Monday, July 3, 2017

MAJALIWA: CHANGAMOTO YA USAFIRI VIJIJINI KUWA HISTORIA

kuf1
,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akizindua  kitabu cha Muongozo  wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini ,katikati  ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI .Simba  Chawene  ,kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Wakala Barabara Vijini na Mijini Mhandisi  Victor Seif .Uzinduzi huo umefanyika leo July 2, 2017 katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma
kuf2
,Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa. kulia   akimkabidhi kitabu cha Muongozo wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini  , Mkurugenzi Mtendaji wa  Wakala Barabara Vijini na Mijini Mhandisi  Victor Seif, katikati  ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI .Simba  Chawene  . Uzinduzi huo umefanyika leo July 2, 2017 katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma
kuf3kuf4
Waziri  Mkuu  Kassim  Majaliwa  akihutubia Viongozi wa Mikoa yote Nchini walio hudhuria  Uzinduzi  wa Wakala  wa Barabara Vijini na Mijini leo july 2,2017, katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma.
kuf5kuf6
Wakuu wa Mikoa na viongozi mbalimbali wakishuhudia   Uzinduzi wa Wawakala wa Barabara Vijijni na Mijini
 Picha na ofisi ya Waziri Mkuu
…………………………………………………………….
               *Azindua Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini 
                *Asema utashusha bei ya vyakula mijini
 CHANGAMOTO ya usafiri nchini, hususan maeneo ya vijijini kuwa historia baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).
 Amesema wakala huo utasaidia kuimarisha mtandao wa barabara za vijijini na kuwawezesha wananchi wengi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi, hivyo kukuza uchumi.
 Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili,  Julai 02, 2017) wakati akizindua wakala huo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma.
 “Wakala huu tunaouzindua leo utakuwa na manufaa makubwa kwa ustawi wa nchi yetu kwa kuongeza chachu ya uzalishaji mali mashambani kutokana na urahisi wa kufika sokoni,”
 “Utashusha bei ya vyakula mijini na bidhaa za viwandani vijijini kutokana na gharama za usafirishaji wa mazao kutoka mashambani na bidhaa za viwandani kutoka mijini kupungua,”
 Aidha, Waziri Mkuu amesema manufaa mengine ya wakala huo ni kuboresha na kubadili hali za kimaisha na kiuchumi kwa wananchi kwani watakuwa wanasafiri kwa muda mfupi.
 Pia utawezesha maeneo mengi ya nchi kufikika kwa urahisi, hivyo kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa wakati.
 Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika ujenzi, ukarabati na utengenezaji wa miundombinu ya barabara ikiwemo ya rushwa katika utoaji wa zabuni.
 Amesema jambo hilo halikubaliki hivyo, amewataka watendaji wa TARURA wahakikishe wanatokomeza vitendo vya rushwa vilivyokithiri kwenye utoaji wa zabuni, zitolewe kwa watu wenye uwezo wa kufanyakazi.
 Waziri Mkuu amesema changamoto nyingine ni usimamizi hafifu wa mikataba ya ujenzi, ambapo ameelekeza isimamiwe vizuri na iwe ya wazi na yenye kutekelezeka.
 Akizungumzia vitendo vya baadhi ya viongozi wa Halmashauri kubadilisha matumizi fedha za barabara, ameagiza fedha zote zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya barabara zitumike kama ilivyopangwa.
 Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mheshimiwa George Simbachawene alisema TARURA ni muhimu kwa kuwa zinagusa wananchi moja kwa moja na ni kichocheo kikubwa cha uchumi wa wananchi, hivyo kuinua uchumi wa  Taifa wenye msingi imara.
 “Barabara hizi zinachochea kilimo katika ngazi ya jamii, zinaboresha ufikaji kwenye huduma za kijamii kama afya, elimu, maji na masoko, hivyo kuliwezesha Taifa kuwa na jamii imara kiafya, kiakili na kiuchumi,”.
 Kutokana na umuhimu wa mtandao wa barabara za Vijijini na Mijini, Mheshimiwa Simbachawene ameomba mgawanyo wa mapato ya Mfuko wa Barabara wa asilimia 70 kwa TANROADS  na asilimia 30 kwa Halmashauri uangaliwe upya, ambapo Waziri Mkuu ameridhia.
 Waziri Mkuu alisema “Naamini kwa kuanzishwa TARURA sasa hoja hii inajadilika, tumieni taratibu zilizopo ili maamuzi yaweze kufanyika,”.
Mtandao wa barabara za Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni kilomita 108,942.2 ambao ni Zaidi ya nusu ya barabara za Kitaifa.

1 comment:

  1. titanium price per ounce - TIPS TIPS TIPS
    All titanium white octane Tinti gold Tinti is crafted in chi titanium flat iron titanium metal, it has a heat 출장마사지 index of citizen titanium dive watch 2500 to 5000 and is a true platinum-quality gold trekz titanium pairing alloy.

    ReplyDelete