Monday, March 4, 2013

AZAM FC YAIRARUA AL-NASRI YA SUDAN 5-0


TIMU ya Azam Fc, ya jijini Dar es Salaam, ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF),jana tena imeeilambisha Al-Nasri ya Sudan jumla ya Ice Cream 5-0, katika mchezo wao wa marudiano uliochezwa leo katika Uwanja wa Juba, Sudan ya Kusini.
Katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Azam waliilaza timu hiyo kwa mabao 3-1, ambapo sasa Azam imefanikiwa kusonga mbele katika katika michuano hiyo kwa kuibanjua jumla ya mabao 8-1 timu hiyo

No comments:

Post a Comment