshi la polisi ni kuwapima madereva wote wanaoingia na kutoka ndani ya mkoa wa Dodoma  kwa kipimo maalumu cha kung’amua ulevi na atakaegundulika kuendesha akiwa amekunywa pombe au aina yoyote ya kilevi ikiwemo viroba atafutiwa leseni.
‘’Hivi sasa mkoa wetu unapoelekea kuwa jiji tunatakiwa pia kuwa mfano wa kuigwa na mikoa mingine kuhusu udhibiti wa madereva walevi, hivyo Dereva yoyote ili awe salama ahakikishe hajihusishi na ulevi ili aweze kupita mkoa huu akiwa salama la sivyo apitie juu ama kama kuna njia ya kuzunguka apite huko’’, alisema Dr. Chimbi
Aidha alisema zoezi hilo la kupima madereva walevi litaanzia kwa wale wa Daladala na Bodaboda ambao wamekuwa wakinyonya viroba hata wanapokuwa wanaendesha abiria wao bila kujali, aliwaagiza polisi kufavamia maeneo yote wanakopakilia na kuhakikisha wanawapima hapo hapo na atakaebainika uzi ni uleule wa kufutiwa leseni.
Awali akikielezea kipimia ulevi hicho kinachotumiwa na polisi wa usalama barabarani Pc Jerome Mbano alisema kipimo hicho kina uwezo wa kubaini kiwango cha pombe alichokunywa mtu hata kama alikunywa masaa 24 yaliyopita [jana yake]

No comments:

Post a Comment