Tuesday, June 4, 2013

MWILI WA ALBERT MANGWEA KUWASILI DAR LEO SAA NANE MCHANA.

Watanzani wa nchini Afrika ya Kusini wakibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Albert Mangwea, kuelekea Uwanja wa Ndege tayari kuanza harakati za kuusafirisha kurejea nchini tanzania, ambapo mwili huo wa msanii wa kizazi kipya aliyefariki Dunia huko nchini Afrika ya Kusini hivi karibuni, unatarajia kuwasili nchini kesho majira ya saa nane mchana na Ndege ya South Africa Air Ways, baada ya kukamilika kwa taratibu za Kisheria za nchini humo na kumaliza taratibu za Watanzania waishio nchini humo, kuaga mwili huo leo.  
Mwamvita Makamba, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu Albert Mangwea.



Baadhi ya watanzania waishio Afrika Kusini wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa  marehemu Albert Mangwea, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo, ambapo ilikuwa ni maalum kwa watanzania waishio nchini Afrika ya Kusini.

No comments:

Post a Comment