Tuesday, April 15, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA UPIMAJI WA KANSA YA KIZAZI KWA WANAWAKE WILAYANI BAHI MKOANI DODOMA

Mama Salma Kikwete akimkabidhi MKUU wa wilaya ya bahi Betty Mkwasa sanduku lenye machine ya kupimia kansa ya shingo ya kizazi kwa akinamama/wanawake wakati wa uzinduzi wa zoezi la uchunguzi wa ugonjwa wa kansa ya shingo ya kizazi wilayani bahi dodoma jana april 14, 2014.
Wakazi wa wilaya ya bahi Dodoma wakisikiliza hotuba ya  mgeni rasmi mama Salma Kikwete wakati akizindua zoezi la uchunguzi wa kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake/akinamama wilayani Bahi mapema jana.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) mama Salma Kikwete akisalimiana na wanafunzi wilayani Bahi Dodoma mara baada ya kuwasili wilayani humo kuzindua zoezi la uchunguzi wa kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake lililoandaliwa kwa ushirikiano baina ya halmashauri ya wilaya ya bahi, hospitali ya DCMC na serikali ya Uswisi, zoezi hilo lilifanyika jana April 14, 2014.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) mama Salma Kikwete akipata maelezo ya kitaalamu juu ya kansa ya shingo ya kizazi kutoka kwa Daktar bingwa wa masuala ya uzazi mkoa Dodoma Dr. Chiwanga (wa pili kushoto) wakati akitembelea mabanda ya maonesho kwenye wilaya ya bahi Dodoma wakati alipokuwa kuzindua zoezi la uchunguzi wa kansa ya shingo ya kizazi wilayani humo mapea jana.

No comments:

Post a Comment