Sunday, May 18, 2014

BENKI YA WANAWAKE TANZANIA [TWB] YAWANEEMESHA WAJASIRIAMALI 3000 MKOANI DODOMA, MWAKA MMOJA TANGU KUFUNGUA TAWI LAKE DODOMA



Na John Banda, Dodma
WAJASIRIAMALI mkoani hapa wametakiwa kuandika majina yao kwenya hati
za mali wanazomiliki ili kuepuka hali ngumu ya kiuchumi ambayo imekuwa
ikiwakumba watu wengi kipindi cha uzeeni.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Benki ya wanawake nchini [TWB]
Margareth Chacha alipokuwa akizungumza na wajasiriamali wa mkoa wa
Dodoma alipofika kutaka kujua namna mikopo inayotolewa na Benki hiyo
inavyowakwamua kiuchumi.
Mkurugenzi huyo alisema watanzania wengi wamekuwa katika wakati mgumu
kimaisha katika maisha ya uzeeni kutokana na kutojitambua wakati bado
wangali na nguvu za kutafuta mali  na kuzitunza  na wenzi wao wakati
umiliki ukiwa wao wenyewe.
Alisema wajasiriamali wengi hasa wanawake wamekuwa wakiandika majina
ya waume zao na watoto kwenye hati na stakabadhi za manunuzi hali
ambayo inachangia wengi wao kukosa au kuchelewa kupata mikopo kutokana
na hatua ndefu ya ushawishi ili hati hizo ziweze kutoka kwa
walioandikwa majina yao.
‘’Sasa ukute mwanaume muelewa umuombe akupe hiyo hati ukakopee
lakinikama siyo umekwama, pia kuandika majina ya watoto siyo mbaya
lakini akikua anaondoka  je wewe uzeeni utaishije, sasa hakikisha
uanajiandaa vya kutosha kwa kutumia akili si nguvu na midomo’’,
alisema
Aidha Margareth alisema Benki hiyo imekuja na bidhaa mpya ijulikanayo
kwa jina la mikopo ya maendeleo kwa ajili ya kuwanufaisha
wajasiriamali ikiwemo kuwajengea nyumba kwenye viwanja wanavyomiliki
na kutakiwa kulipa kidogokidogo, kuwanunulia bajaj, bodaboda, pik up,
mashine za kukamua alizeti na viwanja.
Baadhi ya wajasiriamali hao Neema Ally na Greace Kimaro walimpongeza
Murugenzi huyo kwa kuwajali na kufika kutaka kujua maendeleo yao
yanayotokana na Mikopo wanayopewa katika benki hiyo ya TWB ambapo pia
wameyajua mengi ambayo hawakuyajua kabla ikiwemo kulipa mkopo wa
kilimo mara baada ya mavuno.
Tawi la Benki ya wanawake Tanzania [TWB] lina mwaka mmoja sasa tangu
lifunguliwe mkoani hapa ambapo mpaka sasa lina jumla ya wanachama 3000
ambao wameshanufaika na mikopo  inayotolewa kwa masharti nafuu huku
ikitozwa liba ndogo

Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania Margareth Chacha akiwa katika
pozi la picha ya pamoja na Mwenyikiti wa Kikundi cha Wajasiriamali
chenye watu 40 Greace Kimario tawi la Rusha Roho [kulia] na kushoto
Katibu wa Tawi la ipagala lenye watu 50 Neema Ally, Mara baada ya
kumaliza kuwapongeza kutokana na mwenendo mzuri wa marejesho ya mikopo
huku kila mmoja wao akinufaka kati ya wakopaji 3000 waliopo Dodoma

Wajasiriamali wa kada mbalimbali wakimfuatilia kwa makini Mkurugenzi
wa Benki ya Wanawake Tanzania [TWB] Margareth Chacha aliyetembelea
Dodoma ili kuona maendeleo yao kibiashara na namna wanavyokuza mitaji
kutokana na mikopo wanayopata toka benki hiyo.

PICHA NA JOHN BANDA

No comments:

Post a Comment