Monday, December 30, 2013

ERNEST MANGU I.G.P MPYA AKICHUKUA NAFASI YA SAID MWEMA ALIYESTAAFU.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.

Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi hilo la Polisi.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations). Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
30 Desemba, 2013

SIDO MKOANI DODOMA YATOA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA BIDHAA ZA NGOZI KWA VIJANA WAJASIRIAMALI 27 WA MANISPAA DODOMA


Mkufunzi wa mafunzo ya kutengeneza bidhaa za ngozi Ndg.  Shaban  Lukandamila akimuonesha mkuu wa mkoa dodoma Dr Rehema Nchimbi bidhaa za ngozi zilizotengenezwa na vijana wajasiriamali wa manispaa ya Dodoma waliopatiwa mafunzo ya SIDO Dodoma ya utengenezaji bidhaa za ngozi. Mafunzo hayo yalifungwa jana na mkuu huyo wa mkoa.

Mkuu wa mkoa dodoma  Dr. Rehema Nchimbi akimkabidhi cheti kijana mjasiriamali SEIF DAUD aliyehitimu mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi kwenye kituo cha SIDO Dodoma kinachofundisha mafunzo hayo.
Picha ya pamoja kati ya mkuu wa mkoa wa dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa tatu kulia waliokaa) na vijana wajasiriamali 27 kutoka manispaa ya Dodoma waliopata mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi mara baada ya mkuu wa mkoa kufunga rasmi mafunzo hayo mapema jana  kwenye kituo cha SIDO  Dodoma kinachofundisha utengenezaji wa bidhaa za ngozi. Wengine waliokaa ni viongozi wa SIDO Dodoma na viongozi wa asasi ya marafiki wa elimu Dodoma waliofadhili  mafunzo hayo.

Sunday, December 29, 2013

WATUMIAJI WA NYAMA YA KITI MOTO WAKO KWENYE HATARI YA KUKUMBWA NA UGONJWA WA KIFAFA.


UTAFITI WA KISAYANSI uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo [SUA] umebaini walaji wa nyama ya nguruwe ‘kitimoto’ wapo katika hatari ya kupata ugongwa wa kifafa kutokana na baadhi ya ngururuwe kuwa na minyoo inayopelekea ugonjwa huo. Hayo yalibainishwa na Mhadhiri n a Mtafiti wa Idara ya Sanyansi ya Wanyama na Uzalishaji SUA, Profesa Faustine Lekule alipokuwa akizungumza na mwandishi kutoka chombo cha serikali.

Profesa Lekule alisema, utafiti uliofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark [DANIDA] ulibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.

Uchunguzi huo ulibaini kuwa, nyama hiyo kuwa na minyoo hatari iitwayo TEGU kuwa katika nyama hiyo, hivyo endapo kama nyama hiyo ikiliwa pasipo kuiva vizuri minyooo hiyo kawaida kukimbilia kichwani na hatima yake mlaji kukumbwa na tatizo la kifafa.

Alisema utafiti ulibaini baadhi ya wafugaji hawazingatiii kanuni za ufugaji na kuwaacha wanyama hao kujitafutia chakula wenyewe na wanyama hao kupelekea kula hata kinyesi cha binadamu, kutokana na wafugaji kujisaidia hovyo vichakani na ni moja ya sababu ya wanyama hao kupelekea kupata minyoo hiyo.

Hivyo binadamu nae anapokula nyama hiyo pasipo kuzingatia kanuni na kuila ikiwa haijaiva vizuri hadi minyoo hiyo kuisha ndani ya nyama hiyo hupelekea kupata madhara hayo kwa kuwa kuwa minyooo hiyo hukimbilia kichwani.

Alisema ugonjwa huo hautaweza kukwepeleka kwa walaji wa nyama hiyo kwa kuwa nyama nyingi husafirishwa na kusambazwa maeneo mengi na wanyama hao wengi hutokea maeneo ya mikoani mikoa mikubwa yenye mapori.

Profesa Lekule ameitaka serikali kwa ushirikiano wa wafugaji na wataalamu wa afya kushirikiana kwa hali na mali kudhibiti ugon jwa na kukabiliana na changamoto zilizopo kwakuwa,huo ambao ni hatari

MAANDALIZI YA KUUPOKEA MWAKA MPYA 2014 KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO DODOMA LIVE KATIKA SEMINA YA KUHAKIKISHA 2014 UNATEMBEA KATIKA UTUKUFU WA MUNGU

                                     KWAYA IKIIMBA KATIKA SEMINA HIYO
 MSANII WA NYIMBO ZA INJILI TUMSIFU RUFUTU (mwambie farao)AKIIMBA KATIKA SEMINA YA NENO LA MUNGU KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO DODOMA
                                     BAADHI YA WASHIRIKI WA SEMINA HIYO
 PST KOMBA WA KANISA LA MLIMA WA MOTO AKIHUBIRI KATIKA SEMINA HIYO
            PUNDA WA YESU PST KOMBA AKISISITIZA JAMBO KATIKA SEMINA HIYO
PICHA NA JOHN BANDA

MWENDELEZO WA SEMINA YA NENO LA MUNGU KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO DODOMA.

 BAADHI YA WAUMINI WALIOSHIRIKI SEMINA YA NENO LA MUMGU KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO DODOMA
MCHUNGAJI WA KANILA LA MLIMA WA MOTO DODOMA PST KOMBA(punda wa yesu)AKIFANYA MAOMBEZI KATIKA SEMINA YA NENO LA MUNGU KATIKA MLIMA WA MOTO DODOMA.

Saturday, December 28, 2013

MATUKIO MBALIMBALI YA SEMINA YA NENO LA MUNGU KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO DODOMA.

 MCHUNGAJI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO PST KOMBA AKIHUBIRI KATIKA SEMINA HIYO
 PST KOMBA(PUNDA WA YESU)AKISISITIZA JAMBO NAMNA YA KUMTUMAINI MUNGU KATIKA MAISHA YA BINADAMU
                                                            MAOMBEZI
                                         PST KOMBA AKIFUNDISHA KATIKA SEMINA HIYO
                                                                MAOMBEZI
WATU WENYE MAHITAJI MBALIMBALI WALIOFIKA KATIKA SEMINA WAKIPATIWA MAOMBI NA PST KOMBA WA MLIMA WA MOTO DODOMA

PICHA NA JOHN BANDA

PICHA ZA UFUNGUZI WA SEMINA YA NENO LA MUNGU KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO DODOMA.

 MCHUNGAJI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO PST KOMBA AKIHUBIRI KATIKA SEMINA HIYO
 PST KOMBA (PUNDA WA YESU)AKISISITIZA JAMBO KATIKA MAHUBIRI YAKE KATIKA SEMINA YA KANISA LA MLIMA WA MOTO DODOMA
 ANTONY MAVUNDE M-NEC NI MIONGONI MWA WAGENI WA HESHIMA KATIKA UFUNGUZI WA SEMINA HIYO.
WASHIRIKA WA SEMINA YA NENO LA MUNGU KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO WAKIMSIKILIZA MNENAJI WA SEMINA HIYO PST KOMBA KWA MAKINI SANA