Sunday, October 6, 2013

CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA CHANG'OMBE MKOANI DODOMA WAZINDUA OFISI YAO RASMI



Katibu wa CCM mkao wa Dodoma Albart Mgumba akikata utepe kuzindua ofisi za chama hicho kata ya  Chang'mbe iliyopo chang'mbe Magharibi huku viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya mkoa, wilaya na kata.



Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Drt David Malole akiwa na viongozi wa CCM kata ya Chang'mbe walipokuwa wakimsubili Mgeni Rasmi kwa ajili ya kuzindua ofisi ya chama hicho kata ya Chang'ombe na baadae kuwahutubia wananchi.



Katibu wa CCM Mkoa Albart Mgumba akimtambulimbulisha Katibu wa umoja wa wanawake wa chama hicho [UWT] Kaundime Kasasi ambaye pia ni Mama Mzazi wa Miss Tanzania 2013 Happyness Watimanywa kwa wananchi wa kata ya Chang'ombe, kabla ya kuwahutubia wananchi hao.



Diwani wa Kata ya Chang'mbe Bakari Fundikila mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea Katika manispaa ya Dodoma akiwa kwenye Pikipiki ya mataili matatu maarufu kama bajaj yenye mashine yenye dawa ya kuulia mazalia ya mbu ambayo wameikabidhiwa miezi 2 iliyopita baada ya kukwama kusikojulikana baada ya kutolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Tangu mwaka 2011 kabla ya yeye kuwa Diwani 



Jengo la ofisi ya CCM linavyoonekana baada ya kukamilika kwaajili ya matumizi kama linavyoonekana.

katibu wa ccm mkoa wa dodoma akisalimia

No comments:

Post a Comment