Tuesday, October 22, 2013

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KUMUAGA UNCLE J, JULIUS NYAISANGA LEADERS JIJINI DAR.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah aliewahi kuwa ni mmoja wa viongozi waanzilishi wa Kituo cha Radio One, akitokea Radio Tanzania (RTD).Marehemu Nyaisangah atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma Habari pamoja na vipindi vya muziki,Matamshi yake laini na ufasaha mkubwa wa lugha ya Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji wengine.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwasa ambaye alifanya kazi pamoja na Marehemu Julius Nyaisangah akitoa heshima za mwisho.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.

No comments:

Post a Comment