Monday, August 18, 2014

MKUU WA MKOA DODOMA DR REHEMA NCHIMBI AMEFUNGUA JENGO LA HUDUMA KWA WAGONJWA WA NJE (O.P.D) KWENYE KITUO CHA AFYA LUMUMA MPWAPWA LENYE THAMANI YA MIL.350

Hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la huduma kwa wagonjwa wa nje OPD kwenye kituo cha afya cha lumuma Mpwapwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki ilitanguliwa na ibada takatifu iliyoongozwa na makamu wa askofu kanisa katoliki dodoma padiri Chesco Msaga (wa pili kulia) kituo hiko cha afya kinamilikiwa na kanisa hilo kupitia shirika lake la watawa la Mt. Gema
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akiwa amembeba mtoto aliyepewa jina la Rehema na mama yake kama ishara ya kumuenzi mkuu huyo wa Mkoa kwa kuwa mtoto huyo alizaliwa kwenye kituo cha afya lumuma mpwapwa majira ambayo mkuu huyo wa Mkoa alikuwa ndio anawasili kituoni hapo kufungua jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje OPD lililogharimu kiasi cha Milioni 350 mwishoni mwa wiki.
Umati wa wananchi wa kata ya lumuma mpwapwa na maeneo ya jirani ya wilaya ya kilosa morogoro waliojitokeza kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje OPD kwenye kituo cha afya cha kata ya lumuma mpwapwa mwishoni mwa wiki
picha na JOHN BANDA

No comments:

Post a Comment