Thursday, June 6, 2013

KAMANDA MISIIME AZIDI KUKAMATA WAHALIFU DODOMA.

Na John Banda, Dodoma

WATU watatu wanashikiliwa na polisi mkoani Dodoma kwa makosa ya utapeli kwa njia tofauti ikiwemo ya kutumia Dolla Bandia
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa hapa Suzan Kaganda alisema jeshi hilo liliweka mtego na kufanikiwa kumkamata Abuu Mohmed Omary maarufu kwa jina la Rass Mfanya biashara soko la Sabasaba maeneo ya Nyerere Squere.
Kaganda alisema Rass alikamatwa akijaribu kumrubuni Agostino Mpanda alipokuwa akitaka kumtapeli 7, 500,000 kwa kutumia Dolla Bandia, Dolla nyeusi [Black Dolla] ambapo huwaambia watapeliwa watoe fedha ili kununulia Dawa ya kuzioshea.
Kaimu Kamanda huyo aliongeza kuwa baada ya kumkamata na kumpekua mtuhumiwa huyo nyumbani kwake walimkuta akiwa na Shl 2,600,000 ambazo alishindwa kueleza namna alivyozipata.
Wakati huohuo Jeshi hilo limewakamata Fransisika Gerard Mchaga mkazi wa Area E 27 na Ibahimu Mkwawa Mhehe 40 mkazi wa ipagala wakiwa kwenye Gari aina ya NOAH yenye namba za usajili T 311 BLM likitokea Morogoro kuja Dodoma.
Watu hao waliokamatiwa Wilaya ya Chamwino walikutwa na Chupa kubwa ya Chuma yenye uzito wa kilo 15 ikiwa na lebo ya Red Mercury Industry na Nembo ya UN iliyokuwa imejazwa Goroli ndogondogo za Baiskel  wanazodaiwa kutumia kwa Utapeli wakidai ni madini.
Jeshi hilo limewapongeza wananchi wanaolisaidia kufichua waharifu na kuwataka kuendele ili hatimae waweze kupunguza kama siyo kuondoa kabisa tatizo hilo la watu kujipatia Fedha kwa njia zisizo za halali, huku jeshi hilo likiwataka wanaojihusisha na Utapeli wa namna yoyote kuacha tabia hiyo kwani Sheria haitawafumbia macho.
MWISHO.

No comments:

Post a Comment