Saturday, May 31, 2014

WAFANYA BIASHARA WANAOFANYA BIASHARA KANDOKANDO YA BARABARA WANASABABISHA AJALI

Na John Banda, Dodoma
IMEELEZWA kuwa kitendo cha wafanyabiashara ndogondogo [wamachinga]
kuzagaa sehemu za watembea kwa miguu katika maeneo ya stendi ni hatari
inayoweza kuwasababishia ajali wakati wowote.
Kauri hiyo ilitolewa na Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Dodoma SSP
Peter Sima kwenye baraza la madiwani lilifanyika jana.
Sima alisema machinga hao ambao huuza bidhaa mbalimbali zikiwemo za
masokoni katika sehemu hizo za watembea kwa miguu wakati wowote
wanaweza kusababisha ajali kutokana na watembea kwa miguu kushindwa
kupita na badala yake huwalazimu kupita kwenye barabara.
Alivitaja vituo hivyo kuwa ni kile cha Daladala jamatini, stendi ya
mkoa [oil com] naya magali ya vijijini ya Mshikamano ambako wamachinga
hao huzagaa bila hata kujali usalama wao.
Aidha aliwataka manispaa kuhakikisha wanawaelekeza machinga hao
pakufanyia biashara zao lakini badala ya kuwaacha katika maeneo hayo
ambayo ni hatari kwa maisha yao.
‘’Mhe. Meya hakikisheni wamachinga hao wanaondoka katika maeneo hayo
kwa ajili ya usalama wao na kuuwema mji safi wenye muonekano wa kuwa
jiji la sivyo tutawaondoa kwa nguvu kutokana na sheria
zinavyotuelekeza’’, alisema Sima
Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu kati ya machinga hao ambao wengi wao
hukimbia masokoni wakijazana kwenye vituo hivyo bila utaratibu na
watendaji wa manispaa ambao wanaonekana kuwashindwa maana wamekuwa
wakiachwa kuzagaa hovyo huko wakichafua madhingira katika maeneo hayo
bila kuchukuliwa hatua yoyote.


Madiwani wa Manispaa wa Dodoma wakiwa katika ukumbi wa manispaa
wakifuatilia jambo wakatiwalipokuwa kwenye baraza la kawaida la
kujadili makusanyo ya mwaka wa fedha kwa kiasi walichofikisha mpaka
hivi sasa ambapo zimebaki siku chache ili kuyawakilisha serekali kuu.

Meya wa Manispaa ya Dodoma Emanuel Mwiliko akifafanua jambo kwenye
baraza la madiwani lililokutana mwisho wa wiki kujadili juu ya
makusanyo mbalimbali ili kukamili makadilio ya mwaka huu wa fedha,
kushoto ni Naibu Meya Jumanne Ngede.

Kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma SSP Peter Sima
akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na madiwani wa manipaa ya
Dodoma lililofanya mwishoni mwa wiki hii.

Monday, May 26, 2014

UKATILI GEITA: BABA AMPAKA MWANAE PILIPILI MACHONI NA KUMPIGA HADI KUFA.

JESHI la Polisi mkoani Geita, linamshikilia William Kibyala (40), mkazi wa Kijiji cha Misiri, Kata ya Bugarama, Wilayani Geita kwa kosa la kumpaka pilipili machoni mwanae John Wiliam (4), na kumchapa viboka sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kufa.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Joseph Konyo, amethibitisha Jeshi hilo kumshikilia mtuhumiwa huyo muda mfupi baada ya tukio hilo lililotokea Mei 23, 2014 ambapo amesema mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
“Mtoto huyu alifariki baada ya kupewa adhabu na Baba yake mzazi kwa kupigwa na kupakwa pilipili, huyu mtuhumiwa tunamshikilia hadi sasa na uchunguzi zaidi wa tukio hili bado unaendelea kwahiyo kwa taarifa nyingine tutawaambia ili muujulishe Umma wa watanzania kupitia kwenu na vyombo vingine vya habari”.
Aidha, alisema Baba wa mtoto huyo anadaiwa kufanya ukatili huo baada ya kumtuhumu mtoto huyo kukataa kumfungulia mlango wakati alipotoka matembezini usiku wa manane.
Baadhi ya wananchi wanaoishi katika Kijiji hicho wamesema kuwa mtoto huyo alifariki baada ya kuchapwa fimbo mwili mzima, kupigwa ngumi na mateke, kisha kupewa adhabu ya kukimbia riadha ya kuzunguka nyumba yao usiku wa manane kabla ya kifo chake.
Mmoja wa mashuhuda hao, Irine Kaijage, amesema baada ya mtoto huyo kumaliza adhabu hiyo alipakwa pilipili machoni na makalioni hali iliyosababisha mtoto huyo kuzidiwa na kupoteza maisha Mei 24, 2014 jioni.
Mmoja wa watoto wa Mzazi huyo, Shija William, alisema mdogo wao alikuwa akipewa adhabu hiyo mara kwa mara na Baba yao kwa madai kwamba Mama yao alimbambikizia mdogo wao kwani yeye hakumzaa.
Watoto 863 nchini walifanyiwa vitendo vya kikatili mwaka 2014, ikiwemo kulawitiwa na walezi wao ambpo katika kipindi hicho watu 1,669 waliuawa na wananchi kwa kujichukulia sheria mkononi

Sunday, May 25, 2014

HUU NDIO UKWELI WA BWANA HARUSI KUINGIA MITINI NA KUSABABISHA KUOTA MBAWA NDOA YA MH MBUNGE VICKY KAMATA

Mbunge wa Viti maalumu CCM, Vicky Kamata, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Tabata General, jijini Dar es Salaam baada ya juzi kupatwa na ugonjwa ghafla wakati akijiandaa kuelekea Kanisani kwa ajili ya kufunga ndoa. Picha na Florence Majani 
HABARI zilizizoufikia mtandao huu zinasema kuwa Kilichotokea na kusababisha Bibi Harusi mtarajiwa Vick Kamata, kuanguka  na kuugua ghafla ni mshituko baada ya Bwana harusi kughaili ghafla kuendelea na wazo lake la kufunga ndoa.
Mtonyaji wa habari hizi ametonya kuwa ikiwa imebaki siku moja tu kufungwa ndoa hiyo, wapambe waliibuka na kumtafuta Bwana harusi na 'kumuuma sikio' yaani kumpa umbea ambao haukuweza kufahamika mapema kuwa ulikuwa ni wa aina gani huku ikidaiwa kuwa Bwana harusi alibadilika ghafla baada ya kukutana na watu hao na kuanza kuonyesha msimamo wake.
Wakati akiendelea na msimamo wake huo, ndipo ikamfikia Bi harusi na kushindwa kufikia muafaka huku Bwana harusi akiombwa kutoendelea na msimamo wake lakini hakuweza kubadili maamuzi, na ndiyo sababo hasa ya Bi harusi huyo kupatwa na mshituko.
Harusi hiyo iliyokuwa ifungwe jana Jumamosi, ilikuwa ni moja kati ya harusi zilizokuwa gumzo kubwa na ikitumia gharama kubwa zaidi jijini dar na hata nchini kote kuwahi kufungwa.
Cha kujiuliza ni kwamba hao wapambe hawakuweza kufanya umbea wao hadi ikiwa zimebaki dakika za majeruhi, na hata kama ni kweli hayo waliyomueleza Bwana harusi kama yalitokea huoni kama yalikuwa ni mchongo laamumu ulioandaliwa maalum???
Pamoja na haya yote lakini bado ukweli atabaki kuwa nao Bibi harusi na Bwana harusi kwa kile alichoelezwa na wapambe hao.