Wednesday, July 26, 2017

MAKAMU WA RAIS MH SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA SCAUT MJINI DODOMA NA KUWAVISHA NISHANI VIONGOZI WASTAAFU

 Mama FATMA KARUME akivishwa nishani ya heshima kwa niaba ya hayati ABEID  AMAN KARUBE.
 Rais mstaafu wa tanzania wa awamu ya nne MH JAKAYA KIKWETE akivishwa nishani ya heshima na makamu wa rais MH SAMIA SULUHU.
 Rais mstaafu wa zanzibar akivishwa nishani.
 Rais mstaaf wa awamu ya pili MH ALLY HASSAN MWINYI akivishwa nishani ya heshima na makamu wa rais MH SAMIA SULUHU.
 Makamu wa rais MH SAMIA SULUHU akimvisha nishani ya heshima waziri mkuu staafu MH SALIMU AHMED SALIMU katika maadhimisho ya miaka 100 ya SCAUT TANZANIA.
Makamu wa rais mh SAMIA SULUHU HASAN akiongea katika maadhimisho ya miaka 100 ya SCAUT mjini dodoma.

WALIOFUKUZWA UANACHAMA NA CUF WAPOTEZA NA UBUNGE WAO.



Thursday, July 20, 2017

RAIS WA BURUNDI MH:PIERRE NKURUNZINZA AFANYA ZIARA YA SIKU MOJA TANZANIA.

Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 Julai 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Rais wa Burundi kuwahutubia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwapungia wananchi alipowasili katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwa wamesimama wakipokea salamu za heshima kutoka kwa majeshi ya ulinzi na usalama.
Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akikagua graride la lililoandaliwa na jeshi la ulinzi la Tanzania JWTZ katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Kumpokea katika Uwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye uwanja wa Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta Jambo na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza Mara baada ya kumpokea katika Mji wa Ngara kwenye uwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza kwa maongezi mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na ujumbe wake katika mazungumzo maalum ya kiserikali na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza na ujumbe wake Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza pamoja na mama Janeth Magufuli katika Maongezi.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwapungia mikono wananchimwa mji wa ngara wakati wakiwasili katika uwanja wa posta mjini Ngara kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwapungia mikono wananchi wa mji wa Ngara waliohudhulia katika uwanja wa posta mjini Ngara kwa ajili ya Mkutano wa hadhara.
Umati wa ananchi wa mji wa Ngara waliohudhulia katika uwanja wa posta mjini Ngara kusikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa posta mjini Ngara 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza katika uwanja wa Lemela Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017 baada ya kumaliza ziara yake Rasmi ya kiserikali Nchini. PICHA NA IKULU.

MKUU WA MKOA WA DODOMA MH JORDAN RUGIMBANA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA (TIC)ILI KUJENGA KITUO CHA UTOAJI HUDUMA MKOANI HAPO.



Wednesday, July 19, 2017

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM .

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionyesha kitabu chenye ripoti  ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM) mara baada ya kuzindua taarifa hiyo kwenye Kituo cha Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amezindua Taarifa ya Nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM).Uzinduzi huo  ulihudhuriwa na  kiongozi wa Jopo la Mchakato huo kwa Tanzania ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo  la Watu Mashuhuri Bi. Brigitte Sylvia Mabandla, Viongozi wengine wa APRM Tanzania ni Balozi Ombeni Sefue, Profesa Hasa Mlawa na Balozi Aziz Mlima aliyemuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

APRM ni mpango wa hiari wa kujipima kwa vigezo vya utawala bora uliobuniwa mwaka 2003 na Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Lengo la mpango huu ni kuziwezesha nchi  wanachama kujitathmini kwa vigezo vya utawala bora katika maeneo manne ambayo ni; Demokrasia na Utawala wa Kisiasa; Usimamizi wa Uchumi; Utendaji wa Mashirika ya Biashara; na Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.

Akihutubia katika uzinduzi huo, Makamu Rais amewapongeza Wakuu wa Nchi na Serikali wanaoshiriki katika mchakato wa APRM kwa ujasiri wao wa kushirikishana taarifa za kuaminika kuhusu masuala ya utawala bora katika nchi zao. “Taarifa hizi zinaonesha wazi juu ya hali ya utawala bora katika Bara letu na kutupa nafasi ya kujirekebisha pale ambapo kuna dosari na kujipongeza pale tunapofanya vizuri na kuwapa wengine nafasi ya kujifunza zaidi’’ alisema Makamu wa Rais.

Aidha alisisitiza kuwa kupitia utaratibu huu tumeweza kuuonesha ulimwengu nguvu zetu za pamoja kama Bara la Afrika katika kuboresha demokrasia, amani na utulivu, utawala wa sheria na utawala bora kwa ujumla.

Kwa upande wa Tanzania, Makamu wa Rais alisema mchakato huu unatuonesha na kutukumbusha falsafa na maono ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere (Tujisahihishe, 1962) na Mwongozo wa TANU wa mwaka 1971.  Alisema nchi yetu imefanya mambo mengi katika kutekeleza mpango huo ikiwemo kuimarisha taasisi zinazoshughulikia masuala ya utawala bora ikiwemo Tume ya Haki za binadamu na Utawala Bora, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa na sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma.

Kuhusu changamoto zilizobainishwa kwenye taarifa husika, Makamu wa Rais alisema kwa kiasi kikubwa zimepatiwa ufumbuzi katika Mkakati wetu wa Maendeleo 2025 unaolenga kukuza na kupanua wigo wetu wa uchumi ili kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.  Kuhusu suala la Muungano alisema muundo wa Muungano wetu ni wa serikali mbili ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Makamu wa Rais alisema miongoni mwa maeneo ya vipaumbele katika mchakato wa kuelekea kuwa nchi ya viwanda  ni kuimarisha sekta ya nishati na umeme. “Kwa ujumla tumefanya jitihada kubwa katika huduma ya nishati kutokana  na ugunduzi mkubwa wa gesi asilia hapa nchini” alisisitiza Makamu wa Rais. Kwa sasa umeme unasambazwa kwa kasi katika vijiji vyetu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Serikali imefanya jitihada kubwa katika kuzipatia ufumbuzi changamo za kijamii kama vile elimu, afya na maji ambazo zilitajwa kama vikwazo katika taarifa husika. Aidha, Serikali imeongeza uandikishaji wa wanafunzi kwa shule za msingi na sekondari, imeboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, imejenga madarasa na maabara, imeboresha maslahi ya walimu na kuhakikisha inajenga vyuo vya ufundi katika kila wilaya.

Pia Makamu wa Rais alisema Tanzania inatambua kuwa mchakato huu wa APRM ni endelevu hivyo serikali itaendelea na jitihada zake kuhakikisha kwamba changamoto zote zilizobainishwa ndani ya taarifa zinapatiwa majawabu kupitia serikali na taasisi zake, asasi binafsi na wananchi kwa ujumla.

Mwisho, alishukuru na kutambua mchango wa washirika wa maendeleo katika kufadhili kazi za APRM na kuwaalika kuendelea kuchangia shughuli za APRMTanzania ikiwemo mpango kazi wa Taifa.

Tuesday, July 18, 2017

IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO JESHI LA POLISI.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro

Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ndani ya jeshi hilo.
Katika mabadiliko hayo, Kamanda Sirro amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda kuwa Mkuu wa Kitengo cha Mafao na Fidia Makao Makuu ya Polisi.
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Julai 18 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnaba Mwakalukwa, imeeleza kuwa nafasi ya Kaganda imechukuliwa na Kamishna Murilo Jumanne.
Kabla ya hapo, Kamanda Jumanne alikuwa Kamanda wa Polisi, mkoa wa Shinyanga.
“Nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Jumanne, Shinyanga, imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Simon Sylverius ambaye alikuwa Ofisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Mara,” amesema.
Taarifa hiyo imesema, mabadiliko hayo ni ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi ili kuongeza ufanisi na utendaji wa kazi.

MAKAMU WA RAIS MH SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA MAMIA KUMUAGA LINAH MWAKYEMBE JIJINI DAR ES SALAAM.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hasan amewaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo marehemu Linah George Mwakyembe katika usharika wa kanisa la KKKT- Kunduchi DSM.
Pamoja na Makamu wa Rais, pia ibada hiyo imehudhuriwa na marais wastaafu mzee, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete pamoja na Mawaziri,  Katibu Mkuu kiongozi, makatibu wakuu na wawakilishi kutoka ofisi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania.
Akizungumza mmoja ya watoto wa Waziri Mwakyembe ambaye amesoma wosia wa marehemu mama yake, Bi Linah amesema mama yake alikuwa ana ngozi ngumu kuliko hata mzee wake na alikuwa akimfariji na kumpa moyo endapo zinapotokea changamoto katika kazi yake.
Waziri wa Habari Dkt Harrison Mwakyembe akilia kwa uchungu juu ya Jeneza la mkewe wake Linah Mwakyembe wakati wa kutoa heshima za mwisho leo.
Marehemu Linah Mwakyembe mzaliwa wa Machame Wari huko Kilmanjaro mwaka 1970 na alifariki dunia tarehe Julai 15 mwaka huu saa tano usiku katika hospitali ya AGA KHAN alipokuwa anauguzwa maradhi ya saratani ya matiti ambayo imemsumbua kwa miaka miwili na ameacha mume na watoto watatu wa kiume. 
Prof Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini akitoa heshima zake za mwisho

Sunday, July 16, 2017

RC Dodoma, Jordan Rugimbana ametoa siku 10 kwa vituo vya mafuta mkoani humo kuanza kutumia mashine za kielektroniki EFD kabla havijafungiwa


 

PICHA MBALIMBALI ZA MH RAIS MAGUFULI AKIWA KANISANI CHATO KATIKA IBADA YA JUMAPILI.

1 (1)
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli pamoja na mke wake MamaJaneth Magufuli wakitoa sadaka wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita.Leo 16 julai 2017
1 (2)
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakisikiliza mahubiri toka kwa Padri  Henry Mulinganisa  wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita.Leo 16 julai 2017
1 (3) 1 (4)
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisisitiza jambo wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita.Leo 16 julai 2017
1 (5)
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliyeshika kikapu cha sadaka akipokea sadaka toka kwa Mke wake Bi Janeth Magufuli wakati wa kuchangia ujenzi na upanuzi wa katika kanisa la Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita.Leo 16 julai 2017
1 (6)
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliyeshika kikapu cha sadaka akipokea sadaka toka kwa waumini mbalimbali  waliohudhuria ibada katika kanisa la Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita Leo 16 julai 2017
1 (7)
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa ameshika kikapu chenye michango ya fedha zilizotolewa na waumini wa kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita kwaajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa hiloLeo 16 julai 2017
1 (9)
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru mmoja wa waumini wa kanisa hilo ndugu Mwita Chacha mara baada ya kuchangia mifuko mitano ya saruji kwaaajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita .
1 (10)
Mama Janeth Magufuli mke wa Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiahidi mchango wake wa ujenzi na upanuzi wa kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita .
1 (14)
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akishuhudia  mmoja wa waumini wa kanisa hilo ndugu Deogratius Ambrosi mwenye ulemavu wa mkono,akitoa mchango wake wa kiasi cha shilingi elfu tano kwaajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita
1 (15)
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru  mmoja wa waumini wa kanisa hilo ndugu Deogratius Ambrosi mwenye ulemavu wa mkono,akitoa mchango wake wa kiasi cha shilingi elfu tano kwaajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita
1 (17)
1 (21)
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiondoka kwenye kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita, mara baada ya ibada.
1 (22)
Waumini wa kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita wakimpungia mikono Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli wakati akiondoka kanisani hapo.
1 (23) 1 (24)
Katibu wa Rais Ndugu Ngusa Samike akikabidhi mchango wa Mhe Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli jumla ya shilingi milioni kumi kwaajili ya ujenzi na upanuzi wa  kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita,
1 (26)
Waumini wa kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita wakiwa kwenye ibada
1 (29)
Waumini wa kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita wakitoka kwenye ibada ya jumapili. (PICHA NA IKULU)