Sunday, August 31, 2014

TAZAMA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI ZA UZINDUZI WA VICOBA MKOANI DODOMA.

Mlezi wa Vicoba mkoani Dodoma Anthon Mavunde akipeana mikono na
Naibu waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Godfrey Zambi wakati wa
uzinduzi wa Vicoba uliofanyika jana
Wanachama wa kikundi cha vicoba cha kilimani a' wakishangilia
mara baada ya kutangazwa kushika nafasi ya pili baada ya kujiwekea
hisa za shilingi 23 mili na kupata zawadi ya laki tano toka makao
makuu ya vicoba nchini.

Mmoja wa wanavicoba akikabidhiwa friji ya kampuni ya cocacola
baada ya kufuzu vigezo vya biashara ya vinywaji na Naibu waziri huyo.

Rais wa Vicoba Nchini Devota Likokola akiiwa na baadhi ya viongozi
waliokuwa meza kuu wakati wa uzinduzi huo

 PICHA NA JOHN BANDA

Saturday, August 30, 2014

DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA SARATANI YA MATITI KUTOKA INDIA ALIVYOTOA SEMINA YA UGONJWA HUO KWA MADAKTARI WA TANZANIA NA WADAU WA SEKTA YA AFYA KWA UDHAMINI WA KAMPUNI YA MABIBO BEER WINES AND SPIRITS LTD

Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akifuatilia matukio mbalimbali kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira, akiwa kwenye semina hiyo.
Daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka nchini India, Profesa Anthony Pais, akitoa mafunzo kuhusu ugonjwa huo kwa madaktari wa kitanzania na wadau mbaliombakli wa sekta ya afya. Semina hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana, Hoteli ya Protea Courtyard Seaview.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira, akizungumza katika semina hiyo. Kampuni hiyo ilidhamini semina hiyo.
Profesa Anthony Pais, akiwa na madaktari wa kitanzania. Kutoka kushoto ni Executive Chairman Tanzania Creative Industries Network (TACIN), Anic Kashasha na Dk.Paul Mareale.
Profesa Anthony Pais (kushoto), akielezea jambo kuhusu ugonjwa huo.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira.

Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) , Dk.Malina  Njelekela(kulia), akizungumza na wadau mbalimbali katika semina hiyo.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni mke wake ambaye ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Benedicta Rugemalira na Profesa Anthony Pais.
Profesa Pais (katikati), akiwa na wenyeji wake. Kutoka kulia ni Dk.Paul Mareale, James Rugemalira, Dk.Malina Njelekela na Benedicta Rugemalira.
Profesa Pais akizungumza na waandishi wa habari.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kushoto), akipeana mkono na daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka India, Profesa Anthony Pais (kulia), baada ya kutoa mafunzo kwa madaktari wa Tanzania na wadau wa sekta ya afya kuhusu ugonjwa huo, Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira, waliodhamini mafunzo hayo ya siku moja.
Profesa Pais (mwenye suti katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake.
Profesa Pais (mwenye suti katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake.
Wadau mbalimbali na maofisa wa Kampuni ya Mabibo wakiwa kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) , Dk.Malina  Njelekela(kulia), akiteta jambo na viongozi wengine kwenye semina hiyo

MCHEPUKO NOMA:BINTI AFARIKI KWA AJALI MUME WAKE AKIWA KWENYE MIPANGO YA HARUSI YEYE AKIWA KWENYE MCHEPUKO.

 Binti ambaye hakuweza kufahamika jina lake kwa haraka (pichani chini), ambaye alikuwa afunge ndoa na mchumba wake hivi karibuni,  amepata ajali na kufariki dunia akiwa na 'mchepuko'.
Aidha imeelezwa kuwa wakati mchumba wake akiwa katika harakati za kukamilisha mipango ya ndoa akapata taarifa kuwa mchumba wake huyo amefariki kwa ajali ambapo hakuweza kuamini hadi alipoonyeshwa picha za ajali hiyo.
Imeelezwa kuwa marehemu alimuaga mchumba wake huyo kuwa anakwenda kulala kwa dada yake na kwenda kinyume na alivyoaga na kukutwa na ajali hiyo iliyompelekea umauti. Katika ajali ya gari hilo lililokuwa na wapenzi wawili wote wamepoteza maisha papo hapo huko mkoani Geita.
marehemu enzi za uhai wake (pichani chini na juu)

Tuesday, August 19, 2014

KAMATI KUU YA CCM YAANZA VIKAO VYAKE MJINI DODOMA CHINI YA MWENYEKITI WAKE RAIS JAKAYA KIKWETE.



 Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia kwenye ukumbi wa NEC Dodoma ,akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana tayari kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC ,Makao Makuu ya CCM Dodoma.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk.Maua Abeid Daftari akijadiliana jambo na mjumbe mwenzake Samia Suluhu Hassan muda mfupi kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa hakijaanza kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
 Katibu wa NEC Oganizesheni Dk.Mohamed Seif Khatibu akizungumza na Mjumbe wa Kati Kuu ya CCM DK. Salim Ahmed Salim ndani ya ukumbi wa mkutano wa White House kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakijadiliana kabla ya kuanza kwa kikao kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma, kutoka kushoto ni Profesa Anna Tibaijuka, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Dodoma

Monday, August 18, 2014

MKUU WA MKOA DODOMA DR REHEMA NCHIMBI AMEFUNGUA JENGO LA HUDUMA KWA WAGONJWA WA NJE (O.P.D) KWENYE KITUO CHA AFYA LUMUMA MPWAPWA LENYE THAMANI YA MIL.350

Hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la huduma kwa wagonjwa wa nje OPD kwenye kituo cha afya cha lumuma Mpwapwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki ilitanguliwa na ibada takatifu iliyoongozwa na makamu wa askofu kanisa katoliki dodoma padiri Chesco Msaga (wa pili kulia) kituo hiko cha afya kinamilikiwa na kanisa hilo kupitia shirika lake la watawa la Mt. Gema
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akiwa amembeba mtoto aliyepewa jina la Rehema na mama yake kama ishara ya kumuenzi mkuu huyo wa Mkoa kwa kuwa mtoto huyo alizaliwa kwenye kituo cha afya lumuma mpwapwa majira ambayo mkuu huyo wa Mkoa alikuwa ndio anawasili kituoni hapo kufungua jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje OPD lililogharimu kiasi cha Milioni 350 mwishoni mwa wiki.
Umati wa wananchi wa kata ya lumuma mpwapwa na maeneo ya jirani ya wilaya ya kilosa morogoro waliojitokeza kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje OPD kwenye kituo cha afya cha kata ya lumuma mpwapwa mwishoni mwa wiki
picha na JOHN BANDA