Wednesday, March 20, 2013

KINANA AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, CHINA


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP), Ai Ping, Kinana alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Mambo ya Nje ya chama cha CPC, mjini Beijing, China, leo. Kinana ambaye aliwasili kwenye Ofisi hizo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC. 
 Katibu wa NEC ya CCM,  Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP), Ai Ping, alipowasili na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Mambo ya Nje ya chama cha CPC, mjini Beijing, China, Machi 19, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.

No comments:

Post a Comment