Sunday, June 30, 2013

Mtu Mmoja aliyekuwa akitumia zaidi ya majina manne tofauti ya Paulo, Yakobo, Mohamed na Hassan Joti amekutwa amejinyonga na mwili wake umekutwa ukinin’ginia kwenye paa la nyumba aliyokuwa akiishi iliyopo katika kitongoji cha Njedengwa, kata ya Dodoma makulu baada ya kudaiwa kujinyonga.

Balozi katika mtaa wa njedengwa Sikitu Mrisho akiwafafanulia jambo waandishi wa habari baada ya marehemu mwenye majina zaidi ya manne ya Paulo,Yakobo, Hassan na Joti kukutwa amekufa kwa kujinyonga kwenye nyumba aliyokuwa akiishi njedengwa manispaa ya Dodoma

Hamida Hassan 25 Mke wa Marehemu akiwa amejiinamia kwa huzuni kutokana na Mwanaume aliyekuwa ametengana naye kufa kwa kujinyonga kutokana na wivu wa kimapenzi uliosababishwa na kuishi nyumba zao zikiwa zinatazamana mtaa wa njedengwa Manispaa ya Dodoma.

PICHA  NA JOHN BANDA





Thursday, June 27, 2013

SERIKALI YAKIRI KAZI YA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA BADO NI NGUMU.




Kamishina wa Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za kulevya Christofa Shekiondo akifafanua jambo wakati wa kilele cha maadhimisho ya ya kitaifa ya siku ya kupiga vita Dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika Dodoma.







Wananchi mwa mkoa wa Dodoma wakiandamana kuelekea Viwanja vya nyerere [Nyerere Squere] kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita vita Dawa za kulevya yaliyifanyika jana


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu [Sera, Uratibu na Bunge] William Lukuvi akipewa maelekezo ya Aina ya Madawa ya kulevya na Mkemia mkuu wa Serikali Profesa Samweli Manyere alipotembelea Maonyesho hayo baada ya kuyafunga Dodoma jana.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu [Sera, Uratibu na Bunge] William Lukuvi, Mkemia mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyere, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma DR. Rehema Nchimbi na viongozi wengine wakipokea maandano kabla ya kufunga kuhitimisha maaadhimisho ya siku ya madawa ya kulevya.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu [Sera , Uratibu na Bunge] Willam Lukuvi akielezea jambo wakati alipokuwa akufunga maadhimisho ya kilele cha kupiga vita madawa ya kulevya yaliyofanyika Dodoma jana.


Nuru Saleh Mkazi wa Vijibweni Da es laam akitoa ushuhuda wa jinsi madawa ya kulevya yalivyomtesa kabla ya kuyaacha


Robert Mbeno Mnemele akitoa shuhuda jinsi alivyoanza kutumia madawa ya kulevya tangu akiwa Darasa la tano na baada ya kuacha ameanza kidato cha kwanza, wakati wa maaadhimisho hayo