Wednesday, December 18, 2013

ABAKWA VIBAYA NA KUTELEKEZWA MAKABURINI,HUKU MKE WA MBUNGE WA JIMBO LA MTERA AKIHUSISHWA NA TUKIO HILO.

mwanamke chipegwa chamlomo 25 amefanyiwa kitendo cha kinyama baada ya kubakwa na vijana zaidi ya watano katika makaburi ya mvumi mkoani Dodoma
Akisimulia mkasa huo uliompata mbele ya waandishi wa habari chipenga amesema kuwa tukio hilo lilimkumba tarehe 16desember2013 majiraya saa 1:30 jioni wakati akitoka kwenye sherehe aliyokuwa amealikwa na mke wa mbunge wa jimbo la mtera mh livingstone lusinde.BI EDINA LUSINDE
Chipegwa amesema kuwa wakati yuko njiani kurudi nyumbani ghafla aliona  vijana wawili wakimfuata na mmoja wao kumkaba shingoni kwa kutumia waya ,wakati akitafuta namna ya kujiokoa kutoka mikononi mwa vijana hao walitokea wanaume wengine watatu waliokuwa wamefunika nyuso zao,baada ya kutokea vijana hao alipoteza fahamu mpaka alivyozinduka  na kujikuta yuko makaburi huku akiwa amebakwa vibaya na vijana hao pamojana kufanyiwa vitendo hivyo vya kinyama kinyume na maumbile.

Hata hivyo chipegwa amesema kuwa anahisi mke wa mbunge lusinde BI EDINA LUSINDE ndiye aliyefanya tukio hilo kwa kukodisha vijana hao kwani kabla ya hapo walikuwa naugomvi mkubwa naye kwa kumshutumu bintihuyo kutembea na mumewe ambaye ni mh lusinde,akielezea kwa masikitiko makubwa chipegwa amedai kuwa mara kadhaa mama huyo amekuwa akimtishia kumfanyia kitu mbaya kama hatoacha kutembea na mumewe,ameongeza kuwa hata kabla ya kufanyiwa kitendo hicho cha aibu siku chache kadhaa zilizopita alipokea ujumbe kutoka kwa mmoja wa marafiki wa mama huyo mke wa mmbunge akimtahadhalisha binti huyo kuwa sasa amejipanga kumfanyia kitu kibaya ambacho hatokuja kusahau maishani mwake,hivyo kwa haya matukio hisia zake zinampelekea kuamini  kuwa mke wa mbunge lusinde ndiye mhusika mkuu wa kubakwa kwake.

Hata hivyo tulipojaribu kumuhoji mama mzazi wa bint huyo alikiri kusikia tuhuma hizo za mama wa mbunge huyo kuhusika na tukio la kubakwa kwa mtoto wake  huku akilaumu jeshi la polisi kushindwa kumchukulia hatua zozote za kisheria hata kwa upelelezi licha ya kutajwa na binti yake kuwa ni mhusika namba moja.mama huyo hata hivyo aliendelea kutoa masikitiko yake na kudai kuwa yeye anamuachia mungu.
Alivyotafutwa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa dodoma suzan kaganda alikiri kupokea taarifa hiyo na kueleze kuwa mpaka sasa hakuna mtu yoyote anayeshikiliwa na jeshi la polisi kuhusika na tukio hili na uchunguzi unaendelea pindi watakapowatia mbaroni watuhumiwa watapelekwa mahakamani bila kujali umaarufu ,cheo wala uwezo wa mtu.
Dada wa mtoto huyo wa mchungaji rehema chamlomo akifafanua jambo kuhusukitendo chaubakaji alichofanyiwa mdogo wake na kutelekezwa makaburini akiwahajitambui.
Mama wa Chipegwa jane chamlomo akiwa na dada wa chipegwa katika hali ya masikitiko walipofika kumuona baada ya kupata taarifa ya tukio hilo.

No comments:

Post a Comment