Saturday, May 11, 2013

DKT. MWINYI, WASIOTOA MSAMAHA WA MATIBABU YA AFYA KUKIONA.


WAZIRI WA AFYA MH DKT. HUSSEIN MWINYI.

SERIKALI imewaagiza watendaji na wananchi kupitia kamati za o za afya kuhakikisha misamaha inatolewa kwa wote wanaostahili.

Aidha imesema kuwa  kituo ambacho hakifanyi vizuri katika ukusanyaji na udhibiti  wa matumizi ya fedha  zinazotokana kutoa huduma kwa wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), viongozi husika wapewe onyo. Baada ya muda watakaopewa iwapo hakuna mabadiliko  zichukuliwe hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuondolewa madaraka waliyopewa.

Kauli hiyo ilitolewa  na Waziri wa Afya na Ustawi  wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi  wakati akifungua mkutano  wa mkutano mkuu wa mwaka  wa  waganga wakuu wa mikoa , wilaya na baadhi wa wakurungezi wa hospitali za rufaa na taasisi za wizara hiyo wakiwemo wakurugnezi wa asasi za kiraia, wadau wa maendeleo na washiriki kutoka  Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI).

Mkutano huo wa siku tatu umefanyik katika  ukumbi wa mikutano wa St. Gasper mjini Dodoma.
“Mwongozo wa Serikali kuhusu sera ya  ucahangiajia wa huduma za afya  nchini unajulikana. 

Lakini kuna vituo ambavyo bado vinaendelea kutoza gharama za uchangiaji wa huduma ,kwa  makundi ya watu ambayo sera inaelekeza huduma zitolewe bila malipo. Wizara imekuwa  ikilamzimika kujibu  malalamiko mengi kuhusu  vituo ambavyo havitekelezi maelezo hayo,

Nimeambiwa kuwa katika ukusanayaji wa fedha zinazotokana na kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF ,  vituo binafsi vinaongoza kupata  fedha nyingi kuliko umaa pamoja na ukweli kwamba  wana wagonjwa wachache wanaohudumia.

 Naamini  tunajua sababu “alisema Dk. Mwinyi.
 Hata hivyo alisema wongozo huo unapitiwa ili   uendane na mahitaji ya kisasa.

“Tunajua umuhimu wa vituo vyetu kuwa fedha za kutosha kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi hivyo sisi viongozi lazima tutumie njia zote halali za  kupata fedha ,pia tuweke usimamizi madhubuti wa kukusanya na kutumia fedha hizo, endapo hakutakuwa na  udhibiti  imara uboresahji wa huduma hautakuwepo hata kama kuna fedha nyingi,” alissitiza.

 Alisema kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘Usimamizi Bora wa Utendajia Kazi ndiyo nguzo Kuu katika utoaji wa huduma za Afya na Ustawi wa Jamii’. Hivyo changamoto nyingi zinazojitokeza  katika huduma za afya zinaweza kuondolewa na usimamizi na ufuatiliaji wa utendaji kazi wa walio chini.

 Dk. Mwinyi aliongeza kuwa  tatizo la upungufu wa watumishi katika vituo vya huduma za afya bado lipo. Idadi ya watumishi hao waliopo hadio kufikia Aprili mwaka 2013ni 64,449, ambayo ni asilimia 47 yawanaohitajika katika vituo hivyo.

 Kwa upande wake  Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Dk. Rufaro Chatora  alisema  anampongeza waziri  huyo kwa kujibu hojan kwa umahiri  na kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo.

Aliongeza kuwa changamoto za kiafya zinazoikabili nchi ya Tanzania, pia kwa nyingine duniani. Hivyo rasilimali kila siku hazitoshelezi, kinachotakiwa ni  kuendelea kuboresha huduma hizo.

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo , Regina Kikuli  alisema mkutano hu unatoa fursa ya kujadiliana namna ya kuboresha huduma hizo.

 Awali akiwakarisha wageni hao katika mkutano huo,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rehema Nchimbi alisema mkoa wake umefanikiwa kutekeleza mpango wa chanjo.

No comments:

Post a Comment