Saturday, October 26, 2013

MKE WA MWANAJESHI WA JWTZ AOMBA MSAADA ILI KULEA WATOTO WAKE MAPACHA WA 3.


Na John Banda, Dodoma
MWANAMKE wa mwanajeshi aomba msaada kwa wasamalia wema ili aweze kuwahudumia watoto wake kwa chakula mavazi na elimu kutokana na ugumu wa maisha kiasi cha kushindwa kupata hata lishe ya kuwapa mapacha watatu aliojifungua kinyume na matarajio yake.
Mwanamke huyo Rehema Khamis [30] mkazi wa mkalama kata ya makulu manispaa ya Dodoma aliomba msaada huo baada ya kuona toka ajifungue watoto hao watatu imefika wakati ameshindwa kuwapatia hata uji wenye lishe huku mshahara wa Mumewe ukiishia kwenye madeni.
Rehema alisema  alijifungua watoto hao wa kiume wawili na wa kike mmoja Hassan, Husen na Hasanati katika hospitali ya Rufaa ya Dodoma na sasa wanakaribia kuwa na umri wa mwaka mmoja aliowachisha kunyonya wakiwa na miezi 7 kutokana na kukosekana maziwa.
Alisema hakutarajia kupata watoto watatukwa mpigo kutokana na tayali alishakuwa na wengine wawili hivyo alijua akipata mmoja angepumzika kuzaa ili ajipe nafasi ya kuwalea, hivyo kutokana na watoto hao kuhitaji chakula, mavazi na hata elimu kwa hao wakubwa imekuwa ni sababu ya kuhitaji msaada.
‘’Watu wa kada mbalimbali wamekuwa wakifika kuwaona watoto hawa lakini ni kama uwanja wa \maonyesho na kutaka kuniona mama yao wakishatuona wanaondoka lakini si kwa kuleta msaada wowote hivyo naomba wenye uwezo na moyo wanisaidie ili niweze kuwapa malezi bora’’,alisema Rehema.
Nae Baba wa watoto hao Abubakari Ally Hamad Mwanajeshi wa ajira mpya katika jeshi la wananchi wa Tanzania [JWTZ] kikosi cha 673 Msalato Dodoma alisema mahitaji yamekuwa hayatoshelezi kutokana na mshara anaopata kuishia kwenye madeni ambayo amekuwa akikopa kwa wanajeshi wenzake.
Alisema pesa hata madeni hayo ambayo amekuwa akikopa hayatoshelezi mahitaji ya watoto hao ambao hata hivyo hahitaji kuongeza wengine, hata hivyo aliwataka watu mbalimbali zikiwemo taasisi za kiserikali kumsaidia kutokana na watakavyojaliwa na mwenyezi mungu ili aweze kuwa tunza watoto wake.
Kwa upande wake Ofisa mtendaji wa kijiji cha makulu Namsfu Mihungo alisema wao kama serekali wanajitahidi kufikisha ujumbe kwa watu kuhusu familia hiyo kuhitaji msaada na kufika kuwaona lakini hawakujua kama hakuna msaada unaotolewa, hivyo watajipanga kuona nini watafanya ili kuisadia familia hiyo kwa kadili watakavyoweza.




Rehema Khamis akiwa na watoto wake mapacha watatu na dada yao ambapo hata hivyo kaka yao hakuwe mwenye umri wa miaka 13, mama huyo anahitaji msaada ili aweze kuwatunza kuwalea




Rehema Khamis [30] akimlisha uji mtoto mmoja kati ya mapacha watatu huku wengine wakisubilishwa mpaka wakwanza amalize  kutokana na mama huyo kukosa mtu wa kumsaidi kuwalea watoto hao.

No comments:

Post a Comment