Friday, October 25, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AHITIMISHA MAFUNZO YA WATENDAJI WA CCM MJINI DODOMA.


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Mweneyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipowasili Makao Makuu ya CCM, Jengo la White House, mjini Dodoma, kufunga mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mikoa, jana, Oktoba 24, Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula.
 Mweneyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akionyesha kuwa mwenye furaha, alipowasili ukumbini kufunga mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mikoa, jana, Oktoba 24, 2013 mjini Dodoma. Mafunzo hayo yaliyokuwa ya siku nne yalifunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 Ukumbi ukilipuka kwa mbinje, nderemo na vifijo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipowasili ukumbini, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma kufunga mafunzo ya watendaji na viongozi wa CCM.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, baada ya kuwasilini ukumbini na kulakiwa kwa shangwe na wahitimu wa mafunzo kwa wa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya nchini mjini Dodoma, jana, Oktoba 24, 2013.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya watendaji na viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mikoa hapa nchini, mjini Dodoma , jana , Oktoba 25, 2013. Kushoto ni Kinana na Kulia ni Mangula.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akizungumza namna mafunzo hayo yalivyoandaliwa na Idara yake ya Itikadi na Uenezi na kumalizika kwa mafanikio makubwa.
 Baadhi ya viongozi wa Jumuia na Sekretarieti wakiwa ukumbini
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akitazama bango jipya la picha za wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, baada ya mabango hayo kugawiwa kwa washiriki wa mafunzo hayo ukumbini, wakati wa kufungwa mafunzo hayo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
 Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye akihamasisha baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kifunga mafunzo hayo.

No comments:

Post a Comment