Sunday, June 30, 2013

Mtu Mmoja aliyekuwa akitumia zaidi ya majina manne tofauti ya Paulo, Yakobo, Mohamed na Hassan Joti amekutwa amejinyonga na mwili wake umekutwa ukinin’ginia kwenye paa la nyumba aliyokuwa akiishi iliyopo katika kitongoji cha Njedengwa, kata ya Dodoma makulu baada ya kudaiwa kujinyonga.

Balozi katika mtaa wa njedengwa Sikitu Mrisho akiwafafanulia jambo waandishi wa habari baada ya marehemu mwenye majina zaidi ya manne ya Paulo,Yakobo, Hassan na Joti kukutwa amekufa kwa kujinyonga kwenye nyumba aliyokuwa akiishi njedengwa manispaa ya Dodoma

Hamida Hassan 25 Mke wa Marehemu akiwa amejiinamia kwa huzuni kutokana na Mwanaume aliyekuwa ametengana naye kufa kwa kujinyonga kutokana na wivu wa kimapenzi uliosababishwa na kuishi nyumba zao zikiwa zinatazamana mtaa wa njedengwa Manispaa ya Dodoma.

PICHA  NA JOHN BANDA





No comments:

Post a Comment