Monday, April 21, 2014

WATU WANAODAIWA KUWA NI POLISI,MGAMBO NA JWTZ WAVAMIA SHAMBA LA MKULIMA NA KUFYEKA MAZAO YOTE

Na John Banda, Chamwino
WATU wanaodhaniwa kuwa ni migambo, polisi na wanajeshi wa Jeshi la
wananchi [JWTZ] wakiwa na Bunduki walivamia shamba la Mkulima Msafili
Khatib lenye ukubwa wa hekar 13 na Kufyeka mazao yote yaliyokuwa
shambani humo yakiwemo Mahindi yaliyokuwa yamekomaa na kuchoma vibanda
2 kwa moto wa Petrol na kuiacha familia hiyo ikikosa makazi na
chakula.
Tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Chenene Walayani Chamwino
Dodoma Wiki iliyopita linahusishwa na viongozi wa kijiji hicho akiwemo
Afsa Mtendaji Ester Mhwaji na Mwenyekiti wa Kijiji Gilbert Chitung’ati
Akiongea kwa Masikitiko kuhusiana na Tukio hilo Khatib alisema April
14, 2014 saa 9 alasili Dk chache baada ya kutoka kuzozana na Afsa
mtendaji aliyekuwa akimlazimisha Mmoja wa Maofisa Toka Wakala wa
Barabara aliyefika kumsainisha ili baada ya mavuno alipwe fidia ya
shamba lake.
Alisema yeye akiwa hapo shambani alishtukia kundi kubwa la watu
wanaokadiliwa zaidi ya 30 wakiwa na mapanga na mafyekeo huku watatu
kati yao wakiwa na Bunduki mkononi walifika na kuanza kufyeka mazao
yake huku wakimkejeli nay eye awasaidie kazi hiyo walipomaliza azma
yao na kuhakikisha wamechoma kwa moto wa petrol vibanda 2 walivyokuwa
kitumia kwa makazi wakaondoka.
‘’Walifika watu hao na watatu kati yao walikuwa na Bunduki mkononi,
waliokua wamevalia sale za polisi, za jeshi la wananchi [JWTZ] na za
mgambo huku wengine walivaa za kawaida kitendo hicho kimenitia
umasikini na kunifanya niishi kama wanyama na familia yangu yenye
watoto 5 kwa kukosa pa kulala na chakula kwani tayali mahindi
yalishakomaa na tulikuwa tunayala’’, alisema
Naye Meresiana Kalunju Mke wa mkulima huyo alisema tukio hilo
lilitokana na chuki za viongozi wa Serikali ya kijiji hicho cha
Chenene Afsa mtendaji na Mwenyekiti ambao kwa makusudi waliamua
kumlazimisha Mumewe akubali fedha za fidia ya shamba hilo zipitie
mikononi mwao ndipo azipate na alipokataa wakaamua kumkomoa kwa njia
hiyo.
Alisema mtendaji aliwaambia eneo hilo lipo sehemu ya hifadhi hivyo
watu wa maliasili watafika mashambani  na watakachokifanya  wawaache,
lakini cha kushangaza wamefyeka mazao yao tu huku wakiacha mashamba
mengine  yaliyozunguka shamba lao likiwemo la Mjumbe wa kamati ya
Misitu John Selemani  kisa wachina wamechagu eneo hilo ili kujenga
kiwanda cha Kokoto.
‘’Mwandishi tusingeweza kukubali fedha hizo zipitie mikononi mwa
viongozi hao kwa sababu mwezi wa pili mwaka huu Kampuni ya kichina
iliwaliwapa viongozi hao malipo ya eneo la mashamba ya wananchi ili
waweke makambi yao kwa ajili ya ujenzi wa barabara, chakushangaza
mtendaji akali watu 70,000 kwa heka moja na wengine kulipwa 200,000
heka 5 tukalalamika ndiyo sababu Tanroad wamekuja kusimamia ulipaji
huu’’,alisema
Aidha alisema shamba hilo la hekari 13 lifanyiwa udhamini  siku hiyo,
waliambiwa kati ya mwezi wa 6,7 watakapovuna ujenzi wa kalai la
kusagia kokoto utafanyika mara baada ya kulipwa na ofisi ya Wakala wa
Barabara kwa mkataba wa miaka 3 baada ya hapo watarudishiwa maeneo
yao.
Akizungumzia tukio hilo Afsa Mtendaji wa kijiji hicho Ester Mhwaji
alisema ameshtushwa na tukio hilo na Vilevile anasikitishwa na meseji
ambazo alipokea zikimuonya kutokubali Mkulima huyo kulipwa fidia ya
mazao na Aridhi jambo ambalo aliamua kuliwekla wazi kwa wathamini
waliotoke manispaa.
‘’Tulipomaliza na Yule Mthamini tuondoka na baadae nikajulishwa juu ya
tukio hilo, na vitisho vikafuata toka kwa wakulima  nikiambiwa
nitachomwa mishale na usiku nisitoke kujisaidi la sivyo nitauawa hali
iliyonifanya kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi’’
‘’,Lakini Nimeshangazwa sana na kwa ajili ya usalama wangu naomba
nisiwataje lakini hapa nina ujumbe wa maandishi kwenye simu ulionionya
nisikubali mkulima Msafili Khatib Alipwe fidia, lakini pia sina cha
kufanya maana jioni ya siku hiyo nilipokea ujumbe wa simu toka namba
nisiyoijua ukinijulisha kuwa misitu wamefyeka mazao Chenene na Solow,
na kwanini wafyeke mazao yaliyopo shamba moja tu?’’, alihoji Ester
Mwenyekiti wa kijiji hicho Gilbert Chitung’ati alisema hawezi
kuzungumzia swala hilo hata kama halikupitia ofisi ya mtendaji kwa
sababu lilitokea ngazi za juu.
 Mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino alisema huyo mkulima ni haki yake
kulipwa fidia na kwa kuwa ndiyo kwanza amelipata atalifuatilia ili
ajue nani na kwanini wamefyeka ndipo atachukua hatua juu ya tukio
hilo.
Kampuni ya Kichina ya Chico iliyoweka kambi katika kijiji hicho cha
Chenene ndiyo iliyopewa tenda ya kuchonga Barabara ya kiwango cha Lami
kati ya kijiji mtungutu na babati.

No comments:

Post a Comment