Tuesday, November 19, 2013

ADENI RAGE,KIBADEN NA JULIO WATIMULIWA SIMBA ,SASA JAHAZI KUONGOZWA NA ZADROVIC NA MATOLA.


BAADA ya wanachama wa Simba kuhaha kutaka kumng’oa madarakani Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage sasa dua zao zimetimia baada ya Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kumsimamisha rasmi.

Kikao hicho kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kilifikia maamuzi hayo kutokana na madai ya kuwa kiongozi huyo wa juu wa Simba kukiuka miiko ya uongozi na kukiuka katiba ya klabu hiyo.

Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Rage kuwasainisha mkataba wachezaji wawili kutoka Zanzibar Ally Badru na Awadh Juma aliyekuwa anacheza Mtibwa.

Mabosi wa Simba wamethibitisha kusimamishwa kwa Rage na muda huu wanazungumza na waandishi wa habari sababu za kuchukua maamuzi hayo magumu.

Taarifa ya awali inadai kuwa Rage amekuwa hajishughulishi kwa karibu na timu hiyo lakini pia amekuwa akikiuka baadhi ya mambo ndani ya katiba na ndio maana kamati ya utendaji imepata nguvu ya kumsimamisha kwenye kikao hicho cha jana. 
Wakati mwenyekiti huyo na makocha wa timu hiyo, wakitimuliwa, sasa jahazi la Simba linatarajia kuwa chini ya Kocha mpya kutoka Croatia, aliyekuwa akiinoa timu ya Gol Mahiya ya Kenya, Zadravok Logarusic, ambaye atakuwa akisaidiwa na kocha msaidizi, Suleiman Matola

No comments:

Post a Comment