Tuesday, March 19, 2013

Monday, March 18, 2013 SHYROSE BHANJI, ANNA KIBIRA WAJITOSA CHANETA

Makamu mwenyekiti wa CHANETA  Shyrose Bhanji amechukua fomu ya kuwania nafasi ya mwenyekiti CHANETA ambapo atachuana na Anna Kibira kugombea nafasi hiyo ya uenyekiti. Anna Kibira alikua katibu mkuu CHANETA aliondolewa nafasi hiyo na Uongozi wa CHANETA chini ya Mwenyekiti Anna Bayi Kwa kukiuka sheria za CHANETA. Nafasi ya Makamu mwenyekiti inagombewa na Zainabu Mbiro na nafasi ya mweka hazina inawaniwa na Agness Habibu, wakati waliojitokeza kuchukua fomu za wajumbe wakiwa tisa.

Kaimu katibu mkuu wa CHANETA Rose Mkisi amesema tarehe ya kufanyika uchaguzi ipo palepale na kinachosubiriwa saivi ni usahili kwa wagombea ili uchaguzi ufanyike mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment