Tuesday, November 5, 2013

NAM LIMITED YAFANYA KWELI ,YAKABIDHI MATREKTA YA MKOPO KWA WAKULIMA MKOANI DODOMA.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa tatu kutoka kushoto) akikata uteepe kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la kugawa matrekta ya mkopo  kwa wakulima kutoka wilaya za mkoa wa dodoma, hafla hiyo ilifanyika leo kwenye ofisi za Kampuni ya NAM Ltd mjini Dodoma ambayo inakopesha matrekta hayo kwa wakulima, jumla ya matrekta matano yenye  thamani ya shilingi 175,000,000/-  yalikopeshwa kwa wakulimaleo hii.



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akimkabidhi funguo ya trekta mkulima Kalanga Ngudong' wakai wa hafla ya kukabidhi kwa wakulima matrekta hayo ya mkopo yaliyotolewa na kampuni ya kusambaza matrekta ya NAM Ltd ya Mjini Dodoma, anayeshuhudia katikati ni mkurugenzi mtendaji wa NAM Ltd Bw. Aspenas Mwaranga, hafla hiyo ilifanyika leo mjini Dodoma.



Mkulima Kalanga Ngudong' kutoka kijiji cha Magungu Chamwino Dodoma akiwasha trekta lake alilokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (hayupo pichani) baada ya mkulima huyo kupata mkopo wa trekta hilo kutoka kwa kampuni ya NAM Ltd ya mjini Dodoma iinayokopesha matrekta hayo (NAM Truck), hafla hiyo ya kukabidhi matrekta hayo ilifanyika leo hii kwenye viwanja vya kampuni ya NAM mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment