Sunday, March 31, 2013

Saturday, March 30, 2013

BREAKING NEWS:UHURU KENYATA ALICHAGULIWA KIHALALI

BREAKING NEWS: Mahakama Kuu nchini Kenya imetoa rasmi hukumu yake dhidi ya kesi ya kulalamikia matokeo yaliyotangazwa na IEBC yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake Willliam Ruto.

Mahakama hiyo imeamua kwamba Uhuru Kenyatta na William Ruto walichaguliwa kwa njia ya haki.
 Mahakama Kuu nchini Kenya imetoa rasmi hukumu yake dhidi ya kesi ya kulalamikia matokeo yaliyotangazwa na IEBC yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake Willliam Ruto.

Mahakama hiyo imeamua kwamba Uhuru Kenyatta na William Ruto walichaguliwa kwa njia ya haki

ULINZI KENYA BALAAAAH

Picha: Maafisa wa polisi waliofunga barabara ya City Hall Way karibu na mkahawa wa Hilton kuzuia umma kukaribia majengo ya Mahakama ya Juu uamuzi kuhusu kesi ya uchaguzi wa urais unaposubiriwa. Picha/ANTHONY OMUYA
Picha: Maafisa wa polisi waliofunga barabara ya City Hall Way karibu na mkahawa wa Hilton kuzuia umma kukaribia majengo ya Mahakama ya Juu uamuzi kuhusu kesi ya uchaguzi wa urais unaposubiriwa. Picha/ANTHONY OMUYA NAIROBI

MAITI ZILIZOCHOMOLEWA KATIKA MABAKI YA JENGO LA GHOROFA 16 LILILOPOROMOKA JANA JIJINI DAR ES SALAAM SASA ZAFIKIA 18... MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM SAID MECK SADICK ATHIBITISHA IDADI HIYO YA WAFU...

Mashuhuda wakiangalia jengo lililoporomoka asubuhi hii katika makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi jijini Dar es Salaam jana Machi 30, 2013.

 




Idadi rasmi ya watu waliokufa kufuatia ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa 16 kwenye makutano ya Morogoro Road na Mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es Salaam imefikia 18 na inatarajiwa wengine zaidi watapatikana kutokana na shughuli za kunasua wahanga zaidi zinavyoendelea.

Taarifa iliyothibitishwa na afisa wa ikulu aliyemkariri mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick imedai kuwa hadi sasa shughuli za kuchimbua kifusi cha mabaki ya jengo hilo zinaendelea kufanywa kwa ushirikiano wa vikosi mbalimbali vya uokoaji, wataalam na vifaa kutoka makampuni mbalimbali ya ujenzi na pia kwa msaada wa vijana kibao waliomwagwa kutoka ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Tukio hilo lilitokea jana asubuhi katika mitaa ya Posta, jirani na msikiti wa Shia katika eneo la makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi.

Jana, viongozi mbalimbali wa serikali na makamanda wa Polisi katika kanda maalum ya Dar es Salaam walifika kuangalia mwenendo wa shughuli za uokoaji, miongoni mwao akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sadick ameamuru kusimamishwa mara moja kwa ujenzi wa jengo jingine la ghorofa 16 linaloendelea jirani tu na eneo lilikoanguka jengo la leo na kutaka kwanza kufanyike kwa uchunguzi zaidi ili kujiridhisha kuwa hatua za kiusalama na ubora wa jengo hilo zimefuatwa ili kuepuka maafa mengine.

Akizungumza jana jioni kupitia kituo cha televisheni ya taifa (TBC1), Sadick alisema kuwa serikali imeamua kusimamisha jengo hilo baada ya kubaini kuwa linafanana kwa kila kitu na jengo lililoanguka leo, ikiwa ni pamoja na mmiliki wake na pia mkandarasi anayeendelea na ujenzi huo.

KUANGUKA KWA HILI GHOROFA JIJINI DAR NANI ALAUMIWE?SERIKALI AU MMILIKI?

Tuesday, March 26, 2013

HUU NDIO UKUMBI WA MIKUTANO WA JULIUS NYERERE.


 Hili ndilo jengo la Mikutano la Julius Nyerere lililojengwa jijini Dar es Salaam kwa msaada wa Serikali ya watu wa China. Ukumbi huo unawezo wa kuchukuwa watu 1800


Monday, March 25, 2013

BREAK NEWS.KAJALA YUKO HURU.WEMA MKOMBOZI WAKE AMLIPIA FAINI YA TSH 13 M

MSANII Wema Sepetu amemlipia faini ya shilingi milioni 13 msanii mwenzake, Kajala Masanja, na kumfanya awe huru. Mapema leo, hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili mcheza filamu za Kitanzania anayefahamika kwa jina la 'Kajala Masanja' na mumewe mbele ya Hakimu 'Sundi Fimbo' kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es salaam. 
Katika hukumu hiyo 'Kajala' amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200. 
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe 'Faraji Agustino' kukumbwa na makosa ya kutakatisha fedha haramu.
Hata hivyo baada ya hukumu hiyo kutolea mahakamani hapa, mwanadada maarufu hapa Bongo anayefahamika kwa jina la Wema Sepetu' aliweza kujitolea yeye mwenyewe kiasi cha Tsh. milioni 13 kutoka mfukoni mwake kwa ajili ya kumlipia msanii mwenzake wa filamu 'Kajala' asiweze kutumikia adhabu ya kifungo hicho cha miaka 5 jela. 

Hii ni mara ya pili kwa msanii 'Wema Sepetu' kujitolea kiasi kikubwa cha fedha kusaidia msanii mwenzake.!
Kwa sasa Kajala yupo nyumbani kwao maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam pamoja na ndugu na jamaa

RAIS WA CHINA XI JINPING AKABIDHI RASM UKUMBI WA MIKUTANO WA KIMATAIFA KWA RAIS WA TANZANIA JAKAYA KIKWETE.




Rais Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ufunguo kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya  Watu wa China Mhe.Xi Jinping wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa  Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  leo.Ukumbi huo umejengwa kwa ushirikiano kati ya Seriklai ya China na  Tanzania.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Xi Jinping wa China wakishangilia
jambo wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wageni waliohudhuria sherehe za  makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo  jijini Dar es Salaam.

STARS ILIVYOUA WAMOROCCO TAIFA.


 Mshambuliaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) Thomas Ulimwengu, akichezewa vibaya na beki wa Morocco, wakati wa mchezo wa Kundi C wa Kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Mchezo huo umechezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa, ambapo timu ya Taifa Stars, imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 huku bao la kwanza likifungwa na Thomas Ulimwengu katika dakika ya 46, na mabao 2 yakifungwa na Mbwana Samatta katika dakika ya 67 na 80.
 

''Leo Mtanijua tu'', Ni Thomas Ulimwengu akionyesha uwezo mbele ya beki wa Morocco.....
 
 Samatta (kushoto) na Ulimwengu, wakishangilia baada ya kutupia...
 
 Wachezaji wa Stars, wakishangilia bao la pili....
 Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kuipa sapoti timu ya Taifa....

KUWASILI KWA RAIS WA CHINA MH XI JINPING NCHINI TANZANIA.



Thursday, March 21, 2013

HAPA NDIO KWANZA SHUGHULI INAANZA NDANI YA PLAYTIME BAR MWENGE

NA  BADO NDIO KWANZA SHUGHULI INAANZA
MC MGANGA NDELE NAE YUMO WINDHOEK ISHAKOLEA MBONA RAHAAAAA
VIJANA WA WINDHOEK  KAZINI HAPA MPAKA KIELEWEKE.

WIDHOEK WAANGUSHA BONGE LA SHOW KATIKA PROMOTION YAO NDANI YA PLAYTIME BAR MWENGE

MA MC WA WINDHOEK LAGER MGANGA NDELE KUSHOTO NA JOBISO WAKIKAMUA VILIVYO KATIKA PROMOTION YA WINDHOEK NDANI YA PLYTIME BAR MWENGE
HAPA KULIKUWA NA KILA AINA YA LADHA YA MUZIKI MPAKA BONDENI
VIJANA WA WINDHOEK LAGER  WAKIJITUMA ILE MBAYA
HII SHUGHULI SI MCHEZO LAZIMA UKUBALI MBELE YA WINDHOEK LAGER NI BALAAH

Kampuni za simu za mkononi zaongoza kutangaza biashara nchini



 Mkurugenzi Mtendaji wa Push Observer, Rubelyn Alcantara akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisini mwa Push Observer, Kinondoni.
 Baadhi ya maofisa kutoka makampuni mbali mbali wakielekezwa jinsi kampuni ya Push Observer inavyofanya shughuli zake kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo

WASHTAKIWA WA KESI YA PONDA WAFUNGWA JELA MWAKA MMOJA KILA MTU LEO.

Washtakiwa 52 kati ya 54 katika kesi ya kula njama na kufanya maandamano isivyo halali wamehukumiwa kwenda jela kila mmoja baada ya kukutwa na makosa matatu huku mmoja akiachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia na mwingine kufariki dunia kabla ya hukumu iliyotolewa leo na hakimu Sundi Fimbo wa Mahakama ya Hamimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.  
  
Washtakiwa hao walidaiwa kutenda kosa Februari 15 mwaka huu.

Baada ya pande zote kusikilizwa na washtakiwa kutoa hoja za utetezi, hatimaye hakimu Fimbo alitoa hukumu hiyo leo ambapo aliwatia hatiani washtakiwa 52 kwa makosa matatu kati ya manne na kila mmoja akamhukumu kwenda jela mwaka mmoja kwa kila kosa.

Hata hivyo, Fimbo akasema washtakiwa hao watakwenda kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa vile adhabu zote zinakwenda kwa pamoja.

Mshtakiwa aliyeachiwa huru baada ya kukutwa kuwa hana hatia ni Waziri Omari (namba 48), ambaye katika utetezi wake alidai kwamba siku ya tukio alikamatwa wakati akiwa katika shughuli zake za biashara ya kuuza kwa kutembeza barabarani vyombo vya nyumbani ikiwa ni pamoja na mabeseni.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo leo, wakili Mohamed Tibanyendera alimtaka hakimu awapunguzie adhabu wateja wake kwavile wengi wao wanategemewa na familia zao na kwamba, tayari walishakaa mahabusu kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja.

Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Salum Makame, Said Idd na Ally Nandumbi, Makame, Idd na Nandumbi, Hussein Athumani, Seif Rwambo, Abdull Ally, Waziri Swed, Naziru Waziri, Ahmad Rashid, Jumanne Kayogola, Hamis Tita, Amri Diyaga, Salum Said, Rajabu Mpita na Haji Sheluhenda.

Wengine ni Abdul Ahmed, Bakari Mwambele, Ramadhani Fadhili, Awadh Juma, Omari Mkwau, Kassim Chobo, Abubakari Bakari, Ramadhani Milambo, Hamis Ndeka, Athuman Juma, Abdallah Salum, Juma Makoti, Bashir Kakatu, Imam Omari, Rashid Lukuta na Bakari Athumani, Mbwana Kassim, Nurdin Ahmed, Mustapha Mide, Rajabu Kifumbo, Zuberi Juma, Omari Mkandi, Idrisa Katulimo, Sawali Mola, Said Dudu, Ramadhani Juma, Musa Sinde, Issa Sobo, Yahaya Salum, Jabil Twahil, Shomari Tarimo, Hashim Bendera, Waziri Toy, Athuman Yahaya, Yasin Seleman, Shaban Malenda, Yasin Mohamed, Khatib Abdallah na Rajabu Rashid wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.

Awali, ilidaiwa kuwa katika siku ya tukio, wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama za kufanya maandamano isivyo halali.

Shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kusababisha uvunjifu wa amani.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard Kongola, alidai katika shitaka la tatu kuwa siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, washtakiwa wote kwa pamoja baada ya Jeshi la Polisi kutoa zuio la kufanya maandamano, walikiuka amri hiyo na kufanya mkusanyiko ulisababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Katika shitaka la nne, ilidaiwa kuwa mshtakiwa Makame, Idd na Nandumbi, waliwashawishi wananchi kwa kuwasambazia vipeperushi vya kuhamasisha kufanya maandamano yasiyo halali.

VILIO, SIMANZI
Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, vilio vilitawala katika viunga vya mahakama vilivyofurika watu kufuatia baadhi ya ndugu na jamaa wa washtakiwa kuangua kilio, wasiamini kile kinachotokea.

Baadaye washtakiwa walipandishwa kwenye karandinga na kupelekwa gerezani

HAPA BROTHER AANAONYESHA MSISITIZO WA UBORA WAKE.

JEROME RUGEMARILA ,anasema kama hujaonja windhoek ukaona utamu wake jaribu onja leo tsh 2500/= tu.

RAIS JK AKIZINDUA DARAJA KIMARA SUKA DAR-ES-SALAAM.


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kufungua rasmi Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam leo.Kushoto anayeangalia ni mbunge wa Ubungo John Mnyika.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Madabida,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Sadik Meck Sadik,Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda na kushoto ni Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika

SERIKALI YASALIMU AMRI KWA TFF YAKUBALI YAISHE



Serikali imekubali mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uendelee kwa sharti la kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea waliofika mbele ya Kamati ya Rufani ya Uchaguzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao kati ya uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri Dk. Fenella Mukangara, TFF na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Amesema baada ya maafikiano hayo, TFF italiandikia barua Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo ndilo lililosimamisha mchakato huo ili litume ujumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa.
Rais Tenga ambaye ameishukuru Serikali kwa kuruhusu mchakato huo uendelee, pia ameahidi kuwa uchaguzi wa TFF utafanyika kabla ya Mei 25 mwaka huu kama walivyokubaliana na Serikali, na kuwa haki si tu itatendeka bali ionekane imetendeka.
“Serikali imetuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya Mei 25. Tumewaambia kwetu huko ni mbali. FIFA wakija hata kesho wakituambia endeleeni sisi tuko tayari. Hesabu zetu ziko tayari, makabrasha yote yako tayari yanasubiri mkutano tu. Labda itakuwa kutoa muda tu kwa wajumbe walioko mbali waweze kujiandaa, maana wajumbe huwezi kuwaita ghafla,” amesema.
Amesisitiza kuwa TFF ilishapanga tarehe ya uchaguzi, lakini ukasimamishwa na FIFA baada ya baadhi ya walioenguliwa kulalamika huko. Hivyo maneno kuwa TFF hawataki uchaguzi kwa sababu wanataka kuendelea kubaki madarakani haya maana hata kidogo.
Hivyo amewataka wagombea wote waliofika kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi na wakaendelea kujiandaa vizuri, kwani FIFA watakapofika watawasikiliza wao na vyombo vilivyowaengua.
Pia amesema TFF ina heshimu Serikali na itaendelea kufanya hivyo, lakini vilevile lazima iheshimu FIFA sababu iko kwenye mpira wa miguu, na FIFA ndiyo wasimamizi wa mchezo huo duniani.  
Amewakumbusha wanachama wa TFF, hasa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufahamu kuwa TFF ina katiba, lakini ni lazima pia wafahamu kwanini kuna FIFA.
Rais Tenga amewahadharisha watu wanaopitapita mikoani kuomba saini za wajumbe ili kuita Mkutano Mkuu wa dharura wakati wanajua mkutano ulishaitishwa, lakini ukasimamishwa na FIFA. Jambo hilo kikatiba ni kosa