Wednesday, December 18, 2013

MBAKAJI AZIMIA BAADA YA KUAMBIWA ALIYEMBAKA NI MUATHIRIKA WA UKIMWI.


NewsImages/6969722.jpg
Richard Thomas

 
 
Richard Thomas, 27, alizimia baada ya polisi kumuuliza kama alikuwa anajuakuwa mwanamke aliyembaka alikuwa ni muathirika wa virusi vya ukimwi.

Thomas huku akiwa mnyonge mahakamani alihukumiwa kwenda jela miaka mitano huku akisubiria matokeo yake ya damu kujua kama ameambukizwa virusi vya ukimwi kufuatia tukio lake la kumbaka mwanamke huyo ambaye jina lake limewekwa kapuni.

Thomas alikuwa akimjua vizuri mwanamke huyo na siku ya tukio alivamia nyumbani kwake usiku na kumbaka mwanamke huyo akiwa usingizini.

Katika tukio hilo lililotokea jijini Manchester, Thomas alishtuka baada ya polisi kumwambia kuwa wanampeleka hospitali kumpima ukimwi baada ya kumkamata kwa tukio hilo la ubakaji.

Thomas aliiambia mahakama kuwa siku ya tukio alikuwa amelewa pombe na madawa ya kulevya aina ya cocaine. Mahakama iliambiwa kuwa alivamia nyumbani kwa mwanamke huyo na kumbaka huku mwanamke huyo akiwa usingizini.

Mahakama iliambiwa kuwa kwa mshtuko wa kuamshwa usingizi kwa tukio hilo mwanamke huyo hakusema kitu alimuangalia Thomas akijimalizia haja zake na kisha akaondoka zake.

"Sikumbuki vizuri nilichokifanya lakini kama anasema nimembaka nitakuwa nimembaka kweli hawezi kusema uongo", alisema Thomas katika hali ya kujuta.

Thomas amehukumiwa kwenda jela miaka mitano na miezi minne huku akisubiria matokeo yake ya HIV ajue kama kitendo chake kimempa maradhi yasiyotibika.

No comments:

Post a Comment