Saturday, November 23, 2013

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MH:GEORGE SIMBACHAWENE (MB) ATUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI KATIKA UONGOZI CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM)

Naibu waziri wa nishati na madini George Simbachawene  aliyevaa joho
katikati akiwa katika picha ya pamoja na familia yake katika viwanja vya
chimwaga [UDOM] waliofika kumpongeza  baada ya kuhitimu Shahada ya
pili ya Uzamili katika uongozi
Mhitimu wa Shahada ya Uzamili katika uongozi George Simbachawene
akipiga makofi kufurahia jambo pamoja na wahitimu wenzake wakati wa
mahafali ya nne ya chuo kikuu cha Dodoma yaliyohudhuliwa na Rais
mstaafu Benjamin Mkapa ambaye ni mkuu wa chuo hicho
Mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma [UDOM] Benjamin Mkapa akiwa kwenye
mahafali ya  nne ya chuo hicho yaliyofanyika chimwaga alipohudhuria
kama mgeni rasmi na kushoto ni Mwenyekiti wa Chuo hicho DKT Juma
Mwapachu na kulia ni Makamu mkuu wa chuo hicho Idris Kikula
Wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika uongozi wakiwa katika furaha
baada ya kufikia ngazi hiyo.

No comments:

Post a Comment