Thursday, May 15, 2014

Kampuni ya Tanzania Business Creations Company LTD [TBCC] yapania kuwakomboa wajasriamali wa Dodoma kwa kuwapa mafunzo ya wiki nzima juu ya utengenezaji na uuzaji wa Bidhaa mbalimbali.

Sabuni za miche kama hizi ni moja ya Bidhaa zinazotengenezwa na
wajasiriamali hao katika mafunzo ya vitendo yanayoendelea katika
viwanja hivyo zikiwa katika moja ya mabokis yaliyotengezwa kwa mbao
ambayo yanatumika kezitengenezea.
Mkurugenzi wa kampuni ya Tanzania Business Creations Company LMT
[TBCC] inayojishughulisha na ufundishaji wa utengenezaji wa Bidhaa na
Ujasiriamali Elibarick Mchau akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya
wananchi wa mkoa wa Dodoma wanaoshiriki mafunzo hayo yanayofanyika
katika viwanja vya Mashujaa na yanatarajia kufungwa mwishoni mwa wiki
hii
Wajasiriamali toka maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma wakifuatilia kwa
makini mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali, ufugaji na
usindikaji wa vyakula yanayoendelea katika viwanja vya mashujaa
yaliyoandaliwa na TBCC.

No comments:

Post a Comment