Tuesday, March 17, 2015

KUTANA NA MTOTO HUYU WA AJABU,ANA MIAKA MITATU LAKINI ANAUWEZO WA KUKOKOTOA HESABU ZA SEKONDARI NA KONGEA KIINGEREZA FASAHA

 
Huyu mtoto ana miaka 3 anaitwa Nice, kwao ni Kiteto kijijini huko Manyara. Lakini cha ajabu ana uwezo wa kufanya hesabu za Sekondari na nyingine ngumu kwa uwezo wa kutisha na kuongea kiingereza fasaha kabisa bila kigugumizi. Ukimuongelesha kiswahi li anakwambia 'Please speak english'. Cha kushangaza zaidi ni kwamba tangu azaliwe hajawahi kwenda shule au kuhudhuria darasa la aina yoyote.
  
Na kama ujuavyo mazingira ya kijiji watu huzungumza lugha ya eneo husika lakini yeye ameweza kuongea kingereza bila kujua wapi amejifunza. na unaambiwa wakati mwingine huwafundisha wanafunzi wa form 1.
 
 

MWANAFUNZI ATEKWA ABAKWA NA KUUAWA.

DUNIA imekwisha jamani! Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Mabibo, Dar es salaam, Irene Said (15) ametekwa, amebakwa na kuuawa kikatili kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili huku ikidaiwa kuwa, kijana mmoja asiyejulikana alifika nyumbani kwao, Kigogo Luhanga na kutaka kiroba na mtu mmoja waongozane akabebe ndizi.

Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha sana, mama mdogo wa marehemu, Doto Lucas alisema:
 “Siku ya tukio ambayo ni Alhamisi iliyopita (Machi 12), kijana mmoja ambaye hakuna aliyemfahamu alikuja hapa nyumbani na kumtaka mtu mmoja na kiroba ili akachukue ndizi ambazo kuna mtu aliagiza ziletwe.

“Marehemu ndiye aliyekuwa karibu akijisomea baada ya kutoka shuleni. Mtu mkubwa aliyekuwa nyumbani muda huo ni bibi wa marehemu ambaye ni mtu mzima hivyo alimwambia Irene aongozane na mtu huyo akachukue mzigo akijua uko jirani kwa mujibu wa mtu huyo.

“Baada ya muda, yule kijana alirudi akiwa peke yake na kusema anataka chombo kingine cha kubebea kwa kuwa kile kiroba kilikuwa hakitoshi.“Bibi mtu alimuonesha ndoo kwa vile hakukuwa na kiroba kingine, alipoitwaa na kuondoka nayo ndiyo  hakurudi yeye wala Irene.

“Baada ya kuona muda unayoyoma bibi wa marehemu alianza kupata wasiwasi. Ndipo akatutaarifu kilichotokea nyumbani na sisi tukaanza kumsaka Irene na kijana yule.”

KWA NINI WALIMWAMINI KIJANA HUYO?
“Sisi tuna makaka zetu wakubwa ambao wana kawaida ya kutuagizia mizigo mbalimbali kwenye magari, kwa hiyo tuliamini ni wao. Lakini tulipowapigia simu na kuwaeleza tukio hilo wote walikanusha kuwa si wao na kushangaa.

“Kauli hiyo ilianza kututia shaka zaidi hivyo tulianza kuwasiliana na ndugu na jamaa ambao wote waliishia kushangaa. Tukaenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi, Kigogo na kuanza msako wa kumsaka binti yetu pamoja na mtuhumiwa.”

IRENE APATIKANA AKIWA AMEUAWA
Mwanamke huyo anaendelea kusimulia: “Kesho yake asubuhi  (Ijumaa) tukasikia kuna binti amekutwa ameuawa kinyama kwenye Bonde la Mto Msimbazi, eneo la Sukita. Tulipatwa na mshituko, tukaenda na kuukuta mwili, tulipoukagua tuligundua ni Irene.

“Alikuwa ameharibiwa vibaya. Sehemu za mwii alikuwa na damu, alichomwa na kitu chenye ncha kali. Kwa vyovyote yule kijana alikuwa na wenzake, walimteka huko mbele ya safari na kumbaka kabla ya kumuua. Inauma sana jamani.”

Marehemu Irene ambaye katika mazishi yake wanafunzi wenzake walikuwa wakilia sana, alizikwa Jumamosi iliyopita katika Makaburi ya Mburahati, Dar.

Katika ibada hiyo, Katekista aliyesaidiana na paroko kuendesha ibada hiyo aliyetajwa kwa jina moja la Henjewele aliwalaani vikali walioshiriki kufanya unyama huo na kuwataka wafanye toba haraka iwezekanavyo na kumrudia Mungu wao vinginevyo laana na moto wa milele utawaangukia.
Mungu ailaze roho ya marehemu Irene mahali pema peponi- Amina

Wednesday, March 11, 2015

PICHA ZA TUKIO ZIMA LA AJALI YA BASI LA MAJINJA ILIYOUA WATU 42 MAFINGA HUKU IRINGA PAMOJA NA MAJINA YA BAADHI YA WALIFARIKI

 Miongoni mwa manusura 22 wa ajali ya basi la Majinja lenye namba za usajili T438 CED wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa Iringa kwa matibabu. Abiria 42 wamepoteza maisha katika ajali hiyo. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Barabarani mkoa wa Iringa, Salim Asas Abri (kulia) akiwa na viongozi wengine wakiwajulia hali manusura wa ajali hiyo.
Kontena lilokuwa limepakiwa katika lori la mizigo Scania namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company likiwa limelalia juu ya basi lenye namba za usajili T438 CED, mali ya kampuni ya Majinja. 

Kontena lilokuwa limepakiwa katika lori la mizigo Scania namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company likiwa limelalia juu ya basi lenye namba za usajili T438 CED, mali ya kampuni ya Majinja. 
 
 Kontena likiwa limelalia basi
 Foleni ya magari katika eneo la Changarawe baada ya ajali hiyo. 
 
 Wananchi wakiwa eneo la tukio


Basi likiwa limelaliwa
 
 Basi likiwa eneo la tukio
 
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza  (wa  pili kulia) akiwa na Kamanda  wa Polisi mkoa wa Iringa  Ramadhan Mungi ,Mwenyekiti wa kamati ya  Usalama Barabarani mkoa wa Iringa  Salim Asas Abri (wapili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya  Mufindi, Mboni Mhita eneo la ajali



Hivi ndivyo Basi la Majanja linavyo onekana mara baada ya kuondoa Lori lilikuwa limekandamiza basi hilo. 
 

 Umati wa watu mbalimbali wakiwemo wasafiri wasafiri waliokuwa katika mabasi mengine wakiwa wamejaa kushuhudia Ajali hiyo.


Shughuli za uokoaji zikiwa zinaendelea



Simanzi  ilitawala  katika Hospitali ya Wilaya ya Mafinga wakati maiti zilizopatikana kwenye ajali mbaya iliyotokea mapema leo asubuhi,maeneo ya Changarawe,Mafinga Mkoani Iringa,zikiwasili.
  
 Zaidi ya 45  wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyohusisha Lori la Mizigo na Basi la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam.
Ni majonzi kwa kila alefika kwenye hospitali hii.
Sehemu ya Wasamalia na Mafundi waliosaidia kazi ya kuyatenganisha magari hayo wakiangalia kama kuna watu waliosalia kwenye basi lililopata ajali leo kwa kugongana na kuangukiwa na lori la Mizigo.
 Lionekanavyo basi hilo kwa nyuma.
Basi hilo linavyoonekana baada ya ajali hiyo ambayo imeleta majonji makubwa sana kwa Taifa.
Kontena la Lori hilo likiwa limewekwa pembeni baada ya kuondolewa kwenye eneo la Ajali.


Muonekano wa Basi la Abiria na Lori yaliyo athirika kwa ajali hiyo




Mashuhuda


Basi la Abiria likiwa katika Hali mbaya baada ya ajali


Waokoaji wakiwa wanaendelea kufanya ushirikiano namna ya kuwasaidia watu waliopata ajali hiyo.


Miongoni mwa watu wakiwa wanatazama namna Magari hayo yalivyopata ajali
  



 

Askari wa usalama Barabarani wakiwa wanahakikisha watu mbalimbali waliodhurika katika ajali hiyo wanaweza  kupata msaada/huduma kwa haraka.


 Basi lililokuwa limebeba abiria waliokuwa wakitokea Mbeya kuelekea Dar es salaam  Lenye namba za usajili T438 CDE likiwa katika hali mbaya. 

Watu 42 wamefariki maeneo ya Changalawe mji mdogo wa Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa baada ya basi la abiria lililokuwa likitokea mkoani Mbeya kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limetokea Dar es Salaam.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema tukio hilo limetokea  leo majira ya 09:30 asubuhi ikihusisha basi namba T:438 CDE likitokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam na lori aina ya Scania namba T:689 APK lililokuwa likiendeshwa na dereva Sebastiani Mgama likitokea Dar es Salaam kuelekea Mbeya.

Kamanda Mungi ameongeza kuwa kati ya watu 42 waliofariki kwenye ajali hiyo wanaume ni 33,wanawake 6 na watoto 3 huku maiti nane zimeshatambuliwa na ndugu zao na kuchukuliwa kwa ajili ya shughuli za mazishi.

Aidha amesema maiti hizo zilihifadhiwa  kwa muda katika kituo kidogo cha afya cha Mafinga na kisha kuhamishiwa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa pamoja na majeruhi 22 wa ajali hiyo ambapo waliojeruhiwa kidogo wataendelea kupata matibabu katika kituo cha afya cha mji mdogo wa Mafinga.

Kamanda Mungi amesema kuwa katika eneo hilo kuna bonde na uchakavu wa barabara,kutokana na mwendo kasi wa dereva wa lori ambaye alikuwa akijaribu kulikwepa shimo lililokuwa katikati ya barabara kabla ya kupishana na basi la abiria.

Amesema kufuatia hali hiyo ikasababisha kupoteza mwelekeo kisha kontena lililokuwa limebebwa na lori hilo kuliangukia basi la abiria ambalo kwa muda huo lilikuwa karibu na lori hilo.

Hata hivo Kamanda Mungi amesema taarifa zaidi zitatolewa kesho Machi 12 ,2015  ambapo pia ametoa wito kwa wamiliki wa magari na madereva kuwa makini wawapo barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

 MAJINA YALIYOPATIKANA YA ABIRIA WALIOKUWA KATIKA BASI HILO HADI SASA NI: Baraka Ndone  (dereva), Yahya  Hassan ( kondakta), Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni, Frank Chiwango, Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine Mwate, Mwajengo, Ndulile Kasambala, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule na Dominick Mashauri, Omega Mwakasege.   
  

Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge , Juma Sindu, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule.

Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.

Tuesday, March 10, 2015

CHADEMA WAMFUKUZA RASMI UANACHAMA ZITO KABWE HIVYO SI MBUNGE TENA NA JIMBO LIKO WAZI.



Hatimaye Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kimeshinda kesi dhidi ya aliyekuwa mwanachama wake Zitto Kabwe.


Mahakama imeamua katika hukumu yake leo kuwa Chama kinaweza kuendelea na taratibu zake.


Aidha, Mahakama imeamuru Zitto alipe gharama zote za kesi.
Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kumjadili.

Hoja yake ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.

Alidai anataka mahakama iagize kamati kuu ya CHADEMA kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa yake.

Jopo la wanasheria wa Chadema likiongozwa na Mhe.Peter Kibatala na John Mallya litaongea na wanahabari muda mfupi ujao.

Nimepita katika mitandao ya jamii hiki ndicho kimeandikwa na Wanachadema

Quote By Tumaini Makene View Post
Chama kimeshinda hila nyingine. Wanachadema wameshinda kesi mahakamani.

Kesi aliyofungua Zitto imefutwa mahakamani leo.

So Chama kinaweza kuchukua uamuzi wowote wa kinidhamu kwa kuwa hakuna zuio tena. Hakuna case.


Quote By Peter Kibatala View Post

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo hii tarehe 10 March 2015 imetupilia mbali case ya msingi iliyofunguliwa na Zitto Zubeir Kabwe dhidi ya CHADEMA. 
Mahakama Kuu (Mziray,Judge) amekubaliana na hoja zetu za pingamizi dhidi ya case hiyo kwamba ilifunguliwa bila kufuata utaratibu wa kisheria. Mahakama Kuu imeipa CHADEMA gharama zote za kuendesha case hiyo. Kwa maana hiyo hakuna shauri lolote Mahakamani kwa sasa kuhusu suala hilo.
 
The CHADEMA legal Crown is back where it belongs; Peter Kibatala, Tundu Lissu, John Mallya.
 
Tuliahidi ku-post habari hizi siku moja hata kama ingechukua muda gani, na tumetimiza ahadi yetu

Thursday, March 5, 2015

BALOZI WA MAREKANI ASHAMBULIWA KWA KISU NA KUJERUIWA VIBAYA.

Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini ameshambuliwa kwa kisu usoni na pia katika kifundo cha mkono wake na mshambuliaji aliyekuwa akibwata kuhusiana na suala la kugawanywa kwa kipande cha ardhi ya jumuiya yao.
Mara tu baada ya shambulio hilo Rais wa Marekani Barack Obama amemtakia uponaji wa haraka msaidizi wake wa zamani Mark Lippert akimuombea uponaji wa haraka baada tu ya shambulio lililofanywa wakati wa hotuba ya asubuhi.
Balozi huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa upasuaji wa zaidi ya saa mbili ingawa madaktari wamethibitisha majeraha yake hayatarishi maisha yake.
Jeraha lake limekadiriwa kuwa na sentimeta kumi na moja upande wa kushoto na ameshonwa nyuzi themanini kwenye mkono uliokatwa shambulio lililosababisha baadhi ya mishipa kushindwa kufanya kazi.Msemaji wa Ikulu ya Marekani amelaani kitendo hicho kwa nguvu zote .
Baada ya shambulio hilo maofisa wa polisi walionekana wakimrukia na kumdhibiti mshambuliaji aliyekuwa na kisu chenye urefu wa inchi kumi.
Polisi wamemtambua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 55 aitwaye Kim Ki-Jong, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya shambulio kam hilo kwa kumshambulia balozi wa Japan nchini Seoul mnamo mwaka 2010.
Mkuu wa polisi Yoon Myung na amesema kwamba wanamshikilia mtuhumiwa huyo na wanachunguza sababu ya shambulio hilo na masuala mengine kumhusu