Tuesday, February 27, 2018

LISSU AZUNGUMZIA KUFUNGWA KWA SUGU AKIWA UBELGIJI.



Waheshimiwa wangu salaam kutoka Ubelgiji. Nawapeni pole nyingi kwa yaliyomkuta Mh. Sugu na Goddie Masonga siku ya leo.
.
Naomba kuzungumzia suala hili kwa kirefu kidogo. .
Kwanza, hukumu ya leo sio mwisho wa mjadala mahakamani. Bado kuna fursa, nay haki, ya rufaa High Court na, ikibidi, Court of Appeal.

Pili, hukumu ya leo haina maana Sugu atakaa gerezani muda wote huo. Kuna haki ya dhamana pending appeal. Ndivyo ambavyo tumefanya kwa viongozi na wanachama wetu wengi in the past. .
Tatu, hukumu ya leo haina athari yoyote kwa ubunge wa Sugu. Katiba inaweka masharti ya kifungo cha miezi sita au zaidi, na kwa makosa ya ‘utovu wa uaminifu.’ Uchochezi au kutoa lugha ya matusi sio makosa ya utovu wa uaminifu. .
Nne, pamoja na kwamba sijaona nakala ya hukumu, adhabu ya kifungo bila faini kwa kosa la kwanza ni kinyume na sentencing principles. Hii ni mojawapo ya hoja zetu zilizoshinda katika kesi ya Mh. Juakali High Court mwaka jana. .
Tano, hata kama atakaa gerezani muda wote huo, hukumu za kesi za kisiasa kama hii hazijawahi kuwapunguzia heshima wapigania haki popote pale duniani. .
On the contrary, kifungo cha aina hii ni beji ya heshima kwa kila mpigania haki na uhuru. Orodha ya mifano ni ndefu sana: Nyerere (ijapokuwa yeye alilipa faini), Kenyatta, Mandela, Mugabe, Fidel Castro, etc.

Tuesday, January 30, 2018

RAIS JOHN MAGUFULI KUZINDUA PASIPOTI YA ELEKITRONIKI.


Jonas Kamaleki- MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli kesho atazindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo utafanyika Jumatano, Januari 31, 2018 kuanzia saa moja na nusu asubuhi, Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Mrakibu wa Uhamiaji ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda katika mahojiano maalum na Idara ya Habari (MAELEZO).
Mtanda amesema kuwa Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki ni sehemu ya Mfumo wa Uhamiaji Mtandao ambao utakuwa na visa, vibali mbali mbali na manejimenti mipakani.
Kwa kuwa teknolojia inazidi kukua, Tanzania haiwezi kubaki nyuma ndiyo maana imeamua kuingia katika masuala ya digiti.
Uzinduzi huu utahudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.
Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waheshimiwa, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wa Serikali wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo kwa mujibu wa Mtanda.
Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika kutoa huduma zake kwa wananchi kwa njia ya mtandao. Ikumbukwe kuwa usajili wa makampuni chini ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamezindua usajili wa makampuni kwa njia ya mtandao, miamala ya pesa inafanyika kwa kiwango kikubwa kwa njia ya mtandao na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwepo kulipa kodi mbali mbali.

RAILA ODINGA AJIAPISHA KUWA RAIS WA KENYA.



Raila aondoka uwanja wa Uhuru Park


Punde tu alipofika na 'kula kiapo' Raila Odinga ameondoka.
Wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu na ghamu, bila kutegemea kwamba atachukua muda mfupi hivyo.
Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ' si mapinduzi ya serikali'
Raila 'akula kiapo'

Odinga akula kiapo uwanja wa Uhuru Park

Raila Odinga amefika katika pamoja na viongozi kadha wakuu wa NASA na kujiapisha akishika Biblia.
Amewaambia kuwa mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper ataapishwa baadaye.
Viongozi wengine wenza wa Nasa Moses Wetangula na Musalia Mudavadi pia hawakufika katika wuanja huo.
Bw Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya.
"Hatua ya leo ni kuelekea kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya"
"Maelekezo mengine mtayapata baadae"

Bw Raila Odinga amezungumza na kituo cha habari cha KTN kwa njia ya simu ambapo amesisitiza kwamba Rais Uhuru Kenyatta hakuchaguliwa kwa njia halali.
Alipoulizwa anni atamwapisha, amesema: "Ngoja uone” na akasisitiza kwamba wanachokifanya leo kina msingi wake katika sheria na si mapinduzi.
“Hatutambui uchaguzi wa Oktoba 26 (uchaguzi wa marudio ambao Odinga alisusia), zaidi ya asilimia 86 ya Wakenya hawakushiriki. Tuna serikali ambayo si halali ambao inajidai kuwa mamlakani,” amesema.
Kuhusu taarifa kwamba amepokonywa walinzi, amesema: "Walinzi wangu waliondolewa muda mrefu sana uliopita. Najihisi kuwa hatarini ndio lakini watu raia ndio usalama wangu.”
Bw Odinga ameitaka serikali kutotumia nguvu kuusambaratisha mkutano wa leo.
"Wafuasi wangu wamo safarini kuelekea Canaan. Safari yetu ni halisi na haiwezi kuzuiwa.


  • Raila Odinga azungumza na vyombo vya habari dakika chache kabla ya kuelekea ‘kuapishwa’.
    Akizngumza kwa njia ya simu na kituo cha habari cha KTN, Odinga amesema kuwa hawakutarajia kufungwa kwa vyombo vya habari.
    Ni hali ya ‘kusikitisha’ na ‘inaonesha kuwa tumefika kiwango cha Uganda.'
    Alipoulizwa nani haswa atamuapisha, Odinga alijibu ‘ngoja uone.’
    Alielezea kuwa shughuli yao ni halali na haikiuki katiba. Pia amesema haamini kwamba wanachokifanya si mapinduzi ya serikali.

    MH RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE JAKAYA KIKWETE AKIWA ADDIS ABABA ETHIOPIA.

     Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu  Mstaafu wa Lesotho Mhe. Tom Thabane.
     Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Rais wa Zimbabwe Mhe Emerson Mnangagwa.
     Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete na akiwa na Rais Zuma wa Afrika Kusini
     Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na akiwa na Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dkt. Thomas Kwesi Quartey.
     Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na akiwa wake za waasisi wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika. kushoto kwake ni Mama Maria Nyerere na kulia kwake ni Mjane wa Hayati Rais Obote wa Uganda..
    Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na Rais wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina 
    Rais Mstaafu na Mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika Usulihishi wa Mgogoro wa Libya, Dkt. Jakaya Kikwete katika taswira mbalimbali akiwa Addis Ababa, Ethiopia katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika

    Tuesday, November 28, 2017

    MEYA IRINGA NA MAKADA WATANO CHADEMA WAFIKISHWA MAHAKAMANI


    Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe mwenye koti la suti akitolewa mahabusu kwenda mahakamani kusikiliza kesi ilitolewa ikimkabili ya kutishia kuua kwa bastola 
    Meya kushoto akiwa chini ya ulinzi
    MSTAHIKI meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe (chadema) amepandishwa mahakamani kwa kosa la kutishia kumuua katibu wa UV CCM wilaya ya Iringa mjini Alphonce Myinga wakati wa zoezi la uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kitwiru.

    Meya Kimbe alifikishwa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Iringa John Mpitanjia leo majira ya saa 3 asubuhi na kusomewa shitaka hilo la jinai kesi namba 189 /2017.

    Akisoma shitaka hilo wakili wa jamhuri Allysniki Mwinyiheni alisema kuwa Kimbe alitenda kosa hilo Novemba 26 mwaka huu katika eneo la Kitwiru mjini Iringa kwa kumtishia kumuua kwa bastola Myinga .

    Hata hivyo Kimbe alikana kosa hilo na kesi hiyo kuja tena mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa Desemba 12 mwaka huu na meya huyo yuko nje kwa dhamana baada ya mahakama kukubali kumpa dhamana .

    Wakati huo huo makada watano wa Chadema jana walifikishwa mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya mkoa wa Iringa Richard Kachele kwa makosa matatu likiwemo la unyang’anyi .

    Wakili wa jamhuri alisema mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao Martha Robarth , Leonard Kulujila, Christopher Gerlad,Samweli Nyanda na Asau Bwile kwa pamoja wanashitakiwa kwa makosa matatu ambayo ni kujeruhi, Unyang’anyi wa kutumia nguvu na utekaji .

    Kuwa tukio hilo walilifanya Novemba 19 mwaka huu eneo la Kitwiru kwa kumteka Dikri Frank kada pamoja na kumteka walimpokonya simu yake ya mkononi yenye thamani ya shilingi 100,000 pamoja na kadi ya CCM moja.

    Washitakiwa hao ambao wanatetewa na wakili CHarzy Luoga walikana kosa hilo na kunyimwa dhamana kutokana na kosa la unyang’anyi katika kesi hiyo namba 190/2017 kutokuwa na dhamana .

    Wakili wa washitakiwa hao aliiomba mahakama kuagiza wapelelezaji wa kesi hiyo kufanya haraka kwani wateja wake wana maumivu na mmoja hawezi hata kusimama baada ya kuumizwa na polisi wakati walipokamatwa .

    Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 12 mwaka huu itakapofikishwa tena kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wote walirudishwa mahabusu

    Thursday, September 14, 2017

    VITA YA SPIKA JOB NDUGAI NA MH ZITO KABWE SASA YAFIKIA HAPA.

    Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai, amesema ana uwezo wa kumzuia Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuzungumza mpaka mwisho wabunge, kwani hawezi kupambana naye.
    Spika Ndugai ametoa kauli hiyo Bungeni ambapo amesema Zitto Kabwe hawezi na hapaswi kujibizana naye, na kumtaka Zitto Kabwe kutomfananisha na aliyekuwa Spika wa Bunge marehemu Samuel Sitta, kwani hawezi kufanana naye na kila mtu ana muda wake, kama ambavyo Spika wa bunge aliyepita mama Anna Makinda alivyokuwa na muda wake kuliongoza bunge hhilo
    “Hawa ni watu nawaheshimu sana na wamenilea sana na ni sehemu nilipofika hapa leo. Utanilinganishaje mimi na milima mikubwa kama Kilimanjaro? Hata siku moja sikio haliwezi kuzidi sikio,” amesema.
    Amesema katika Bunge la 9 Zitto aliwahi kupeleka hoja ya Mgodi wa Buzwagi ambayo ilikataliwa na Bunge lakini ikazuka hoja ya kimaadili ambapo alihukumiwa hapo hapo.
    “Alihukumiwa hapo hapo akapigwa miezi mitatu. Mnatakaniende mkuku mkuku kama lile la Bunge la tisa nifanane na mzee Sitta? Hilo pia naliweza kwa nini mnaalika matatizo nashangaa unapambana na Spika,” amesema.
    “Ninauwezo wa kupiga marufuku kuzungumza hadi miaka yote mitano iishe hauna pa kwenda, hakuna cha swali, nyongeza wala kuzungumza utanifanya nini?Amemtaka kupambana na mtu mwingine lakini sio yeye.”Kwa haya ya Spika sina sababunayo lakini ya kulidharau Bungehayo sitaweza kuyavumilia nitalinda mihimili huu kwa nguvu zangu zote,” amesema.
    Amesema hawawezi kuacha wabunge kulidhalilisha Bunge na kuhoji kwamba watachukuliaje Watanzania wengine watakapolidhalilisha Bunge.Amesema hilo kosa la pili kwa Zitto na kuagiza liende katika kamati ya maadili.
    “Tutaenda sambamba mguu kwa mguu hadi kieleweke,” amesema juzi Spika Ndugai alimtaka Zitto Kabwe kufika kwenye kamati ya maadili kutoa maelezo juu ya taarifa alizoziweka kwenye mtandao, na Zitto Kabwe kumjibu kuwa mambo anayoyafanya Spika yanaporomosha bunge

    YUSUPHU MANJI SASA RASMI YUKO HURU.


    Image result for manji yusuf mahakamani
    KISUTU: Mahakama imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo ikionyesha kuwa hana nia ya kuendelea na kesi dhidi yake.
    Manji na watuhumiwa wenzake watatu walikuwa wakikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na plate number mbili za magari ya serikali.
    Watuhumiwa wengine walioachiwa huru kwenye kesi hiyo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja.