Saturday, November 30, 2013

1331 WAHITIMU FANI MBALIMBALI KATIKA CHUO CHA SERILALI ZA MITAA HOMBOLO DODOMA .


Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi kwa mamlaka aliyopewa akitunuku astashahada na stashahada kwa jumla ya wahitimu 1331 walihitimu fani za utawala,  usimamizi rasilimaliwatu, uhasibu na fedha na maendeleo ya jamii katika mamlaka Za serikali za mitaa, katika chuo Cha serikali za mitaa hombolo jana,  Mkuu wa Mkoa alifanya kazi hiyo kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa pili kulia ) mwenyekiti wa bodi ya chuo cha serikali za mitaa hombolo Ndg. Ramadhani  Khalfan (kulia ) , meza kuu na halaiki yote iliohudhuria mahafali ya tano chuoni hapo wakiimba wimbo wa taifa tayari kuanza mahafali.
Baadhi ya wahitimu (majina yao hayakufahamika mara  moja) wakipongezana kwa furaha baada ya kumalizika kwa mahafali ya tano ya chuo Cha serikali za mitaa hombolo jana.
Maandamano ya wanataaluma wa Chuo Cha serikali  za mitaa HOMBOLO DODOMA yakielekea viwanja vya Mahafali  chuoni  hapo kuanza  rasmi sherehe  ZA mahafali ya tano  ya chuo hiko ambapo jumla ya wahitimu 1331 walihitimu astashahada na stashahada katika fani za utawala, usimamizi rasilimaliwatu, uhasibu na fedha na maendeleo ya jamii katika mamlaka za serikali za mitaa.
PICHA ya pamoja Mkuu wa Mkoa, bodi ya chuo, uongozi wa chuo, wanataaluma na wwfanyakazi wa chuo Cha serikali za mitaa hombolo mud mfupi baada ya kumalizika kwa mahafali ya tano chuoni hapo jana.


No comments:

Post a Comment