Sunday, December 1, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHEREHESHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwai, chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Angela Ramadhan, wakati alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahi na mtoto Samir Isagetee (miezi 7) akiwa na Mama yake, Lilian Amani, wakati alipotembelea katika Banda la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi NACOPHA, katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Mtoto huyo ni mmoja kati ya watoto waliozaliwa na wazazi wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na yeye kuzaliwa salama. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda katika maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment