Sunday, May 31, 2015

LIVE KUTOKA CHUO CHA MIPANGO DODOMA MWIGULU NCHEMBA AKITANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS.


Sasa  ni  zamu  ya  Mwigulu  Nchemba  kutangaza  nia  ambapo tayari amewasili katika ukumbi wa Mwl. Nyerere katika chuo cha mipango Dodoma ili kutangaza   nia  yake  ya  kugombea  Urais  kwa  tiketi  ya  Chama  cha  Mapinduzi, CCM.

Hapa  nimekuandikia  pointi  muhimu  anazotoa  Mwigulu Nchemba (Zinaanzia  juu  kuja  juu);

13: Mtu yoyote akithibitika amefanya vitendo vya rushwa, atafilisiwa, atafukuzwa kazi na atafungwa. 
  
12: Rushwa hupofusha macho ya wenye akili na rushwa hurudisha nyuma maendeleo. 
  
11: Awamu ya 5 nataka kuona nchi ikiingia kwenye uchumi wa viwanda na vijana wakifanya kazi kwa shift usiku na mchana .
  
10: Pia jambo lingine la kuzingatia ni Udhibiti wa matumizi mabaya ya fedha na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. 

9:Mambo ya kuzingatia ni Kila mtu kulipa kodi anayostahili na sio kukandamiza wafanyakazi na kinamama wauza vitumbua .

8:Mkataba wa Rais wa awamu ya tano ni juu kazi anazoenda kufanya na sio kazi alizowahi kufanya.  


7: Faida  ya  kuwa  kiongozi  Kijana  ni  kuwa Unafanya kazi ukiwa na nguvu na ukimaliza unapumzika, kwahiyo unajiuliza tena hilo? 
  
6: Kiongozi akipatikana kwa mazoea, atafanya kazi kwa mazoea. Nawaambieni tunataka tukomeshe kufanya kazi kwa mazoea

5: Kukaa sana serikalini si kigezo, unaweza kukaa sana serikalini na ukawa umesababishia hasara kubwa Taifa hili. 


4: Nilipomaliza shahada ya 2  nilibeba zege na mke wangu alipika mama ntilie, natambua tatizo la ajira kwa vijana. 

3: Kiongozi aliyekaa muda mrefu madarakani maana yake ni kwamba amesahau shida za wananchi. 

2: Nimeamua kutangazia nia Dodoma kwakuwa ni Makao makuu ya Nchi na pia makao makuu ya chama.
 
1: Namshukuru MUNGU kwa kuniwezesha leo kusimama mbele yenu kwaajili ya kutangaza jambo kubwa kwaajili ya nchi yetu 

MZIKI WA MMASAI ,LOWASA NI NOA SANA

 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jana, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jana, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha, kumsikiliza  Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).
 Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha .
 Mh. Lowassa akiwapungia wananchi.
 Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akihutubia katika mkutano wa hadhawa wa kutangaza nia yake hiyo,  kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha.
Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mkewe Mama Regina Lowassa wakati wa mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Mh. Edward Lowassa akipongezwa na baadhi ya Wabunge waliohudhulia mkutano huo, baada hotuba yake.




























Saturday, May 30, 2015

SIFA TANO ZA LOWASSA KUWA NIA URAIS 2015 ZATAJWA.

Edward Lowassa, ehemaliger Premierminister Tansanias, im Interview mit der DW
DW/ Aboubakar Liongo
Niliwahi kutoa ahadi kuwa nitaweka sababu nzito Tano ambazo mimi binafsi naziona zinafaa sana kumtathmini Edward Lowasa kama Rais ambae Tanzania inamuhitaji kwa muongo mwingine ujao.

Nikiri wazi kwamba kwa CCM ni Lowasa pekee mwenye sifa hizo labda nitamlinganisha na Dr. Slaa ambae kwa muono wangu kidogo anamkaribia Lowassa nikimaanisha kidoogo wanalandana na nitasema wapi Lowassa anampiku Slaa. 


Kwa utangulizi tu ni kuwa Nchi hii ili iendelee inahitaji KIONGOZI kwa ufupi kabisa niseme hivyo inahitaki KIONGOZI SHUPAVU tena SHUPAVU KWELIKWELI sio 

Tupo kwenye umaskini mkubwa,watu wanateseka bila sababu ya msingi. Vijana tunashabikia tuu kama wehu, wengine ni wasomi lakini tunapelekwa kama upepo tukisikia hiki "hewala" tukisikia kile "sawa" tukiambiwa hivi "alhamdulilah" tukiambiwa kile "poa tu". 


Hatutaki kuchambua na kuielewa siasa kwamba kwenye siasa kuna majungu,fitna,kuchongeana,uchu wa madaraka na mali na mambo meeeengi ambapo msipokua makini mnaweza KUMCHUKIA MZURI MKAMPENDA MBAYA. kwa misingi hii ninaanza uchambuzi wangu. Na uchambuzi huu nitauandikakwa facts and figures kama anavyosemaga Prof.Muhongo. 

1.LOWASSA NA "BIG RESULTS NOW".
Nianze na hili.Tunajua wote kuwa serikali yetu sasa ipo kwenye mpango wa matokeo makubwa sasa BRN.Mpango huu mbali na mambo mengine unahitaji kiranja mkuu (RAIS) ambae ni SHUPAVU,JASIRI,MTHUBUTU,MWENYE KUWEKA MALENGO NA KUSIMAMIA KUONA YANATEKELEZEKA lakini pia kama jina la mpango lenyewe lilivyo "MATOKEO MAKUBWA SASA" yaan we want things to happen now. 


Kwa minajili hiyo ni kiongozi gani mnaeona anaeweza kuleta matokeo makubwa sasa?embu tuwe wakweli LOWASSA tunamjua alipoingia kuwa waziri mkuu alitangaza kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ambacho angekuwa WAZIRI MKUU angetaka kata zote ziwe na shule za sekondari. Sote ni mashahidi alivyosimamia sera hiyo shule zilianza kumea kama uyoga yaani kama mazingaombwe.


Hata maeneo kama ya Kinondoni ambapo ardhi huuzwa kiholela hivyo ardhi kutopatikana lakini ilipatikana kuanzia vijijini hata miji wananchi walianza kujenga shule.ni mashahidi kama sio fitna za yeye kupelekea kujiuzulu sijui leo kielimu tungekuwa wapi. 

HE HAD A MASTER PLAN OF OUR EDUCATION SYSTEM AND HE LEFT WITH IT BUT STILL HE HAS IT IN HIS HEAD.  
Naamini huyu mzee akipata nafasi tutafika. Si hilo tu tunajua mambo mengi aliyokuwa nayo kichwani ambayo mengi yapo kwenye huu mpango ni shupavu ambae angeweza na anaweza kuyasimamia yatekelezeke. Dr.Slaa ni mzuri wa kusimamia mabo lakini somtimes huwa analoose focus nitaliongelea kwenye point ya tatu. 


2.LOWASSA ANAJUA KUWEKA VIPAUMBELE NA KUJUA TUNAVIFIKIAJE.

Jamani Nchi hii ili iendelee na ndivyo hata nchi zilizoendelea zilivyoanza ni kuwekeza katika elimu ya watu wake, Kilimo na Viwanda nikimaanisha sekta ya uzalishaji. Tunajua jinsi LOWASSA alivyo anza na hayo shule za kata nilishazizungumzia na mipango mingi ya elimu ukitaka kuijua waulize walimu alipoanzisha program ya kuwajengea nyumba,alivyoanzisha program ya kuhakikisha watoto hawakai chini kila mtoto akae kwenye dawati,alivyoshusha ada n.k Tusisahau kwenye kilimo aliyoanzissha kilimo cha umwagiliaji mpaka akataka kuleta Mvua ya kutengenezawa mimi huwa nasema hata kama isingewezekana lakini inaonyesha ile nia njema aliyonayo mzee huyu. 


Ukitaka kuelewa vizuri waulize wakulima wakuhadithie jinsi alivyokua anawatimua kazi na kuwashtaki watu waliokua wanakula hela za mbolea za ruzuku. Jinsi alivyokua anatafuta masoko ya nje ya mazao ya kilimo waulize wafanyabiashara wakuhadithie. 


Ni kiongozi nani mwenye hulka na kariba hii ndani ya CCM? Tunajua wote kuwa mapinduzi ya kilimo na viwanda ndiyo yaliendeleza bara la ulaya historia inatuambia hivyo na elimu ndiyo imeikomboa JAPAN na nchi nyingine LOWASSA ni jenmbe katika hili ana master plan ya mambo haya na anajua kusimamia haya sio siri wala kumpigia debe HE IS REAL. 


3.LOWASSA SIO MTU WA KUPOTEZA UELEKEO (TO LOOSE FOCUS) 
Lowassa siku zote akitaka kitu ni mpaka kitimie na kikishindikana basi ujue kumpata wa kukiweza ni shughuli pevu na akitaka kitu hakati tamaa idimradi kiwe ni chema hata kama hakina maslahi kwake na ikitokea yeyote akasimama mbele yake kumzuia basi ama zake ama za huyo mtu. wazungu wanasema "You are either with me or against me".


Tunakumbuka jinzi alivyokua akitimua viongozi waliokuwa wakitaka kumkwamisha kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Hakujali urafiki wala nini anakuweka ukimzingua anakumwaga THAT IS THE TYPE OF THE PRESIDENT WE WANT kwa sifa hii hana tofauti na Dr. Slaa japo Slaa huwa wakati mwingine anapoteza uelekeo.

Mfano mzuri wa kutopoteza uelekeo ni kwamba mwaka 1995 alitaka kuwa Rais wakatoswa,2005 akakubali swahiba wake achukue lakini akabaki kuwa focused, fitna zikajengwa akajiuzulu 2007 lakini hata sasa bado hajaloose focus japo anaface a lot of challenges. 


Sio mfano mzuri sana huo kutoa lakini inaonyesha ni mtu wa namna gani kuwa siku akitaka vijana tukimaliza vyuo tupate kazi maana yake atalisimamia hilo by hooks or crooks kama ni viwanda kufufuliwa vitafufuliwa idimradi tu vijana tulambe ajira THAT IS THE PRESIDENT WE WANT. 


A FOCUSED MAN 4.LOWASSA NI HALF DICTATOR HALF DIPLOMATIC Hahahahaha nianze kwa kucheka maana tunajua hakuna nchi iliyoendelea kwa kiongozi kuwa full diplomatic yaani kitu kidogo "Tume iundwe" jambo dogo "NJOO MEZANI TUONGEE" kitu kidogo "TUSUBIRI UCHUNGUZI" jambo kidogo "DUNIA ITATUELEWAJE". jamani tunamjua LOwassa ni mtu wa action kwa kwenda mbele Ghorofa limeanguka nani mkandarasi piga chini. Halmashauri imekula hela za maendeleo nani mkurugenzi piga chini.


Wizara inatokota nani muhusika piga chini. Tunatatizo fulani solution ni nn tekeleza.yaani hakuna longolongo.Hii ndio type ya uongozi itakayotukomboa Tanzania. 


Na ukitaka kujua faida yake waulize wachina yaani watakwambia vizuri udictator kidogo unavyoharakisha maendeleo yao. Hakuna TANZANIA hii viongozi wa type hii mbali na LOWASSA na Dr. SLAA tatizo SLAA ....(nitamuongelea wakati mwingine) 

5.LOWASSA ANASIKILIZIKA,ANAFUATILIA,SI KIGEUGEU NA SI MVIVU.
Hii ni sifa kubwa kwa mtu kuwa RAIS unapoona unataka kuwa Rais au unamchagua mtu ambae kwa haiba yake tu hasikiliziki ujue unaturudisha nyuma. 

Rais anatakiwa awe akisema hili lifanyike huyo anaeambiwa linamuingia moyoni. Nirudie Rais anatakiwa anapoongea hata kwa simu tu ile pitch ya sauti iashirie kuwa jambo hili ni lazima lifanyike.Yaani kama anaongea mbele yako ukimwangalia kuanzia nywele mpaka unyayo uashirie kuwa kiongozi anataka hili lifanyike.

LOWASSA yupo hivyo akisema jambo linatekelezwa na haiishi hapo anafatilia mwanzo mwisho si mvivu hata kidogo.kutwa anaizunguka Tanzania hii vijijini hadi mijini nyote ni mashahidi wa hili.