Sunday, March 17, 2013

BREAKING NEWS: WANACHAMA SIMBA SC WAUNG’OA UONGOZI/ RAGE NJE!

Ismail rage
Mkutano wa Dharura ulioitishwa na wanachama wa klabu ya Simba umeung’oa uongozi wa juu wa klabu hiyo unaoongozwa na Mwenyekiti Ismail Aden Rage aliyepo kwenye matibabu nchini India.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, maamuzi hayo yamefikiwa kwenye mkutano huo uliofanyika na kumalizika mchana huu kwenye ukumbi wa Starlight Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Majukumu ya kuiongoza kwa muda klabu hiyo yamekabidhiwa kwa kamati maalum inayoongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Usajili, Zakaria Hanspope na Rahma Al Kharoos. Hanspope na Bi Rahma maarufu kama Malkia wa Nyuki wataiongoza Simba mpaka pale utakapofanyika uchaguzi mkuu wa kupata viongozi wapya wa klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment