Tuesday, April 29, 2014

WALIOPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI YA BASI LA SUMRY MKOANI SINGIDA WAFIKIA 22.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiieXA8f0qZ_ehRoyI62TOqh8KFsxPU1WmWjCC8YugiIKChWkTXClfCWG2Pg3nlaVcxCFi0CleTUoK8yukQCE1CxIiJ7bCahHA39miq4y_oYbJ91XN89UP3tXvXSaU9eVNY-TL3me-YIhPZ/s1600/AJALI+YA+BASI+LA+SUMRY+DAR-MNZ+BARABARA+KUU+DODOMA-MOROGORO+PIX+NO+5.JPGWATU 22 akiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida usiku huu. 
Ajali hiyo imetokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 22 kupoteza maisha eneo hilo. 
Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida. 
Miili 22 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi 18 waliopelekwa hospitalini hapo.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

No comments:

Post a Comment