Wednesday, April 30, 2014

UKAWA WATIKISA ZANZIBAR MKUTANO WAFANYIKA KIBANDA MAITI,SOMA HOTUBA ZA VIONGOZI WA UKAWA KILA MMOJA ALICHOSEMA


KATIBU WA SHURA YA MAIMAMU
Katibu wa Shura ya Maimamu na Taasisi za Kiislamu amesema taasisi zote za Kiislamu zinaunga mkono Shirikisho la Serikali Tatu na kwamba walitoa maoni yao mbele ya tume na wanaungana na UKAWA kulidai hilo. Hakuna atakayeweza kuhimili vishindo vya UKAWA na wapenda haki na matumaini kwa ajili ya amani ya kweli nchini kwetu, Tanzania.

Ameishambulia Serikali na CCM kwa uchochezi wa kidini, kuwachonganisha Watanzania, kutokana na kauli ya uchochezi iliyotolewa na Waziri wa Serikali ya CCM, aitwae William Lukuvi tena kanisani akiwasema waislamu. Amehoji je mashehe nao wakifanya hivyo, nchi itatawalika?

Ametoa rai kwa viongozi wa UKAWA kuimarisha UKAWA na kuhakikisha kuwa UKAWA haufi.
 
ISMAIL JUSSA
Jussa alipanda kuwakilisha wabunge wote wa UKAWA kutokea Zanzibar. Amewaambia Wazanzibar wawe tayari kuwasaliti na kuwazomea wale wote wanafiki wanaowasaliti wanapofika Dodoma kama Asha Bakari.

Amesema Wazanzibar wawashukuru watu kama akina Freeman Mbowe, James Mbatia, Tundu Lissu, John Mnyika na UKAWA nzima kwa kuwa wamesimama kidete kuitetea Zanzibar tofauti na Wazanzibar wengine kama akina Asha Bakari, Balozi Seif Idd na wawakilishi wote wa CCM kutoka Zanzibar.

Amemtangaza Balozi Seif Idd kuwa adui namba moja wa Zanzibar kwa ububu wake bungeni kama kiongozi mkuu kutoka Zanzibar ndani ya Bunge Maalum la Katiba.

Akaongeza kusema ujanja ujanja wanaotaka kufanya wa kubadilisha sheria ya mabadiliko ya katiba kuondoa sharti la 2/3 anasema wafanye wafanyavyo lakini hawataweza kwa kuwa mtarimbo umeganda.

Jussa akasema yeye alikuwa anaweza uwanja sawa tu lakini mchezaji hasa ni anayekuja punde ambaye ni Tundu Lisu.

TUNDU LISSU
Wazanzibar wanamwita Lissu Christiano Ronaldo. Wananchi wameshangilia balaa alipoanza kwa kuwasalimia kwa jina la Zanzibar Huru na Tanganyika Huru na Shirikisho lenye hadhi kuu ya nchi.

Kwa miaka 50, anasema Tundu Lisu, Zanzibar imekuwa koloni la Tanganyika, Zanzibar imefungwa minyororo na Tanganyika na sio huru tena.

Kwa miaka 50 masuala yote ya nje yamekuwa yakiamriwa Dar es Salaam, Mambo ya Ulinzi yanaamriwa na Dar, masuala ya fedha ya Zanzibar yamekuwa yakifanywa na Dar na kwa hiyo ni koloni la Tanganyika.

Anasema mtia minyororo kwa mtu mwingine naye pia hawezi kuwa huru. Akatolea mfano wa mfunga minyororo wa magereza kuwa naye hawezi kuondoka., hivyo Tanganyika iliyoifunga Minyororo Zanzibar nayo haiko huru.

Akasema Tanganyika ilikana jina lake na kuliondoa kwenye katiba ili iendelee kuinyonya Zanzibar, anasema ilikuwa na Tanganyika huru ni kuwa na Zanzibar huru.

MAALIM SEIF
Maalim Seif  kaanza kwa kumtambulisha Mzee Moyo ambaye alikuwa Waziri wa Katiba wa Mzee Abeid Amani Karume, Mzee Moyo kasema 'ni tatu, tatu, tatu bila mzaha'. Kasema leo anaacha majembe yazungumze.

Maalim amesema kama wanaogopa Shirikisho la Serikali Tatu, basi yeye yuko tayari kuunga mkono serikali mbili kwa maana ya Zanzibar huru na Tanganyika huru, tofauti na hapo kila mtu na lwake.

Maalim anawatambulisha viongozi wa UKAWA nje ya bunge, akianza na Mosena Nyambabe- Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi.

Maalim Seif akaongeza kusema kuwa kama Kikwete anao uwezo wa kuwadhibiti Wazanzibar basi aende na cha moto kitaonekana.

Amesema kuwa kuna magari yameletwa kwenye mkutano na vikosi vya KMKM, akaasa kuwa ole wake aguswe mtu akasema anazungumza kama Makamu wa Rais, watajua jini liliko Zanzibar, uwanja ukalipuka kwa shangwe na nderemo.

DR SLAA
Dkt. Slaa amesema kuwa Jeshi la Tanzania halijakosa uzalendo kama walio nao mafisadi wa CCM na serikali yake. Kutokana na uzalendo ambalo JWTZ linao kwa wananchi na nchi, haliwezi kupindua serikali eti tu kwa sababu ni Shirikisho la Serikali Tatu.

Anasema kuwa wanajeshi wetu wamekuwa wazalendo kiasi cha kuvumilia kukosa mishahara, maslahi yao madogo na shida nyingine iweje wafanye hivyo kwa serikali tatu, amesema Kikwete halijui jeshi ndiyo maana amepotoka...

Maalimu Seif aliendelea ambapo aliwasihi viongozi wa UKAWA kujiimarisha na kuulinda UKAWA kwani wabaya wao wanajipanga.

Akasema kuwa wakati wa kutishana tishana umeshapita. Kuendelea kutisha Wazanzibar ni kuwaongezea ari na hamasa.

MAKAIDI
Makaidi amesema kuwa Watanganyika wamebakia bila serikali kwa sababu Mwalimu Nyerere Baba wa Taifa aliitupa serikali yote ya Tanganyika kwenye Muungano na Karume hakuitupa yote na ndiyo maana wamekuwa ngaringari leo.

Amewaomba Wazanzibar kuungana na Watanganyika kudai serikali zao...

Makaidi anasema CCM hakuna wanasiasa bali wajasiriamali na ndiyo maana hawataki kujisahihisha kama Mwalimu alivyotaka. Kisha akapanda Mtikila..
 
MTIKILA
Mtikila; Kinachowasumbua CCM kuhusu serikali tatu ni unywani. Watanganyika wanapumbazwa kuwa uhuru ni mizinga uwanja wa taifa. Anasema kuwa kuwatisha wananchi na majeshi ni ugonjwa wa apedomia. Wanasahau kuwa wanajeshi wana ndugu zao wengi uraiani. Akamalizia kwa kusema saa ya ukombozi ni sasa...
 
JAMES MBATIA
Mbatia; muungano haukuridhiwa kwa sheria za Zanzibar kwa hiyo ni batili. Anasema Zanzibar kujitangazia mamlaka yake ni kuikomboa Tanganyika. Amesema kuwa wajumbe wa UKAWA kutoka Zanzibar wamewanyima turufu majiCCM huko BMK hivyo asitokee mtu wa kuisaliti Zanzibar.

Amesema kuwa chokochoko za udini zinapandikizwa na CCM, lakini hazitafua dafu. Anasema huwezi kuwa muislamu safi halafu ukahubiri udini na ubaguzi wa aina yoyote, huwezi kuwa Muislam safi kisha ukahubiri matusi na kejeli. Vivyo hivyo kwa mkristo safi.

MBOWE
Mbowe; maandamano nchi nzima ya kudai Katiba Mpya na bora inayotokana na maoni ya wananchi yanakuja baada ya mikutano ya Zanzibar. UKAWA haitarudi bungeni kushiriki dhambi ya kupingana na maoni ya wananchi, dhambi ya kuhubiri matusi kwa wananchi.

Amesema kuwa UKAWA huu si kwa ajili ya Katiba tu bali ni kwa ajili ya maslahi halisi ya wananchi. Ametangaza rasmi kuvunja Baraza Kivuli na sasa ataliunda upya kwa ushirika na NCCR, CUF CHADEMA.

Wananchi wakalipuka kwa furaha baada ya Kamanda Mbowe kutangaza kuwa UKAWA utaendelea hadi uchaguzi.;

LIPUMBA
Prof. Lipumba; wanaopinga serikali tatu kwa kigezo cha gharama hawajielewi. Anasema nchi inaingizwa kuzimu kwa matumizi ya hovyo na mabovu ya serikali kila siku.

Amesema ofisi ya rais inaongoza kwa matumizi ya hovyo. Anatoa mfano ambavyo imekuwa ikitumia mabilioni kwa Rais Kikwete kujitangaza Vasco Da Gama kwa kuzurura ughaibuni.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA IBADA MAALUMU YA KUMUAGA ASKOFU WA KANISA KATOLIKI JIMBO LA DODOMA GERVAS JOHN NYAISONGA ANAHAMIA MPNDA MKOANI KATAVI IBADA HIYO IMEFANYIKA LEO KATIKA KANISA LA MT:PAUL WA MSALABA MJINI DODOMA

Waumini wa Madhehebu ya Roman Katoliki [RC] Jimbo la Dodoma wakiwa
katika ibada maalumu ya Shukurani kwa ajili ya kumuaga Aliyekuwa
Askofu wa jimbo hilo Gervas John Nyaisonga aliyehamishiwa Mpanda.
Mke wa Waziri mkuu Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda, Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma DKT Rehema Nchimbi na viongozi wengine Wakiwa katika ibada
maalumu ya kumuaga aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma Gervas
John Nyaisonga aliyehamishiwa Jimbo la Mpanda.
PICHA NA JOHN BANDA

Tuesday, April 29, 2014

KAVUMBAGU AIKIMBIA YANGA RASMI ATUA AZAM FC.

                                DIDIE KAVUMBANGU ASAINI MIAKA MIWILI AZAM FC

MCHEZAJI WA KLABU YA YANGA DIDIE KAVUMBAGOU AKIWEKA WINO TAYARI KWA KUWEKA DOLE GUMBA KATIKA FOMU ZA MKATABA  NA KLABU YAKE MPYA YA AZAM FC LEO

WALIOPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI YA BASI LA SUMRY MKOANI SINGIDA WAFIKIA 22.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiieXA8f0qZ_ehRoyI62TOqh8KFsxPU1WmWjCC8YugiIKChWkTXClfCWG2Pg3nlaVcxCFi0CleTUoK8yukQCE1CxIiJ7bCahHA39miq4y_oYbJ91XN89UP3tXvXSaU9eVNY-TL3me-YIhPZ/s1600/AJALI+YA+BASI+LA+SUMRY+DAR-MNZ+BARABARA+KUU+DODOMA-MOROGORO+PIX+NO+5.JPGWATU 22 akiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida usiku huu. 
Ajali hiyo imetokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 22 kupoteza maisha eneo hilo. 
Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida. 
Miili 22 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi 18 waliopelekwa hospitalini hapo.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

BASI LA SUMRY LAUA WATU 14 SINGIDA.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiieXA8f0qZ_ehRoyI62TOqh8KFsxPU1WmWjCC8YugiIKChWkTXClfCWG2Pg3nlaVcxCFi0CleTUoK8yukQCE1CxIiJ7bCahHA39miq4y_oYbJ91XN89UP3tXvXSaU9eVNY-TL3me-YIhPZ/s1600/AJALI+YA+BASI+LA+SUMRY+DAR-MNZ+BARABARA+KUU+DODOMA-MOROGORO+PIX+NO+5.JPGWATU 14 akiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida usiku huu. 
Ajali hiyo imetokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha eneo hilo. 
Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida. 
Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

ANGALIA PICHA HIZI ZA JWTZ HALAFU NIPE MAONI YAKO TUNABAKI SERIKALI 2 AU TWENDE SERIKALI 3.

2

8

I

10

7


3

4

5

6

1


12

Thursday, April 24, 2014

MBUNGE WA BUNGE MAALUM DODOMA AANGUKA NA KUKIMBIZWA HOSPITALINI KWA PRESHA.


 Wauguzi na Waganga wa Zahanati ya Bunge mjini Dodoma wakitoa msaada wa huduma ya kwanza na kufanya maandalizi ya kumpeleka Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ziana Mohamed Haji katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma leo baada ya kupata matatizo ya  mshutuko.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambapo pia ni Ndugu na Jamaa wa Mjumbe wa Bunge hilo Ziana Mohamed Haji wakijadiliana na watendaji wa Bunge hilo jinsi ya kumsaidia baada ya kupata matatizo ya mshutuko leo mjini Dodoma.
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambapo pia ni Ndugu na Jamaa wa Mjumbe wa Bunge hilo Ziana Mohamed Haji wakijadiliana na watendaji wa Bunge hilo jinsi ya kumsaidia baada ya kupata matatizo ya mshutuko leo mjini Dodoma.

Wednesday, April 23, 2014

MJI WA DODOMA NA KASHFA YA BIASHARA YA NGONO/UKAHABA KIPINDI CHA BUNGE.

BIASHARA ya ngono katika mji wa Dodoma imeshika kasi kubwa ambapo imebainika kuwa wateja wakubwa ni watumishi wa serikali, wanasiasa na madereva.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuwa katika biashara hiyo kuna makundi mbalimbali yanayotofautiana kwa malipo ya biashara hiyo.

Wapo wanafunzi wa vyuo vikuu na wanawake ambao wamedai kuwa wanalazimika kufanya biashara hiyo kutokana na kubanwa na maisha, hususani katika marejesho ya mikopo wanaichukua kutoka katika taasisi mbalimbali ya kifedha.

Mmoja wa wafanyabiashara ya ngono (jina tunalo) bila kujua anaongea na nani, alieleza kuwa kwa sasa katika mji wa Dodoma kuna ushindani mkubwa wa biashara ya ngono kwani wanafunzi wa vyuo vikuu vya mjini hapa vimeteka soko hilo.

Alisema kutokana na ushindani huo kwa sasa kima cha chini ni sh 7,000 kwa mchepuo mmoja na sh 30,000 hadi 40,000 kwa kulala.

Mfanyabiashara huyo alieleza kuwa wateja wakubwa wa ngono ni wafanyakazi wa serikali, wanasiasa (wabunge), madereva pamoja na wafanyakazi wa benki.

Bila hofu mfanyabiashara huyo alieleza kuwa kuanzia muda wa saa tatu hadi sita usiku wanajipanga katika maeneo ya biashara na yanapofika magari hujipanga mbele ya gari ili mteja amchague anayemtaka.

“Hapa tupo wengi, lakini pia wengine ni wafanyakazi wa serikali wanakuja hapa kujiuza, wanafunzi wa vyuo vikuu nao hivyo hivyo… Mimi nipo hapa ninakuja kwa siku maalum ambazo ninakuwa nimekwama.

“Ninakabiliwa na masuala ya mikopo. Unajua hapa tupo kama kumi akina mama ambao tumekopa mikopo katika taasisi mbalimbali, lakini mitaji inapoyumba unajiuliza utapata wapi, unalazimika kuja kufanya biashara,” alisema.

Aliongeza kuwa kwa kawaida mtu mmoja anaweza kufanya ngono na watu wasiopungua saba kwa siku, hivyo ana uhakika wa kujipatia kiasi cha sh 70,000 iwapo siku itakuwa nzuri.

Alibainisha kuwa na kama siku ni mbaya anaweza kupata kiasi cha sh 49,000 iwapo atalipwa sh 7,000 kwa mchepuo mmoja.Uchunguzi wa kina uliofanyika umebaini maeneo ambayo yana wasichana wengi ambao ni makahaba ni Chako Nichako, Double H na Mtaa wa Uhindini ambako kuna gesti maarufu kwa kufanya biashara hiyo.

Hata hivyo, imebainika kuwa makahaba wa vyuo vikuu viwango vyao ni kuanzia sh 200,000 kulala na sh 30,000 kwa mchepuo mmoja.

Mmoja wa waendesha bodaboda ambaye hakutaka jina lake litajwe, alieleza kuwa katika biashara hiyo yapo maeneo ambayo kwa sasa kuna wakala wenye kundi kubwa la wasichana anaowauza.

Wakati biashara ya ngono ikionekana kushamiri, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Nchimbi alishatangaza kuwawinda na kuwatia kwenye mikono ya sheria wale wanaojihusisha nayo.

Hata hivyo, kauli hiyo inaonekana kukosa mashiko kwani biashara hiyo inazidi kushamiri siku hadi siku.

Imeandikwa na

Danson Kaijage, Dodoma

Tuesday, April 22, 2014

MBUNGE SOMALIA AUWAWA KWA BOMU.

Polisi wa Somalia akiangalia mabaki ya mlipuko wa gari lililopigwa bomu huko Mogadishu, Somalia, Jumatatu, April, 21, 2014.
Walinda amani wa Umoja wa Afrika Somalia.
Walinda amani wa Umoja wa Afrika Somalia.
Mbunge mmoja wa Somalia ameuwawa kwa bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari huko Mogadishu.
Isak Mohamed Ibrahim aliuwawa wakati bomu lililokuwa limefichwa kwenye gari yake lililpolika kwenye makao makuu ya wilaya ya Hamar Weyne.
Mbunge mwingine Mohamed Abdi alijeruhiwa katika shambulizi hilo. Shambulizi hilo na majeruhi vilithibitishwa na ofisi ya waziri mkuu wa Somalia .
Kundi la wanamgambo la Alshabab la Somalia limedai kuhusika na shambulizi hilo.
Kundi hilo limepoteza maeneo yake mengi iliyokuwa ikidhibiti katika miaka ya karibuni kwa majeshi ya Umoja wa Afrika na serikali ya Somalia. Lakini wanajeshi hao waliendelea kufanya mashambulizi ya kila mara .
Mwezi Februari watu 17 waliuwawa wakati wapiganaji wa Alshabab walipovamia ikulu ya rais. Rais Hassan Sheikh Mohamud hakujeruhiwa katika shambulizi hilo

Monday, April 21, 2014

WATU WANAODAIWA KUWA NI POLISI,MGAMBO NA JWTZ WAVAMIA SHAMBA LA MKULIMA NA KUFYEKA MAZAO YOTE

Na John Banda, Chamwino
WATU wanaodhaniwa kuwa ni migambo, polisi na wanajeshi wa Jeshi la
wananchi [JWTZ] wakiwa na Bunduki walivamia shamba la Mkulima Msafili
Khatib lenye ukubwa wa hekar 13 na Kufyeka mazao yote yaliyokuwa
shambani humo yakiwemo Mahindi yaliyokuwa yamekomaa na kuchoma vibanda
2 kwa moto wa Petrol na kuiacha familia hiyo ikikosa makazi na
chakula.
Tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Chenene Walayani Chamwino
Dodoma Wiki iliyopita linahusishwa na viongozi wa kijiji hicho akiwemo
Afsa Mtendaji Ester Mhwaji na Mwenyekiti wa Kijiji Gilbert Chitung’ati
Akiongea kwa Masikitiko kuhusiana na Tukio hilo Khatib alisema April
14, 2014 saa 9 alasili Dk chache baada ya kutoka kuzozana na Afsa
mtendaji aliyekuwa akimlazimisha Mmoja wa Maofisa Toka Wakala wa
Barabara aliyefika kumsainisha ili baada ya mavuno alipwe fidia ya
shamba lake.
Alisema yeye akiwa hapo shambani alishtukia kundi kubwa la watu
wanaokadiliwa zaidi ya 30 wakiwa na mapanga na mafyekeo huku watatu
kati yao wakiwa na Bunduki mkononi walifika na kuanza kufyeka mazao
yake huku wakimkejeli nay eye awasaidie kazi hiyo walipomaliza azma
yao na kuhakikisha wamechoma kwa moto wa petrol vibanda 2 walivyokuwa
kitumia kwa makazi wakaondoka.
‘’Walifika watu hao na watatu kati yao walikuwa na Bunduki mkononi,
waliokua wamevalia sale za polisi, za jeshi la wananchi [JWTZ] na za
mgambo huku wengine walivaa za kawaida kitendo hicho kimenitia
umasikini na kunifanya niishi kama wanyama na familia yangu yenye
watoto 5 kwa kukosa pa kulala na chakula kwani tayali mahindi
yalishakomaa na tulikuwa tunayala’’, alisema
Naye Meresiana Kalunju Mke wa mkulima huyo alisema tukio hilo
lilitokana na chuki za viongozi wa Serikali ya kijiji hicho cha
Chenene Afsa mtendaji na Mwenyekiti ambao kwa makusudi waliamua
kumlazimisha Mumewe akubali fedha za fidia ya shamba hilo zipitie
mikononi mwao ndipo azipate na alipokataa wakaamua kumkomoa kwa njia
hiyo.
Alisema mtendaji aliwaambia eneo hilo lipo sehemu ya hifadhi hivyo
watu wa maliasili watafika mashambani  na watakachokifanya  wawaache,
lakini cha kushangaza wamefyeka mazao yao tu huku wakiacha mashamba
mengine  yaliyozunguka shamba lao likiwemo la Mjumbe wa kamati ya
Misitu John Selemani  kisa wachina wamechagu eneo hilo ili kujenga
kiwanda cha Kokoto.
‘’Mwandishi tusingeweza kukubali fedha hizo zipitie mikononi mwa
viongozi hao kwa sababu mwezi wa pili mwaka huu Kampuni ya kichina
iliwaliwapa viongozi hao malipo ya eneo la mashamba ya wananchi ili
waweke makambi yao kwa ajili ya ujenzi wa barabara, chakushangaza
mtendaji akali watu 70,000 kwa heka moja na wengine kulipwa 200,000
heka 5 tukalalamika ndiyo sababu Tanroad wamekuja kusimamia ulipaji
huu’’,alisema
Aidha alisema shamba hilo la hekari 13 lifanyiwa udhamini  siku hiyo,
waliambiwa kati ya mwezi wa 6,7 watakapovuna ujenzi wa kalai la
kusagia kokoto utafanyika mara baada ya kulipwa na ofisi ya Wakala wa
Barabara kwa mkataba wa miaka 3 baada ya hapo watarudishiwa maeneo
yao.
Akizungumzia tukio hilo Afsa Mtendaji wa kijiji hicho Ester Mhwaji
alisema ameshtushwa na tukio hilo na Vilevile anasikitishwa na meseji
ambazo alipokea zikimuonya kutokubali Mkulima huyo kulipwa fidia ya
mazao na Aridhi jambo ambalo aliamua kuliwekla wazi kwa wathamini
waliotoke manispaa.
‘’Tulipomaliza na Yule Mthamini tuondoka na baadae nikajulishwa juu ya
tukio hilo, na vitisho vikafuata toka kwa wakulima  nikiambiwa
nitachomwa mishale na usiku nisitoke kujisaidi la sivyo nitauawa hali
iliyonifanya kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi’’
‘’,Lakini Nimeshangazwa sana na kwa ajili ya usalama wangu naomba
nisiwataje lakini hapa nina ujumbe wa maandishi kwenye simu ulionionya
nisikubali mkulima Msafili Khatib Alipwe fidia, lakini pia sina cha
kufanya maana jioni ya siku hiyo nilipokea ujumbe wa simu toka namba
nisiyoijua ukinijulisha kuwa misitu wamefyeka mazao Chenene na Solow,
na kwanini wafyeke mazao yaliyopo shamba moja tu?’’, alihoji Ester
Mwenyekiti wa kijiji hicho Gilbert Chitung’ati alisema hawezi
kuzungumzia swala hilo hata kama halikupitia ofisi ya mtendaji kwa
sababu lilitokea ngazi za juu.
 Mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino alisema huyo mkulima ni haki yake
kulipwa fidia na kwa kuwa ndiyo kwanza amelipata atalifuatilia ili
ajue nani na kwanini wamefyeka ndipo atachukua hatua juu ya tukio
hilo.
Kampuni ya Kichina ya Chico iliyoweka kambi katika kijiji hicho cha
Chenene ndiyo iliyopewa tenda ya kuchonga Barabara ya kiwango cha Lami
kati ya kijiji mtungutu na babati.