Saturday, October 19, 2013

MATUKIO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA DODOMA.

Mwanafunzi wa ufundi na udereva kutoka VETA Dodoma Ndg. Mzungu Peter akimuonesha mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi  (kushoto) mfano wa kifaa kinachoonesha namna mifumo mbalimbali iliyopo kwenye magari inavyofanya kazi . Maonesho haya yalifanyika wakati wa serehe za maadhimisho ya wiki ya usaama barabarani mkoa wa Dodoma iliyofanyika leo mjini Dodoma.

Askari wa usalama barabarani Athuman Rashid (kulia) akimwelezea mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi  (kushoto) namna kifaa maalum cha kupimia mwendokasi wa vyombo vya usafiri brabarani  kinavyofanya kazi, maonesho haya yalifanyika wakati wa sherehe za usalama barabarani leo mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment