Monday, March 25, 2013

BREAK NEWS.KAJALA YUKO HURU.WEMA MKOMBOZI WAKE AMLIPIA FAINI YA TSH 13 M

MSANII Wema Sepetu amemlipia faini ya shilingi milioni 13 msanii mwenzake, Kajala Masanja, na kumfanya awe huru. Mapema leo, hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili mcheza filamu za Kitanzania anayefahamika kwa jina la 'Kajala Masanja' na mumewe mbele ya Hakimu 'Sundi Fimbo' kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es salaam. 
Katika hukumu hiyo 'Kajala' amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200. 
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe 'Faraji Agustino' kukumbwa na makosa ya kutakatisha fedha haramu.
Hata hivyo baada ya hukumu hiyo kutolea mahakamani hapa, mwanadada maarufu hapa Bongo anayefahamika kwa jina la Wema Sepetu' aliweza kujitolea yeye mwenyewe kiasi cha Tsh. milioni 13 kutoka mfukoni mwake kwa ajili ya kumlipia msanii mwenzake wa filamu 'Kajala' asiweze kutumikia adhabu ya kifungo hicho cha miaka 5 jela. 

Hii ni mara ya pili kwa msanii 'Wema Sepetu' kujitolea kiasi kikubwa cha fedha kusaidia msanii mwenzake.!
Kwa sasa Kajala yupo nyumbani kwao maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam pamoja na ndugu na jamaa

No comments:

Post a Comment