Friday, May 31, 2013

CHADEMA NA CUF WAOMBA RADHI KWA VURUGU BUNGENI

145
Dodoma, Tanzania.Chama cha CUF na Chadema hivi punde Bungeni , vimekubali kuomba radhi kutokana na vurugu zilizosababishwa na CUF  yenye mrengo wa Kiliberali  na Chadema imemafanya hivyo kutokana na kuihusisha CUF na masuala ya ushoga na usagaji.
Vyama hivyo vimeomba radhi baada ya Kamati ya Maadili ya Bunge kufanya kikao  kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 2:30 usiku na kukubaliana kila chama kumuomba spika radhi na pia kuliomba Bunge radhi kutokana na vurugu za jana.
CUF wamelazimika kumuomba spika radhi; kuomba radhi Bunge na kuwaomba radhi Chadema kwa kumtukana Waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekeil Wenje wakati akisoma hutuba yake ambayo ndani yake ilieleza sera za mrengo wa Kiliberali ambazo  pamoja na mambo mengine ni ushoga na usagaji.
Awali Mnadhimu wa Chama cha CUF, Rashidi wakati akiomba radhi aliipongeza Kamati ya Maadili na Chadema kwa kufikia muafaka kwa maslahi ya Taifa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“ Napenda kuomba radhi kwa watu wote walioumizwa na vurugu za jana,” amesema hivi punde Rashidi.
Naye Kiongozi wa Kambi rasni ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesimama Bungeni hivi pinde na kuwaomba radhi CUF, Bunge na Spika kutokana na hotuba ya jana iliyosomwa bungeni jana na Wenje.
Awali kabla ya kuomba radhi leo, Freeman Mbowe jana kwenye kikao cha Kamati ya Maadili ya Bunge, alisema kwamba CUF wanafuata mrengo wa Kiliberali ambao msingi wa sera zao ni shoga na usagaji na kwamba hawakufanya kosa, pia alisema CUF alimdhalilisha Wenje (Chadema), CUF walichana hotuba yao na kuwaudhi na kuwakera Chadema.
Kutokana na hali hiyo CUF walishauriwa kuomba radhi jambo ambali wamelifanya leo asubuhi.
Wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo  John Chiligati ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki amesema jana CUF walikiri kwenye kamati hiyo kwamba wao ni wanachama wa mrengo wa Kiliberali, lakini chama chao hakikubaliani na sera zote kama za ushoga na usagaji kwa kuwa serikali imeshatoa msimamo kwamba haiungi mkono masuala hayo

WAUMINI WAUKIMBIA MSIKITI KISA KAULI YA BEATRICE SHELUKINDO BUNGENI.

Na John Banda, Dodoma.

KUFUATIA kauli iliyotolewa na mbunge wa kilindi Beatrice Shelekindo ya kuwa msikiti wa barabara ya saba uliopo katika manispaa ya Dodoma unafundisha mafunzo ya ugaidi na kareti kwa waumini wake imeuathiri msikiti huo.

Akizungumza na dodomafamily Shekhe Mohamed Awadhi wa msikiti huo alisema kauli yake hiyo Imeuhathiri waumini wake kutokana kuukimbia na baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakisoma masomo kuhamishwa na wazazi wao.

Awadhi alisema hivi sasa wapo katika wakati mgumu kutokana na waumini waliokuwa wakiswali ndani ya msikiti huo kuamua kuhama baada ya kutolewa kauli ambayo wanaamini ni ya uzushi na uchochezi kwa ajili ya kupotosha jamii na serikali.
Shekhe huyo alisema kuwa msikiti huo umejengwa kwa miaka mingi na karibu baadhi ya wanaoswali ni pamoja na viongozi wa kiserikali wakiwemo askari toka taasisi mbalimbali kama vile polisi,wanajeshi,usalama na takukuru.
“Sasa kama kweli sisi tungekuwa tunafundisha hayo mafunzo ya ugaidi na kareti,serikali pamoja na waumini kutoka vyombo vya dola kweli msikiti huo ungeachwa bila kuchukuliwa hatua zozote”aliuliza Shekhe Awadhi.

Naye mlezi wa wanafunzi wa msikiti huo wa barabara ya saba Husseni Hamedi Fundi,alikiri baadhi ya wazazi na walezi kuwahamisha watoto wao kutokana na kauli iliyotolewa na mbunge huyo wa jimbo la Kilindi.

Fundi alisema kuwa msikiti unapokea wanafunzi kutoka nje ya Mkoa wa Dodoma kama vile Kigoma,Singida,Mwanza,Pemba,Zanzibar,Tanga na Bukoba kwa ajili ya kujifunza  lugha ya kiarabu na elimu ya Quran.
“Lakini hivi sasa baadhi yao wamehamishwa na wazazi, walezi hii yote ni kutokana na uzushi uliotolewa na Mbunge huyo wa Kilindi ambaye sisi kama waumini wa msikiti huo tunaona amepotosha jamii na serikali yetu,
''Kutokana na kauli yake hiyo imetudhalilisha sana hivyo tunaamini Mwanamama huyo anatakiwa kusema ukweli ukizingatia kuwa sehemu anayoielezea ni Bunge ambalo linalotengemewa na Watanzania wote'', Alisema Fundi
Kauli hiyo iliyoleta utata ilitolewa na Mbunge wa  jimbo la Kilindi Beatrice Shelukindo mei 4, mwaka huu wakati akichangia bajeti ya Wizara ya mambo ya ndani alisema msikiti huo wa barabara ya saba unatoa mafunzo ya ugaidi na kareti.

Mwisho

WENJE ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI AWAVURUGA CUFNA HOTUBA YAKE.

 Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, leo amechafua hali ya hewa bungeni baada ya kusoma hotuba yaake iliyowakasirisha wapinzani wenzao wa Chama cha CUF, jambo lililomfanya Naibu Spika Job Ndugai, kuahirisha Kikao cha Bunge mapema asubuhi.

Wabunge wa Chama cha CUF wamezua tafrani hiyo Bungeni mjini Dodoma leo wakati Mbunge huyo wa Nyamagana, akisoma hotuba ya Kambi ya Upinzani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Wenje akiendelea kusoma hotuba hiyo  ndipo Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud Abdalla Salim, aliomba muongozao kwa Naibu Spika, Job Ndugai,  akipinga maneno yaliyokuwa yameandikwa katika ukurasa wa nane wa hotuba hiyo yaliyosomeka Hivi:- 

Mheshimiwa Spika wa Upande wa CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na kupigania haki za ndoa ya Jinsia moja, usagaji na ushoga hii ni kwa mujibu wa tangazo lao la kwenye mtandao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, ikiungwa mkono na Waziri wa Haki na usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka Chama cha Libera Democratis.

Baada ya hapo wabunge wa Cuf walisimama na kusema wakitaka maneno hayo yafutwe ingawa msomaji wa hotuba hiyo alikuwa hajafika katika ukurasa huo wa hotuba wakati huo msomaji alikuwa amefika kwenye ukurasa wa nne.

Baada ya kuona mabishano na kutoelewana ukumbini humo, Naibu Spika , Job Ndugai, alitumia busara zake na kutangaza kusitisha shughuli za Bunge  kabla mambo hayajawa mabaya maana kulikuwa na kila dalili za kuanza kushikana mashati baada ya baadhi ya wabunge wa Chama hicho kuanza kufoka kwa sauti kubwa ndani ya Bunge, bila kufuata utaratibu

WAZIRI MKUU AFUNGA SEMINA YA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KUHUSU UTARATIBU WA KUPATA MBOLEA YA RUZUKU KWA WAKULIMA.



Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimfafanulia jambo  Mkuu wa Wilaya ya Bunda Angelina Mabula nje ya ukumbi wa Royal Village Dodoma walipoku wakitoka Kwenye Semina ya wakuu wa mikoa, Wilaya na Wabunge kuhusu Mfumo mpya wa utoaji wa Ruzuku ya Mbolea ya mazao kwa wakulima, iliyoandaliwa na Wizara ya kilimo na Chakula.




Waziri mkuu Mizengo Pinda akitoka kufunga Semina ya siku Mbili iliyofanyika Dodoma jana iliyowahusisha Wabunge, Wakuu wa Mkoa na Wilaya wa Nchi Nzima Kuhusu Utaratibu mpya wa Utoaji wa Ruzuku ya mbolea ya mazao kwa Wakulima katikati ni Waziri wa Kilimo na Chakula Christopher Chiza Naibu Waziri wa wizara hiyo Adamu Malima na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Angelina Mabula




Washiriki wa Semina ya Utaratibu Mpya wa utoaji wa Ruzuku ya Mbolea Kwa wakulima iliyofanyika mjini Dodoma kwa siku mbili

                                         PICHA NA JOHN BANDA