Saturday, May 31, 2014

WAFANYA BIASHARA WANAOFANYA BIASHARA KANDOKANDO YA BARABARA WANASABABISHA AJALI

Na John Banda, Dodoma
IMEELEZWA kuwa kitendo cha wafanyabiashara ndogondogo [wamachinga]
kuzagaa sehemu za watembea kwa miguu katika maeneo ya stendi ni hatari
inayoweza kuwasababishia ajali wakati wowote.
Kauri hiyo ilitolewa na Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Dodoma SSP
Peter Sima kwenye baraza la madiwani lilifanyika jana.
Sima alisema machinga hao ambao huuza bidhaa mbalimbali zikiwemo za
masokoni katika sehemu hizo za watembea kwa miguu wakati wowote
wanaweza kusababisha ajali kutokana na watembea kwa miguu kushindwa
kupita na badala yake huwalazimu kupita kwenye barabara.
Alivitaja vituo hivyo kuwa ni kile cha Daladala jamatini, stendi ya
mkoa [oil com] naya magali ya vijijini ya Mshikamano ambako wamachinga
hao huzagaa bila hata kujali usalama wao.
Aidha aliwataka manispaa kuhakikisha wanawaelekeza machinga hao
pakufanyia biashara zao lakini badala ya kuwaacha katika maeneo hayo
ambayo ni hatari kwa maisha yao.
‘’Mhe. Meya hakikisheni wamachinga hao wanaondoka katika maeneo hayo
kwa ajili ya usalama wao na kuuwema mji safi wenye muonekano wa kuwa
jiji la sivyo tutawaondoa kwa nguvu kutokana na sheria
zinavyotuelekeza’’, alisema Sima
Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu kati ya machinga hao ambao wengi wao
hukimbia masokoni wakijazana kwenye vituo hivyo bila utaratibu na
watendaji wa manispaa ambao wanaonekana kuwashindwa maana wamekuwa
wakiachwa kuzagaa hovyo huko wakichafua madhingira katika maeneo hayo
bila kuchukuliwa hatua yoyote.


Madiwani wa Manispaa wa Dodoma wakiwa katika ukumbi wa manispaa
wakifuatilia jambo wakatiwalipokuwa kwenye baraza la kawaida la
kujadili makusanyo ya mwaka wa fedha kwa kiasi walichofikisha mpaka
hivi sasa ambapo zimebaki siku chache ili kuyawakilisha serekali kuu.

Meya wa Manispaa ya Dodoma Emanuel Mwiliko akifafanua jambo kwenye
baraza la madiwani lililokutana mwisho wa wiki kujadili juu ya
makusanyo mbalimbali ili kukamili makadilio ya mwaka huu wa fedha,
kushoto ni Naibu Meya Jumanne Ngede.

Kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma SSP Peter Sima
akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na madiwani wa manipaa ya
Dodoma lililofanya mwishoni mwa wiki hii.

No comments:

Post a Comment