Wednesday, November 6, 2013

BREAK NEWS:MBUNGE WA UKEREWE AKAMATWA KWA UTAPELI ASWEKWA RUMANDE.


MAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe Faustine Kashyeni,  imemuamuru Mbunge wa Jimbo la Ukerewe Salvatory Machemli pamoja na wadhamini wake watatu kwenda rumande siku 14 baada ya kuidharau mahakama kufuatia kesi ya utapeli na madai inayomkabiri.

Inatajwa kuwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita  mbunge huyo alikopa fedha kutoka kwa marafiki zake kwa ahadi ya kuzirejesha, ili kunua nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 130 ambapo alifanikiwa kulipa kiasi cha shilingi milioni 50 na akawa anadaiwa milioni 130 ambazo alipaswa kulipa kwa wakati lakini mbunge huyo hakufanya hivyo kiasi cha kuwa mtu wa kula chenga na ahadi za kesho kesho zisizotimia.

Kuona hivyo marafiki waliomkopesha fedha waliamua kulifikisha mahakamani suala hilo kwa kufungua kesi ya madai ambapo mdaiwa alikiri kuchukuwa fedha zilizotajwa.

Mara kadhaa Machemli alitakiwa kuhudhuria mahakamani lakini hakufanya hivyo hali iliyoipelekea chombo hicho ambacho ni moja kati ya mihimili ya dola kuchukuwa uamuzi wa kuwasweka rumande wadhamini wake wote watatu ambao walipaswa kumwakilisha mahakamani na hawakufanya hivyo, kisha hii leo mbunge huyo naye akakamatwa na kuwekwa ndani ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Watatu wengine walio kumbana na adhabu hiyo ni pamoja na Shelfu Ngelezya, Max Mhogo na Consolata Machemli ambao walikamatwa awali na tayari wameshamaliza adhabu zao.

No comments:

Post a Comment