Thursday, November 14, 2013

WAFUGAJI WILAYANI BAHI KUTOZWA FAINI ENDAPO MIFUGO YAO ITAPITISHWA BARABARANI KIHOLELA.

Na John Banda, Bahi

WAKAZI wa kijiji cha nagulo wameonywa kutopitisha mifugo yao katika
barabara bila mpangilio maalumu uliowekwa na uongozi wa kijiji hicho, la
sivyo watatozwa faini kali.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi [CCM wilayani
Bahi Mkoani Dodoma Philemon Mdate alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea
miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.

Mwenyekiti huyo alisema kumekuwa na upitishaji holela wa mifugo katika
maeneo mengi ya barabara wilayani humo hali ambayo imekuwa ikichangia
uhalibifu mkubwa ikiwemo mashimo huku usalama wa mifugo yenyewe ukiwa
hatarini.

Mdate alikuwa akisisitiza hilo mara baada ya kumaliza kuitembelea
barabara  iliyomalizika
kujengwa katika kijiji hicho cha nagulo, yenye urefu wa KM. 6 kwa
kiwango cha changalawe, huku akiwataka afisa mtendaji na Mwenyekiti wa
kijiji hicho kuhakikisha wanatenga kuwa njia pekee ya kupitishia
mifugo.

‘’Ili kuepusha uhalibifu wa barabara mwenyekiti na mtendaji tengeni eneo na
mlijenge ili mifugo yote ipitishwe hapo na mtu yoyote atakaekiuka atatozwa
faini isiyopungua 5000 kwa ng’ombe mmoja na mbuzi mmoja 2500 na msiwe na
huruma kwa mtu’’, alisema

Aidha aliwataka wananchi wote wa kijiji hicho kuilinda barabara hiyo
kutokana na kujengwa kwa gharama kubwa ya 71.6 milioni, hivyo watoe
ushirikiano wa kutoa taarifa kwa viongozi wao.

Katika ziara hiyo  Mwenyekiti huyo wa CCM Bahi alitembelea miradi mingine
ya Afya, Elimu na ofisi ya serekali ya kijiji iliyojengwa kutokana na nguvu
na gharama za wakazi wa kijiji hicho.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bahi Philemon Mdate akimkabidhi
muwakilishi wa kikundi cha vikoba kilichopo katika kijiji cha Nagulo
Sevelin Mtemba Jembe la kukokota kwa mkono lenye thamani ya 200,000
lililotolewa na mbunge wa jimbo la bahi Omari Baduwel toka kwenye
mfuko wa jimbo.
Kiongozi wa kikundi kimojawapo cha vikoba katika kijiji cha Nagulo
Elfrida Matonya akipokea msaada wa jembe la kukokotakwa mkono toka
mfuko wa jimbo uliotolewa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi Philemon
Mdate kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Bahi Omary Baduwel.
Wanachi wa kijiji cha Nagulo wakiwa kwenye mkuto wa hadhara
uliohutubiwa na mwenyekiti wa CCM walaya ya Bahi mara baada ya
mwenyekiti huyo kumaliza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kijijini
hapo.

No comments:

Post a Comment